Paul Makonda aitwa kwenye Kamati ya Maadili ya CCM

Paul Makonda aitwa kwenye Kamati ya Maadili ya CCM

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Ndugu Paulo Makonda ameitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi.

Ameelekezwa kufika kwenye Kamati hiyo tarehe 22/04/2024.

=====

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemuita Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kwenye Kamati ya Maadili.

Makonda anatarajiwa kufika mbele ya Kamati hiyo Jumatatu, Aprili 22, 2024 asubuhi na kukutana na wajumbe wa kamati hiyo.

Hata hivyo, Mwananchi inafahamu kuwa Makonda alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Aprili 20, 2024 majira ya asubuhi, lakini haikuelezwa sababu za kusogezwa mbele.

Barua ya wito wa CCM kwa Makonda haikueleza sababu za kumuita huku ikieleza kwamba, kuna masuala mbalimbali kati yake na wajumbe wanakwenda kujadili.

Lakini, wito huo huenda unahusishwa na kauli ya Makonda aliyoitoa wakati wa kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Waziri mkuu wa zamani, Edward Sokoine iliyofanyika Monduli, Arusha ambako Makonda alidai kuwa viongozi wakiwemo mawaziri wamekuwa wakilipa watu kumtukana Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mitandao ya kijamii.

Makonda alitoa onyo kwa viongozi hao akisema kama wakiendelea atawataja hadharani na kwamba, hayuko tayari kuona Rais Samia akitukanwa.


Chanzo: Mwananchi online

Pia soma:
Hiii imekaaje🤔😎 unajitekenya mwenyewe unacheka mwenyewe!
 
Oyooooo!
Imetulia hiyo. Huyu mropokaji abananishwe ili awataje mawaziri wanaomtukana rais. Asitafute umaarufu ubwete (cheap popularity)
unazan wanamuita ili awataje au ili wampe muongozo wa vitu vya kuongea hadharani na vya kupotezea kiufupi wanaenda kumpiga pini asiweke wazi mapungufu ya wana sisiemu mafisadi na manafiki ili kulinda heshima ya chama na si kutatua matatizo
 
Oyooooo!
Imetulia hiyo. Huyu mropokaji abananishwe ili awataje mawaziri wanaomtukana rais. Asitafute umaarufu ubwete (cheap popularity)
Kuitwa kwa Makonda kwa Kamati ya Maadili ya CCM ni "red flag". Itabidi asome alama za nyakati na atambue kwamba hizi si enzi za JPM ambapo alikuwa anaweza kufanya lolote( kama kuvamia kituo cha Clouds) au kutoa kaui tata (kama kuwataka wabunge wotw wa upinzani watoke mkoani kwake) bila hatua yoyote kuchukuliwa. Aache kuropoka kama vile alivyoropoka mara tu baada ya kuteuliwa kuwa Katibu Mwenezi ambapo alimpa waziri Mkuu agizo la kumaliza migogoro ya ardhi ndani ya miezi 6.

Asiposoma alama za nyakati tutaona hivi karibuni Zuhura Yunus anaandika: "Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Paul Makonda kama Mkuu wa Mkoa wa Arusha". Narudia tena asome alama za nyakati. Hizi si enzi za JPM.
 
Oyooooo!
Imetulia hiyo. Huyu mropokaji abananishwe ili awataje mawaziri wanaomtukana rais. Asitafute umaarufu ubwete (cheap popularity)
Mbona Lissu hajawai taja waliompiga liasasi na nyie mpo kimya mmetuliza matikiti?
 
Kuitwa kwa Makonda kwa Kamati ya Maadili ya CCM ni "red flag". Itabidi asome alama za nyakati na atambue kwamba hizi si enzi za JPM ambapo alikuwa anaweza kufanya lolote( kama kuvamia kituo cha Clouds) au kutoa kaui tata (kama kuwataka wabunge wotw wa upinzani watoke mkoani kwake) bila hatua yoyote kuchukuliwa. Aache kuropoka kama vile alivyoropoka mara tu baada ya kuteuliwa kuwa Katibu Mwenezi ambapo alimpa waziri Mkuu agizo la kumaliza migogoro ya ardhi ndani ya miezi 6. Asiposoma alama za nyakati tutaona hivi karibuni Zuhura Yunus anaandika: "Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Paul Makonda kama Mkuu wa Mkoa wa Arusha". Narudia tena asome alama za nyakati. Hizi si enzi za JPM.
Mbona mnaongea tu nyie watu wa chadema,angaikieni kurudi Bungeni walau mpate viti 20 tu...Ccm wanapiga ngona yao na nyie mnaruka nayo tu.
 
Mbona mnaongea tu nyie watu wa chadema,angaikieni kurudi Bungeni walau mpate viti 20 tu...Ccm wanapiga ngona yao na nyie mnaruka nayo tu.
Leo kuna maandamano kupinga sheria mbovu za uchaguzi; haijulikani kama watashiriki uchaguzi chini ya sheria hizo japo mwenye chama kishasema wataweka wagombea kila mtaa/kitongoji hadi jimbo.
 
Mkuu wa mkoa ni mtumishi wa umma huko ccm wanamwitia nini? Kwani ofisi ya rais utumishi iko wapi? Watu wanashauriwa kipuuzi nao wanafuata,
 
Nilitegemea angeitwa sekretarieti ya maadili ya umma
 
Mkuu wa mkoa ni mtumishi wa umma huko ccm wanamwitia nini? Kwani ofisi ya rais utumishi iko wapi? Watu wanashauriwa kipuuzi nao wanafuata,
Mtumie ujumbe apuuze huo wito kwa vigezo vyako hivyo.
 
Mkuu wa mkoa ni mtumishi wa umma huko ccm wanamwitia nini? Kwani ofisi ya rais utumishi iko wapi? Watu wanashauriwa kipuuzi nao wanafuata,
Huyu hafai kote!
Sio utumishi wa umma wala CCM
Ni mchonganishi, mpayukaji na asie na maadili.
 
Wajumlishe na udhalilishaji alioufanya kwa yule muhandisi wa TARURA kwenye clip inayotembea mtandaoni kwa sasa

Kule sio kumuwajibisha mtumishi, ule ni udhalilishaji wa wazi ningekuwa mimi ningetoka ukumbini halafua aagize askari wanikamate wanipeleke ndani kesi ianzie hapo

Kuna lugha za uongozi wenye mamlaka zisizohusisha dhihaka, CCM wanatakiwa wawafundishe vijana wao.
Jamaa Ni mpumbafu sana
 
Huyu hafai kote!
Sio utumishi wa umma wala CCM
Ni mchonganishi, mpayukaji na asie na maadili.
CCM wamemuita mwanachama wao kumuonya kwahiyo hawajakosea. Upande wa serikali nao wakiona inafaa watamuita kwenye secretariat ya maadili ya viongozi wa umma.
 
Back
Top Bottom