Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya

Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya


Hofu kubwa imetanda kufuatia tukio la kuvamiwa na kujeruhiwa kwa Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania (TEC) Padri Dkt.Charles Kitima.

Kupitia mitandao ya kijamii, imeripotiwa kuwa watu Wasiojulikana walimvamia Dkt Kitima majira ya saa 3 usiku wa April 30, 2025 na kuanza kumshambulia wakati akiwa kwenye makazi yake yaliyopo Ofisi za Baraza la Maaskofu (TEC) Kurasini, Dar Es salaam.

Mashuhuda wa tukio hilo waliokuwa eneo la tukio lililozungukwa na mgahawa walisema kuwa Padri Dkt Kitima ikiwa ni utamaduni wake wa kupita na kusalimu watu katika mgahawa mmoja eneo hilo, ghafla walitokea watu Wasiojulikana na kuanza kumshambulia kwa sekunde chache na kisha kuondoka.

Padri Kitima alijeruhiwa maeneo mbali mbali ya Mwili maana alikuwa akivuja damu katika sehemu mbalimbali za mwili wake na haijulikani alijeruhiwa na kitu Gani.

Mara baada ya shambulizi hilo, Dkt Kitima amepatiwa matibabu ya awali kwenye Kituo kidogo cha afya cha TEC kilichopo eneo hilo.

=====
UPDATES:

Polisi wadai kumshikilia mmoja: Polisi: Tunamshikilia Mtu mmoja kutokana na tukio la Padri Kitima kushambuliwa

=====
TAARIFA ZA AWALI:

"Tumepokea taarifa muda huu kuwa Father Dr Charles Kitima ameshambuliwa usiku huu nyumbani kwake na kujeruhiwa vibaya - hali yake si nzuri

Tunaendelea kufuatilia hii taarifa ila ieleweke kuwa shambulio kama hii hatuwezi kuchukulia kama bahati mbaya "

Ameandika hivyo Maria Sarungi kupitia mtandao wa X.

Ikumbukwe Padre Charles Kitima ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Kama hizi ni taarifa za kweli, ni nini hatima ya hali hii inayoendelea nchini?

CCM mnataka kutupeleka wapi kama taifa?

View attachment 3321209

View attachment 3321207


Wanaofurahia haya mwisho ni watu kuanza kulipiza. Wakatoliki hawawezi kuinamia maovu kwenye nchi na kamwe hawawezi kuwa machawa
 
Haka ka nchi sasa kanaanza kuchangamka, unajua nn kipindi cha shujaa Magu watu wote waliufyata kumbuka uchaguzi wa mkuu wa 2020 ila now uchaguzi huu wa 2025 wameibuka kambale wengi kila mtu anajaribu kutunisha msuli ngoja tuone itakavyo ishia
 
Hivi Kwa Hali hii wakatoliki watashiriki uchaguzi Kweli?
 
Ambao mpo Singida hapo kwenye utambulisho wa viongozi wa Dini kuna muwakilishi kutoka TEC?majibu kwa mwenye kujua tafadhali
 
Pabaya wapi? Who is Kitima? Mimi niko RC namfahamu vizuri sana huyo Kitima, inasemekana alikuwa analewa na wenzake hapo TEC Kurasini baada ya kikao na wenzake wa dini zingine labda aliwaudhi kwa lugha zake kama za mnyaturu mwenzake Lissu!! Who knows ngoja tusubiri upelelezi wa Polisi na uzuri amepigiwa kwenye bar ya TEC ukweli utajulikana tu.
Wewe danganya watu wajinga unafikiri kila mtu ni mjinga
 
Jamani c tulikubaliana JPM Ndo alikuwa katili mpaka watu kufurahia kifo chake na kusema mama ameiponya nchi, hii imetoka wapi tena wakuu 😎
'CCM ni ile ile' au wewe huwa unasikiliza ladha ya muziki na si kinachoimbwa?
 
Vitu vingine kuzuia inahitajika akili tu, sio nguvu.

Wajameni haya mambo ya kuumizana kwakweli watanzania atupendezewi nayo.

Nimtakie Dr Kitima a healthy recovery if he can be healed na kama kweli kaumizwa au kavamiwa.

Hoja, aijibiwi kwa rungu.
Hapa umenena
 
Samia kazi unayo,tulikwambia kemea utekaji,chukua hatua haraka,wewe ukajifanya chura kiziwa sasa angalia wanavokuchezea movie hilo.

CCM imepoteza kabisa mvuto!
CCM imepoteza kabisa ushawishi!
Njia pekee kwa CCM kuendelea kuwa hai na kuendelea kushika madaraka katika Utawala wa nchi hii ni kwa kupitia kwenye kufanya Siasa za Propaganda za Vitisho Kama hizi za kuteka watu, kuua Watu, kuwashambulia na kuwapoteza wale Watu wenye ushawishi wanaokipinga Chama hicho. Nje ya Kuendesha Propaganda za Vitisho, CCM haiwezi kubaki salama Wala haiwezi kuwa hai, LAZIMA itakufa!

Utawala wowote ule uliofitinika na ambao upo mwishoni unakaribia kuanguka na kufa, huwa ni kawaida kabisa kutokea matukio mabaya Kama haya. Watawala huwa wanakuwa wameshikwa na kiwewe, wanaingiwa na hofu kubwa, kila Mtu mwenye Fikra mbadala na anayewakosoa au kuwapinga wanamchukulia kuwa ni Mhaini anayetaka kuwapindua.
Hali Kama hii pia iliwahi kumkumba aliyekuwa Rais wa Zaire (DRC) wakati huo akiwa madarakani, Hali ambayo ilimfanya amteke hata Mkuu wake wa Majeshi General Mahele na kisha kumuua kikatili Sana Kama nguruwe pori, Mobutu alimshuku Jenerali huyo wa Jeshi kwamba alikuwa anamsaliti na kuwaunga mkono Wapinzani wake wa kisiasa.
 
CCM imepoteza kabisa mvuto!
CCM imepoteza kabisa ushawishi!
Njia pekee kwa CCM kuendelea kuwa hai na kuendelea kushika madaraka katika Utawala wa nchi hii ni kwa kupitia kwenye kufanya Siasa za Propaganda za Vitisho Kama hizi za kuteka watu, kuua Watu, kuwashambulia na kuwapoteza wale Watu wenye ushawishi wanaokipinga Chama hicho. Nje ya Kuendesha Propaganda za Vitisho, CCM haiwezi kubaki salama Wala haiwezi kuwa hai, LAZIMA itakufa!
Labda Chadema ndio imepoteza mvuto angalia siku ya tarehe 24/04/2025 pamoja na kuhamasishwa na viongozi wa Chadema waende Kisutu kukinukisha watz hawakujitokeza badala yake ni viongozi tu wa Chadema ndio walienda na wakapata kipigo cha mbwa koko.

CCM bado iko juu sana otachukuwa miaka mingi sana kuitoa madarakani na wala si vyama hivi uchwara.
 
1.Hofi ya Mungu wenu Huwa inakuaje? Inapimwaje?

2.Nipe majibu ya kipimo Cha mtu mwenye uchungu na Nchi yake .

Si ajabu Wanasiasa wanapata mbumbumbu wengi wa kuwatumikia na kuwapigania kama wewe.
Kama sa100 alivyokupata wewe
 
Tumefikia hatua ya kuona kuwa kutekana, kuuana na kufunguliana kesi nzito nzito za uongo kuwa ni kawaida.
Hayati Magufuli alaumiwe milele.
Yeye ndiye amefanya tufike hapa.
Mungu yupo karibu kuliponya taifa.
Upumbavu ni kumlaumu mfu kwa makosa ambayo yanafanywa na watu waliopo hai sasa tena kwa utashi wao wenyewe, na nyie mnaokereka mna uwezo wa kuyazuia.
 
Mmoja aliyemtembelea Father Dr.Charles Kitima anashuhudia kuwa "Hakika lilikuwa shambulio baya lenye lengo la kudhulumu maisha yake"

Mungu ni mwema sana anaendelea vizuri.

Huu ni Ujumbe wake kwetu

"....Lazima Tuwe Imara kusimamia masuala ya Msingi katika Taifa.

"Hatutakiwi kuogopa kulipa gharama katika kusimamia haki na Wajibu wetu kwa Taifa.

"Kila Mmoja atalipa gharama kwa kiasi chake na hilo lazima tuwe tayari.

"Tunapozungumzia mambo ya Msingi Kitaifa yanayotakiwa kurekebishwa ili uchaguzi ufanyike kwa haki tusiogope kulipa gharama."

Father Dr. Charles Kitima leo Tarehe 1 May 2025.
 
Back
Top Bottom