Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya

Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya

Tumefikia hatua ya kuona kuwa kutekana, kuuana na kufunguliana kesi nzito nzito za uongo kuwa ni kawaida.
Hayati Magufuli alaumiwe milele.
Yeye ndiye amefanya tufike hapa.
Mungu yupo karibu kuliponya taifa.
Kamlaumu mama yako aliyekuzaa ukiwa mjinga na mpumbafu hivi. Inaonekana ndio nyinyi mliothibitiwa na Rais Magufuli ndio maana una hasira naye sana. Acha wizi na ushoga, nyumbu mkubwa!
 
Kusema serikali ndo imehusika sidhani,Serikali ya chama cha mapindizi haijafikia huko
Sio haijafika, iko huko muda mrefu. Ni kawaida sana vyama ama kiongozi anapokaa muda mrefu madarakani, huishia kupoteza ushawishi kwa umma. Namna moja ya kuendelea kubaki madarakani, ni kutengeneza vikundi vya kihalifu ili kupoteza, hata kuua wapingaji kwa lengo la kutisha ili asalie madarakani. Mara nyingi uhalifu huu wa kidola huwa na baraka zote za dola.

Hicho ndio wanachofanyiwa kwa wapinzani wa kweli, na wanaharakati wa makundi mengine. Mtindo huu ulishika kasi sana chini ya utawala wa Magufuli, na sasa Mama Samia anatumia kama njia za kuilinda ccm na madaraka yao. Hivyo kama mnadhani kuna watu wa kupotea maboya kwa maelezo ya polisi, basi mnapoteza muda. Ingekuwa kweli ni mtu kakamatwa tungeona yakiwekwa majina yake matatu pamoja na namba yake ya NIDA. Kinyume na hapo ni hadaa za bei rahisi. Ila iwe itakavyokuwa, mabadiliko ni lazima.
 
SHIDA KUBWA HAPO NI SIASA WAKUU VYAMA VYOTE VYA SIASA VIFUTWE AU KUPUMZISHWA KWA MUDA HATA MIAKA SITA KUPISHA UCHUNGUZI WA MAUJI, UTEKAJI, UBAMBIKIAJI KESI NA USHAMBULIAJI...
 
Naomba kusahihishwa juu ya huyu Padre. Hivi siyo huyu Padre aliewahi kumwagiwa TINDIKALI na watu wasiojulikana au nimechanganya mafaili. Naomba kufagamishwa.
 
Tetesi za kushambuliwa kwa Padri Kitima na kuhusishwa kwa serikali hazipaswi kuchukuliwa kama ukweli bila ushahidi. Serikali haina sababu ya kumlenga kiongozi wa dini ambaye hana uhasama wowote wa moja kwa moja nayo. Katika mazingira ya sasa, si ajabu kuona tukio la uhalifu likigeuzwa ajenda ya kisiasa. Tuwe makini na propaganda, tusubiri ukweli ujulikane.
Nani unayemsubiri akupe ukweli...?

Kama ukweli wa Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi 37, katikati ya mji mkuu Dodoma, kwenye makazi ya viongozi wa serikali yanayolindwa masaa 24 siku zote haukujulikana mpaka tarehe 10/4 mwaka huu ndo ukajulikana kwa walewale waliomshambulia kumkamata na kumbambikia kesi ya uhaini..?

Yaani kwa tukio hili unataka kutuambia hawa mapolisi wa aina ya RPC wa DSM Jumanne Muliro ndo wakupe ukweli..?

Nani kakuroga wewe hata usiuone ukweli ulio wazi...?

Huyu si ndiye Father Kitima, mtu anayeongea kila wakati kuhusu HAKI, akipinga wizi wa kura ktk chaguzi, akitoa wito wa mara kwa mara kufanyika kwa mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi ili kuwe na chaguzi huru, wazi na za haki...?

Sasa tujiulize maswali rahisi tu yafuatayo na tukipata majibu yake kwa usahihi, utajua kuwa huhitaji kusubiri kujua ni kina nani wanafanya ushenzi huu:

SWALI #1: Kina nani wanaowachukia watu wanaodai mifumo ya haki ktk nchi hii kwenye chaguzi, mahakamani, bungeni na kwenye taasisi za umms?

JIBU: Ni CCM na serikali yao...!!

SWALI #2: Ni kina nani wanaumiza yeyote anayekosoa serikali hii na Bi Chura Kiziwi a.k.a Samia Suluhu Hassan kwa kuteka, kutesa na kuuua na kutupa miili porini.?

JIBU: Ni watu wa CCM waliovikwa magwanda ya polisi (wale walioteka watu mchana kweupe mahakamani Kisutu tarehe 24/4/2025 wakawapiga na kuwatesa, kwa kuwavunja miguu na mikono na kisha kuwatupa porini Mabwepande - Bagamoyo)

SWALI #3: Ni kina nani wanaobambikiza kesi za jinai, uchochezi na uhaini au ugaidi yeyote anayepinga sera na mipango mibovu ya serikali ya CCM, ufisadi na wizi, anayetaka reforms za mifumo HAKI ikiwemo mfumo wa uchaguzi Tanzania..?

JIBU: Ni serikali ya CCM na watu waliokwisha kuunda jeshi la siri wanalolivika magwanda ya jeshi halali la Polisi ili kufanya ujambazi na uhalifu huu wa kisiasa tunaoushuhudia ili kulinda maslahi maovu ya CCM na serikali yao...

#Mpaka hapo unataka usubiri kuelewa nini kuwa hawa ndio wahusika? Nani akupe jibu? Hawahawa wanaotenda uhalifu huu wakupe majibu..?
 
Tumefikia hatua ya kuona kuwa kutekana, kuuana na kufunguliana kesi nzito nzito za uongo kuwa ni kawaida.
Hayati Magufuli alaumiwe milele.
Yeye ndiye amefanya tufike hapa.
Mungu yupo karibu kuliponya taifa.
Samia alipoingia madarakani mlisema Mungu ameiponya nchi, eh kumbe bado au yule Mungu n Mungu gn aliyeiponya nchi wakati ule?
 
Eric Kabendera yupo anaandika kitabu kingine!
Hakuna kitu kama hicho, huyo yupo kwa ajili ya JPM tuu, sasa hv n marehemu kwahy unadhani ataandika yeye ndo amemuua mzee kibao au kumuumiza padri?
 
Back
Top Bottom