Paul Makonda aitwa kwenye Kamati ya Maadili ya CCM

Wanazidi kumpa umaarufu...inaonekana wanamuogopa ndomana wanampa cheo licha ya matendo meengi yasiyofaa!!
Alafu mtu ananiambia eti niwe mzalendo!! Mzalendo huku mtuhumiwa anapewa cheo na rais nasisi watiifu tunateswa Kwa mishahara midogooo
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Ndugu Paulo Makonda ameitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi.

Ameelekezwa kufika kwenye Kamati hiyo tarehe 22/04/2024.

=====

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemuita Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kwenye Kamati ya Maadili.

Makonda anatarajiwa kufika mbele ya Kamati hiyo Jumatatu, Aprili 22, 2024 asubuhi na kukutana na wajumbe wa kamati hiyo.

Hata hivyo, Mwananchi inafahamu kuwa Makonda alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Aprili 20, 2024 majira ya asubuhi, lakini haikuelezwa sababu za kusogezwa mbele.

Barua ya wito wa CCM kwa Makonda haikueleza sababu za kumuita huku ikieleza kwamba, kuna masuala mbalimbali kati yake na wajumbe wanakwenda kujadili.

Lakini, wito huo huenda unahusishwa na kauli ya Makonda aliyoitoa wakati wa kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Waziri mkuu wa zamani, Edward Sokoine iliyofanyika Monduli, Arusha ambako Makonda alidai kuwa viongozi wakiwemo mawaziri wamekuwa wakilipa watu kumtukana Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mitandao ya kijamii.

Makonda alitoa onyo kwa viongozi hao akisema kama wakiendelea atawataja hadharani na kwamba, hayuko tayari kuona Rais Samia akitukanwa.

Chanzo: Mwananchi online

Pia soma:
Hii ndo kazkazini😋😎 ataondokA tu..
 
Maisha yanaenda kasi. Juzitu alikua anahoji hadi mawaziri leo anahojiwa na wale aliokua anawaona ni manamba tu
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Ndugu Paulo Makonda ameitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi.

Ameelekezwa kufika kwenye Kamati hiyo tarehe 22/04/2024.

=====

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemuita Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kwenye Kamati ya Maadili.

Makonda anatarajiwa kufika mbele ya Kamati hiyo Jumatatu, Aprili 22, 2024 asubuhi na kukutana na wajumbe wa kamati hiyo.

Hata hivyo, Mwananchi inafahamu kuwa Makonda alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Aprili 20, 2024 majira ya asubuhi, lakini haikuelezwa sababu za kusogezwa mbele.

Barua ya wito wa CCM kwa Makonda haikueleza sababu za kumuita huku ikieleza kwamba, kuna masuala mbalimbali kati yake na wajumbe wanakwenda kujadili.

Lakini, wito huo huenda unahusishwa na kauli ya Makonda aliyoitoa wakati wa kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Waziri mkuu wa zamani, Edward Sokoine iliyofanyika Monduli, Arusha ambako Makonda alidai kuwa viongozi wakiwemo mawaziri wamekuwa wakilipa watu kumtukana Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mitandao ya kijamii.

Makonda alitoa onyo kwa viongozi hao akisema kama wakiendelea atawataja hadharani na kwamba, hayuko tayari kuona Rais Samia akitukanwa.

Chanzo: Mwananchi online

Pia soma:
kwanza tujue ni mawaziri wepi ndio tujue nini la kufanya.
 
huyu kijana hafai kuwa kiongozi, alishawahi kuota mapembe Mungu akamshusha, hakujifunza, sasaivi amerudi na kiburi kilekile na kuaibisha watu wazima mbele za watu ili yeye apate credit. aonywaye mara nyingi na kushupaza shingo atavunjika na hata pata data. kwa kifupi, wakimuita kama watamrudisha au watamwondoa, ipo wazi, huyu ni kiongozi muonevu, kiongozi asiye na maadili na hafai kuongoza watu wazima. hata asipowajibishwa na ccm kuna siku Mungu atamwajibisha. aombe Mungu awajibishwe na ccm, manake akiwajibishwa na Mungu hawezi kustahimili kabisa.
Sisi tunaangalia kazi yake nzuri kuhusu kutetea maslahi ya umma na yenye matokeo makubwa. Kama unamchukia hapo hujasema nini ameharibu. bila shaka utakua mmoja wa watu wabinafsi na dhulumati kwa wanyonge na mali ya umma.
 
dhulumati ni wewe mkewe na makonda mwenyewe, mlitaka kumdhulumu GSM nyumba yake, mmedhulumu magari sasa hapo kati yenu na sisi nani dhulumati nyooooooo
 
Nasikia huko wanakamatana, kwa sababu kamati ya kumuhoji ina dhambi kubwa kuliko dhambi ya makonda.

Hivyo imeishia kushauriana na wala sio kumhoji kwa sababu dogo anajua dhambi zao wote.

Ccm imeoza
 
IMG-20240423-WA0056.jpg
 
Back
Top Bottom