TANZIA Patrick Mfugale wa TANROADS afariki dunia Jijini Dodoma

Mkuu hujakosea, ulivyomuelezea ni kama alivyo.
Mfugale alikuwa mtu mwenye madaraka makubwa sana kutokana na kuendesha TANROADS, Shirika la umma lenye kutumia pesa nyingi za serikali kuliko hata wizara nyingi.

Namfahamu personally Mfugale , hakuwa mjivuni wala mtu kwa kujikweza au tamaa.
Na alikuwa makini sana kama mhandisi.
Pengine ndio maana alikaa cheo alivyokuwa nacho kwa muda mrefu.
RIP Eng Patrick Mfugale.
 
tulio baki hai tunajambo la kujifunza haswa viongozi/watendaji.

jueni kuwa cheo/vyeo ni dhamana, kamwe huwezi kuzikwa na cheo chako, uwe waziri, uwe mbunge, uwe diwani, uwe Jaji, auwe Hakimu, uwe mkurugenzi, uwe Dasi, uwe RASI, n.k n.k.

Jambo la msingi zingatieni kutenda Haki, acheni kuonea watu, fanyeni kazi kwa maendeleo ya wananchi.

R.I.P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
*"Namjua Engineer Mfugale ni mzalendo wa hali ya juu. Nakumbuka mwaka 2008 Engineer Mfugale na Engineer Mvungi walitishiwa kufukuzwa kazi kwa kusimamia ukweli na professionalism na Wakatupwa Wizarani bila kupewa kazi yoyote ya kufanya. Jinsi ninavyowsjua Wahehe kwa kupenda kujiua nilifikiri Engineer Mfugale angejiua lakini hakujiua, alivumilia.

Mwenzake, Engineer Mvungi, akajipiga risasi na kupoteza maisha!. Leo Engineer Mvungi ni marehemu kwa kupigania ukweli na hiyo ndio saa zingine gharama ya kupigania ukweli. Nikamteua Engineer Mfugale kuwa Chief Executive Officer wa Tanroads. Amejenga madaraja mengi sana nchini"*_

Hayati Dr. JPM, 28.9.2018

R.I.P Wazalendo.
 
Mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Patrick Mfugale amefariki dunia leo Jumanne Juni 29, 2021 jijini Dodoma.

Katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Joseph Malongo amesema Mfugale atakayekumbukwa kwa kusimamia ujenzi wa barabara na madaraja zaidi ya 1000 nchini amefariki dunia leo saa 5 asubuhi katika hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Amebainisha kuwa taratibu nyingine za msiba huo zitatolewa baadaye.

Taarifa zilieleza kuwa Mfugale akiwa katika moja ya kikao kazi alijisikia vibaya na kukimbizwa hospitalini ambako akiwa njiani hali yake ilizidi kuwa mbaya.

Awali Waziri wa Ujenzi, Dk Leonard Chamuliho na naibu waziri wa wizara hiyo, Mwita Waitara alieleza kuwa hawana taarifa za kifo cha Mfugale
 
Thanks, but it was a typo.
Grateful that at least there is another person apart from me who is proficient in the Queen's language in jf.
Cheers.
... inaeleweka Kiongozi. Nilitaka kucholaza tu. Typos ni kawaida sana; kuwa na amani.
 
Ila wafanyakaz wa tanrod Chini yake wanaukwasi mkubw mnoo sizani hata dereva wa tanrod tu c ajabu umkute nae anamiliki gorofa yaani
 
Pamoja na mapungufu yake ila hili jamaa lilikuwa na akili mingi sana.
 
Mbona habari haijawekwa Tag ya Tanzia kama toka asubuhi imetangazwa rasmi?
 
Yaani wewe usiku huu ndio umejua? Halafu unakimbilia hapa ku-post bila kusoma post za watu wengine! Kwa taarifa yako, hii siyo habari ngeni hapa JF.
 
Jamaa alikuwacna kisu kikali. Sijui kama ameacha kabinti nikasaidie kulinda mali alizoacha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…