Hofu kubwa imetanda kufuatia tukio la kuvamiwa na kujeruhiwa kwa Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania (TEC) Padri Dkt.Charles Kitima.
Kupitia mitandao ya kijamii, imeripotiwa kuwa watu Wasiojulikana walimvamia Dkt Kitima majira ya saa 3 usiku wa April 30, 2025 na kuanza kumshambulia wakati akiwa kwenye makazi yake yaliyopo Ofisi za Baraza la Maaskofu (TEC) Kurasini, Dar Es salaam.
Mashuhuda wa tukio hilo waliokuwa eneo la tukio lililozungukwa na mgahawa walisema kuwa Padri Dkt Kitima ikiwa ni utamaduni wake wa kupita na kusalimu watu katika mgahawa mmoja eneo hilo, ghafla walitokea watu Wasiojulikana na kuanza kumshambulia kwa sekunde chache na kisha kuondoka.
Padri Kitima alijeruhiwa maeneo mbali mbali ya Mwili maana alikuwa akivuja damu katika sehemu mbalimbali za mwili wake na haijulikani alijeruhiwa na kitu Gani.
Mara baada ya shambulizi hilo, Dkt Kitima amepatiwa matibabu ya awali kwenye Kituo kidogo cha afya cha TEC kilichopo eneo hilo.
=====
UPDATES:
Polisi wadai kumshikilia mmoja: Polisi: Tunamshikilia Mtu mmoja kutokana na tukio la Padri Kitima kushambuliwa
=====
TAARIFA ZA AWALI:
"Tumepokea taarifa muda huu kuwa Father Dr Charles Kitima ameshambuliwa usiku huu nyumbani kwake na kujeruhiwa vibaya - hali yake si nzuri
Tunaendelea kufuatilia hii taarifa ila ieleweke kuwa shambulio kama hii hatuwezi kuchukulia kama bahati mbaya "
Ameandika hivyo Maria Sarungi kupitia mtandao wa X.
Ikumbukwe Padre Charles Kitima ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).
Kama hizi ni taarifa za kweli, ni nini hatima ya hali hii inayoendelea nchini?
CCM mnataka kutupeleka wapi kama taifa?
View attachment 3321209
View attachment 3321207
hawatashiriki kwa ujinga huu. hata hivyo no reforms no electionHivi Kwa Hali hii wakatoliki watashiriki uchaguzi Kweli?
Daa! 😢Jamani c tulikubaliana JPM Ndo alikuwa katili mpaka watu kufurahia kifo chake na kusema mama ameiponya nchi, hii imetoka wapi tena wakuu 😎
Padri Kitima ana matatizo ya afya ya akili kama Lissu. Hawa wanyaturu wana shida ya akili zao wanahitaji matibabu! 🤣sababu haimbi mama mama ndo anaonekana chadema., Kitima ni mtu wa haki
Wewe danganya watu wajinga unafikiri kila mtu ni mjingaPabaya wapi? Who is Kitima? Mimi niko RC namfahamu vizuri sana huyo Kitima, inasemekana alikuwa analewa na wenzake hapo TEC Kurasini baada ya kikao na wenzake wa dini zingine labda aliwaudhi kwa lugha zake kama za mnyaturu mwenzake Lissu!! Who knows ngoja tusubiri upelelezi wa Polisi na uzuri amepigiwa kwenye bar ya TEC ukweli utajulikana tu.
'CCM ni ile ile' au wewe huwa unasikiliza ladha ya muziki na si kinachoimbwa?Jamani c tulikubaliana JPM Ndo alikuwa katili mpaka watu kufurahia kifo chake na kusema mama ameiponya nchi, hii imetoka wapi tena wakuu 😎
.Lazima watakuwa wanafuatilia kwa umakini Sana mjadala huu, OSINT.
Mimi nadanganya nyumbu kama wewe!Wewe danganya watu wajinga unafikiri kila mtu ni mjinga
Hapa umenenaVitu vingine kuzuia inahitajika akili tu, sio nguvu.
Wajameni haya mambo ya kuumizana kwakweli watanzania atupendezewi nayo.
Nimtakie Dr Kitima a healthy recovery if he can be healed na kama kweli kaumizwa au kavamiwa.
Hoja, aijibiwi kwa rungu.
Samia kazi unayo,tulikwambia kemea utekaji,chukua hatua haraka,wewe ukajifanya chura kiziwa sasa angalia wanavokuchezea movie hilo.
Labda Chadema ndio imepoteza mvuto angalia siku ya tarehe 24/04/2025 pamoja na kuhamasishwa na viongozi wa Chadema waende Kisutu kukinukisha watz hawakujitokeza badala yake ni viongozi tu wa Chadema ndio walienda na wakapata kipigo cha mbwa koko.CCM imepoteza kabisa mvuto!
CCM imepoteza kabisa ushawishi!
Njia pekee kwa CCM kuendelea kuwa hai na kuendelea kushika madaraka katika Utawala wa nchi hii ni kwa kupitia kwenye kufanya Siasa za Propaganda za Vitisho Kama hizi za kuteka watu, kuua Watu, kuwashambulia na kuwapoteza wale Watu wenye ushawishi wanaokipinga Chama hicho. Nje ya Kuendesha Propaganda za Vitisho, CCM haiwezi kubaki salama Wala haiwezi kuwa hai, LAZIMA itakufa!
Kama sa100 alivyokupata wewe1.Hofi ya Mungu wenu Huwa inakuaje? Inapimwaje?
2.Nipe majibu ya kipimo Cha mtu mwenye uchungu na Nchi yake .
Si ajabu Wanasiasa wanapata mbumbumbu wengi wa kuwatumikia na kuwapigania kama wewe.
Upumbavu ni kumlaumu mfu kwa makosa ambayo yanafanywa na watu waliopo hai sasa tena kwa utashi wao wenyewe, na nyie mnaokereka mna uwezo wa kuyazuia.Tumefikia hatua ya kuona kuwa kutekana, kuuana na kufunguliana kesi nzito nzito za uongo kuwa ni kawaida.
Hayati Magufuli alaumiwe milele.
Yeye ndiye amefanya tufike hapa.
Mungu yupo karibu kuliponya taifa.