Paul Makonda aitwa kwenye Kamati ya Maadili ya CCM

Paul Makonda aitwa kwenye Kamati ya Maadili ya CCM

Makonda munamchukia tu, lakini jamaa kaumbwa kuja kuongoza.

Makonda ni aina ya viongozi wanaohitajika kwenye serkalizetu za Africa, baahati mbaya anachukiwa na wengi.
 
Kuna mtu kaandika eti haya ni mambo ya ndani CCM yasiingiliwe, haiwezekani kuachwa.
Bashite kilaza kalituhumu baraza la mawaziri ambalo ndio timu yetu ya taifa inayofanya kazi na Rais kuliongoza taifa, jee ni sawa wakaishi na kufanya kazi hawaaminiani usaliti ndani yao?
Alichofanya Makonda ni kama kumtuhumu Rais na vyombo vyake vya usalama kuwa HAWAWEZI KAZI HADI WANATEUA WAHAINI NA WASALITI bila kujua na nchi haiko salama.
Kwamba waziri anayeweza kulipa watu wamtukane Rais wanashindwaje kuuza siri za nchi kwa maadui ili wanufaike?
Ni kwa vile nchi hii imejaa woga na unafiki, lakini kwingine hao mawaziri wangesha mtaka Rais wajiuzulu wote maana hawaaminiki kwa raia tena kama wasaliti au amuwajibishe Bashite.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Usiogope, hatakutaja!
 
Sina mashaka nae
Kwanza huenda kashafika mjini toka juziiiii
Navyomjua mm yule mwamba haogopi atawataja watu humo mpka waoneane aibu
 
Makonda munamchukia tu, lakini jamaa kaumbwa kuja kuongoza.

Makonda ni aina ya viongozi wanaohitajika kwenye serkalizetu za Africa, baahati mbaya anachukiwa na wengi.
Labda kukuongoza wewe na wengine jamii yako! Ila viongozi bora kwa nchi za watu wenye akili hawana uongozi kama wa Makonda.
 
Makonda fanya kama kina ngwajina boy hakuna kukalia kiti hakuna kugusa mlango au miimo yake isitumie kipaza sauti na mengine riho wa Mungu atayokufunulia
 
huyu kijana hafai kuwa kiongozi, alishawahi kuota mapembe Mungu akamshusha, hakujifunza, sasaivi amerudi na kiburi kilekile na kuaibisha watu wazima mbele za watu ili yeye apate credit. aonywaye mara nyingi na kushupaza shingo atavunjika na hata pata data. kwa kifupi, wakimuita kama watamrudisha au watamwondoa, ipo wazi, huyu ni kiongozi muonevu, kiongozi asiye na maadili na hafai kuongoza watu wazima. hata asipowajibishwa na ccm kuna siku Mungu atamwajibisha. aombe Mungu awajibishwe na ccm, manake akiwajibishwa na Mungu hawezi kustahimili kabisa.
Kwa hii nchi ilipofikia,na kwa watu wapumbavu kama wewe na mimi,tunahitaji kiongozi katili zaidi ya makonda.
 
Inakuaje ccm waanze kumsumbua kijana wao? Kama wanaona ni mtovu wa nidhamu na maadili waachane nae wasimteue kwenye nyadhifa zao
 
kwanza konda kaitika wito au kasema yuko busy wasogeze mbele kama awali
 
Kamati ya Maadili ya CCM ikikuita inabidi usali sana, sio mchezo, utatiwa adabu kweli kweli, Kamati ya Maadili ya CCM ina watu wenye akili sana na lazima uwe na majibu ya uhakika ukiitwa na chai utapewa ukiitwa..!!
 
Huyu siyo wa kumpa uhuru wa kufanya anayoyataka, hakawii kurudi kwenye mambo yake ya kuua watu, kuteka na kupora mali za watu. Huyu ni shetani ambaye hakustahili kupewa nafasi hata ya ubalozi wa nyumba 10. Wenye akili wote na wenye hekima wanamshangaa aliyemteua na kumpa nafasi ya uongozi mtu aliyetakiwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kujibu tuhuma mbalimbali.

Akiendelea kumkumbatia, anaweza kuondoka naye siku umma ukiamka.

Kisasi cha damu alizozimwaga, tunaomba zikawe juu yake na kizazi chake muovu huyu.

RIP Sanane, RIP Azory. Mungu muweza wa yote uwapunguzie majonzi wanafamilia wa hawa ndugu zetu ambao shetani aliwapoteza.
Hakuna kipindi umma utaamka,acha kuota mzee!!!
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Ndugu Paulo Makonda ameitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi.

Ameelekezwa kufika kwenye Kamati hiyo tarehe 22/04/2024.

=====

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemuita Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kwenye Kamati ya Maadili.

Makonda anatarajiwa kufika mbele ya Kamati hiyo Jumatatu, Aprili 22, 2024 asubuhi na kukutana na wajumbe wa kamati hiyo.

Hata hivyo, Mwananchi inafahamu kuwa Makonda alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Aprili 20, 2024 majira ya asubuhi, lakini haikuelezwa sababu za kusogezwa mbele.

Barua ya wito wa CCM kwa Makonda haikueleza sababu za kumuita huku ikieleza kwamba, kuna masuala mbalimbali kati yake na wajumbe wanakwenda kujadili.

Lakini, wito huo huenda unahusishwa na kauli ya Makonda aliyoitoa wakati wa kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Waziri mkuu wa zamani, Edward Sokoine iliyofanyika Monduli, Arusha ambako Makonda alidai kuwa viongozi wakiwemo mawaziri wamekuwa wakilipa watu kumtukana Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mitandao ya kijamii.

Makonda alitoa onyo kwa viongozi hao akisema kama wakiendelea atawataja hadharani na kwamba, hayuko tayari kuona Rais Samia akitukanwa.


Chanzo: Mwananchi online

Pia soma:
Wameshampa onyo Kali kabla hawajamsikiliza
 
Back
Top Bottom