1. Ushoga hautangazwi bali inaweka uelewa kwa jamii sababu jamii nyingi zimekariri mapenzi ni ya Me na Ke bila kujua kuna Me na Me, kuna Ke na Ke,
2. Kuna tofauti kati ya Jinsi (Sex) na Jinsia (Gender),
Jinsi (Sex) zipo mbili tu Me na Ke mahususi kwa kuzaana lakini Jinsia (Gender) zipo nyingi sanaaaa,
Nenda kasome Sexual Orientation na Gender Identity.
3. Mtoto akiwa Shoga ajabu ni nini sasa si amechagua njia yake? Au unadhani akiwa Shoga hawezi kusoma na kufanya kazi zake?
4. Hakuna aliyelazimishwa kua Shoga au wewe unao ushahidi kuna Mtu alikuomba akufire? Kama hujawahi basi jua hakuna anayelazimishwa kilichopo ni kuweka usawa wa kibinaadam, kila Mtu awe huru kuishi katika jamii yake kwa amani as long as hatoi madhara.
5. Kama ushoga ulikuwepo tangu enzi za hekaya za Sodoma na Gomora kwanini uhisi sasa hivi kuna ajenda? As if hao unaowahisi ndio waliozalisha Mashoga? Kama unatetea Albino asiuliwe basi tetea na Shoga asiuwawe, hizo nchi zimeamua kua sauti ya wanyonge.