Paul Makonda aitwa kwenye Kamati ya Maadili ya CCM

Paul Makonda aitwa kwenye Kamati ya Maadili ya CCM

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Ndugu Paulo Makonda ameitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi.

Ameelekezwa kufika kwenye Kamati hiyo tarehe 22/04/2024.

=====

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemuita Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kwenye Kamati ya Maadili.

Makonda anatarajiwa kufika mbele ya Kamati hiyo Jumatatu, Aprili 22, 2024 asubuhi na kukutana na wajumbe wa kamati hiyo.

Hata hivyo, Mwananchi inafahamu kuwa Makonda alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Aprili 20, 2024 majira ya asubuhi, lakini haikuelezwa sababu za kusogezwa mbele.

Barua ya wito wa CCM kwa Makonda haikueleza sababu za kumuita huku ikieleza kwamba, kuna masuala mbalimbali kati yake na wajumbe wanakwenda kujadili.

Lakini, wito huo huenda unahusishwa na kauli ya Makonda aliyoitoa wakati wa kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Waziri mkuu wa zamani, Edward Sokoine iliyofanyika Monduli, Arusha ambako Makonda alidai kuwa viongozi wakiwemo mawaziri wamekuwa wakilipa watu kumtukana Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mitandao ya kijamii.

Makonda alitoa onyo kwa viongozi hao akisema kama wakiendelea atawataja hadharani na kwamba, hayuko tayari kuona Rais Samia akitukanwa.

Chanzo: Mwananchi online

Pia soma:
Hakawii kulia huyu, walimwuliza Kuhusu vyeti akaanza kwenda nyumba za ibada kulialia
 
Hivi jitu linaloua watu, kutrka na kupora mali za watu, lina uzalendo gani? Huyu ni jambazi. Bahati mbaya tu nchi yetu inaendeshwa kimagumashi. Hili jitu lilistahili kuwa jela.
Mlimezeshwa sumu na wapinzani wa JPM na nyie mkameza kama zilivyo alimuua nani fungua shauri mahakamani si una ushaidi zaidi zaidi toa porojo hapa kama ni USA ndo nchi inayoongoza kwa mauji
 
Kiongozi yeyote lazima awe na marafiki na maadui pia ndani ya mifumo na nje ya mifumo. Kwa vyovyote lazima Makonda atakuwa ameshajua nini kinaendelea kama ni tuhuma na majibu yake ameshayaandaa. Hana kesi ya criminal offense, hivyo wapo walioupande wake pia. Ktk Kila uamuzi hata kama umetolewa na Rais lazima ziwepo pande mbil zitakazokuwa na mitazamo tofauti. Let always the natural justice prevail ndo maana ameitwa. Reaction ya tume itategemea accusations alizonazo atazijibu vipi, hivyo let's not pre empty the fate of the circumstance.
 
CCM na maadili wapi na wapi
Sema kamati ya madili imemuita mwana madili mwenzao.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Ndugu Paulo Makonda ameitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi.

Ameelekezwa kufika kwenye Kamati hiyo tarehe 22/04/2024.

=====

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemuita Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kwenye Kamati ya Maadili.

Makonda anatarajiwa kufika mbele ya Kamati hiyo Jumatatu, Aprili 22, 2024 asubuhi na kukutana na wajumbe wa kamati hiyo.

Hata hivyo, Mwananchi inafahamu kuwa Makonda alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Aprili 20, 2024 majira ya asubuhi, lakini haikuelezwa sababu za kusogezwa mbele.

Barua ya wito wa CCM kwa Makonda haikueleza sababu za kumuita huku ikieleza kwamba, kuna masuala mbalimbali kati yake na wajumbe wanakwenda kujadili.

Lakini, wito huo huenda unahusishwa na kauli ya Makonda aliyoitoa wakati wa kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Waziri mkuu wa zamani, Edward Sokoine iliyofanyika Monduli, Arusha ambako Makonda alidai kuwa viongozi wakiwemo mawaziri wamekuwa wakilipa watu kumtukana Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mitandao ya kijamii.

Makonda alitoa onyo kwa viongozi hao akisema kama wakiendelea atawataja hadharani na kwamba, hayuko tayari kuona Rais Samia akitukanwa.

Chanzo: Mwananchi online

Pia soma:
Mbona namwona hapo viwanja vya leaders club akiaga mwili wa Gardner Habash ambao unasafirishwa kwenda rombo kwa mazishi?
 
Mbona Mwananchi Digital wameonyesha picha ya Bashite akiwa msibani kwa Gadner hapo viwanja vya Leaders Club!

Kwamba ameshotoka DODOMA tayari?
 
Leo makonda alikuweko kwenye msiba wa Habash. Sijui anaeatafuta CMG kitu gani.
 
Wajumlishe na udhalilishaji alioufanya kwa yule muhandisi wa TARURA kwenye clip inayotembea mtandaoni kwa sasa

Kule sio kumuwajibisha mtumishi, ule ni udhalilishaji wa wazi ningekuwa mimi ningetoka ukumbini halafua aagize askari wanikamate wanipeleke ndani kesi ianzie hapo

Kuna lugha za uongozi wenye mamlaka zisizohusisha dhihaka, CCM wanatakiwa wawafundishe vijana wao.
Makonda ni bomu. Ila mimi ningekuwa mtumishi wa umma aje anga zangu pangechimbika. Bora nirudi kulima kuliko kudhalilishwa na huyu mpambavu.
 
Back
Top Bottom