Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya

Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya

Not true wasiojulikana waliibuka zamani sana. Sema mitandao umeifahamu Juzi tu. Unamfahamu dokta aliyetekwa akang'olewa kucha kisa kuongoza migomo kwa madokta nchini enzi za JK
Yeye ndio aliunda watu wasio Julikana huyu mama anaendeleza .
 
Not true wasiojulikana waliibuka zamani sana. Sema mitandao umeifahamu Juzi tu. Unamfahamu dokta aliyetekwa akang'olewa kucha kisa kuongoza migomo kwa madokta nchini enzi za JK
Ilikuwa nadra ila awamu ya tano na hii kama za kigaidi
 
Mashekhe wakikamatwa mnashangiia namimi nasema ilikuaje wamemkosa huyo
 
Ndo nataka ujue hilo. Vizuri kama umejua sasa acha kuleta utoto kwa watu wazima.
Watu wazima wanatukanana kwenye dunia yako.

Kwenye dunia yetu, kukosolewa au kupishana hoja ni sehemu ya mjadala.

Sivunjil watu heshima humu, kama umesoma majibizano yetu na Kalamu huyo ni taahira. Ugomvi wetu tunaujua wenyewe

Vinginevyo situkani watu humu

Anza na hoja kinzani, kabla ya kutukana watu humu,
 
Kuna mipaka ya uzushi jamani!! Kuwahusisha watu au taasisi Fulani bila ushahidi ni hatari Kwa jamii. Hizi ni tetesi tu, hivyo kuibebesha serikali lawama Kwa tukio ambalo halijathibitishwa ni ushahidi wa namna baadhi ya watu mlivyo tayari kutumia Kila jambo kama silaha ya kisiasa. Tusiwe Taifa la hisia, Bali la hoja.
Hoja zipi hizo Bwana Juma wakati CCM hawataki kujibu na kuishia kupiga na kuteka watu kama sote tunavyoshuhudia now haya matukio?
 

Hofu kubwa imetanda kufuatia tukio la kuvamiwa na kujeruhiwa kwa Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania (TEC) Padri Dkt.Charles Kitima.

Kupitia mitandao ya kijamii, imeripotiwa kuwa watu Wasiojulikana walimvamia Dkt Kitima majira ya saa 3 usiku wa April 30, 2025 na kuanza kumshambulia wakati akiwa kwenye makazi yake yaliyopo Ofisi za Baraza la Maaskofu (TEC) Kurasini, Dar Es salaam.

Mashuhuda wa tukio hilo waliokuwa eneo la tukio lililozungukwa na mgahawa walisema kuwa Padri Dkt Kitima ikiwa ni utamaduni wake wa kupita na kusalimu watu katika mgahawa mmoja eneo hilo, ghafla walitokea watu Wasiojulikana na kuanza kumshambulia kwa sekunde chache na kisha kuondoka.

Padri Kitima alijeruhiwa maeneo mbali mbali ya Mwili maana alikuwa akivuja damu katika sehemu mbalimbali za mwili wake na haijulikani alijeruhiwa na kitu Gani.

Mara baada ya shambulizi hilo, Dkt Kitima amepatiwa matibabu ya awali kwenye Kituo kidogo cha afya cha TEC kilichopo eneo hilo.

=====
UPDATES:

Polisi wadai kumshikilia mmoja: Polisi: Tunamshikilia Mtu mmoja kutokana na tukio la Padri Kitima kushambuliwa

=====
TAARIFA ZA AWALI:

"Tumepokea taarifa muda huu kuwa Father Dr Charles Kitima ameshambuliwa usiku huu nyumbani kwake na kujeruhiwa vibaya - hali yake si nzuri

Tunaendelea kufuatilia hii taarifa ila ieleweke kuwa shambulio kama hii hatuwezi kuchukulia kama bahati mbaya "

Ameandika hivyo Maria Sarungi kupitia mtandao wa X.

Ikumbukwe Padre Charles Kitima ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Kama hizi ni taarifa za kweli, ni nini hatima ya hali hii inayoendelea nchini?

CCM mnataka kutupeleka wapi kama taifa?

View attachment 3321209

View attachment 3321207
Official closure of the awamu ya 6. Ni ujinga sana wamefanya.
 
Ukiacha utabiri .. mtu mmoja alohusika kwenye shambulio ashakamatwa ... Endelea na utabiri kiongozi 😂😂😂
huyo ni mtuhumiwa tu, nani kasema amehusika?

Polisi wanavyosema mtu mmoja kakamatwa kuhusiana na hilo tukio haimaanishi wamekamata muhalifu husika.

kuna uchunguzi na majojiano(reid interrogation technique) husaidia kubaini muhusika ila muda mwingine havisaidii maana it happens some criminals play smarter than detectives
 
Naendelea kusisitiza CCM ni Chama Cha Majambazi.

Hata JPM siku za mwisho alianza kupambania maisha yake lakini waoi, ndiyo hivyo hovyo kwa Chama Cha Majambazi!
 
Najua uzi huu hautadumu na leo mods mtapambana kuzima kila uzi utakaohusu kupigwa kwa Padri Dr. KITIMA ila sisi Wakatoliki tupo tayari na tunasubiri tamko rasmi.

Tunasubiri tamko la viongozi wetu na tupo tayari kuitii Mamlaka yetu ya Kanisa kanisa moja la mitume. Kanisa katoliki.

Tunajua mtaleta blah blah na kuleta movies kama yule Mkenya wa kipindi kile ila kama Kanisa litafanya uchunguzi na kutupa majibu washirika wake.

napenda kutoa wito kwetu wakatiliki twemde kwenye Jumuia kwa wingi kuanzia Jumamosi hii na zingine kwani huko tutapata maelekezo rasmi ya Kanisa.

Mwenye namba na mawasiliano ya Steve Mengele atuwekee humu. Mfikishieni ujumbe ajipange kwani tunakuja.
 

Attachments

  • 1746044096666.jpg
    1746044096666.jpg
    192.4 KB · Views: 22
Kitendo cha kushambuliwa kwa Padri Dkt. Charles Kitima katika makazi yake, kama inavyoripotiwa, ni tendo la kishenzi linalohitaji kulaaniwa na kila mtu anayeipenda amani na utulivu wa Taifa letu la Tanzania. Hili sio suala la uhalifu wa kawaida, bali ni kitendo chenye nia mbaya ambacho kinaweza kuathiri umoja na mshikamano wa jamii yetu.
Naiomba Jeshi la Polisi la Tanzania (@tanpol) kufanya uchunguzi wa kina na wa haraka, na kutoa taarifa kwa umma kwa wakati ufaao. Natarajia kwamba wahusika wote waliotekeleza kitendo hiki watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria za nchi yetu. Kitendo hiki ni cha aibu, kinyama, na kinaweza kusababisha athari mbaya kwa maendeleo ya amani na ustawi wa Taifa letu.
Pia, namtakia Padri Dkt. Charles Kitima apone haraka na Mungu ampe nguvu pamoja na familia yake katika kipindi hiki kigumu. Tujenge Taifa la amani, upendo, na haki kwa wote.
 
Sasa mbona kelele zilienda kwa JPM tuu?
Ubaya wa JPM umeendelezwa na Samia, sio kwamba ubaya wa Samia ndio unafuta maovu ya JPM. Hata kama alikua hafanyi yeye, kukaa kimya huku maovu yantendeka means alikua anasupport.
 
Najua uzi huu hautadumu na leo mods mtapambana kuzima kila uzi utakaohusu kupigwa kwa Padri Dr. KITIMA ila sisi Wakatoliki tupo tayari na tunasubiri tamko rasmi.

Tunasubiri tamko la viongozi wetu na tupo tayari kuitii Mamlaka yetu ya Kanisa kanisa moja la mitume. Kanisa katoliki.

Tunajua mtaleta blah blah na kuleta movies kama yule Mkenya wa kipindi kile ila kama Kanisa litafanya uchunguzi na kutupa majibu washirika wake.

napenda kutoa wito kwetu wakatiliki twemde kwenye Jumuia kwa wingi kuanzia Jumamosi hii na zingine kwani huko tutapata maelekezo rasmi ya Kanisa.

Mwenye namba na mawasiliano ya Steve Mengele atuwekee humu. Mfikishieni ujumbe ajipange kwani tunakuja.
Ni vibaka wa Samia hawa na polisi hata wakisema nini hawataaminika.
 
Back
Top Bottom