Paul Makonda aitwa kwenye Kamati ya Maadili ya CCM

Paul Makonda aitwa kwenye Kamati ya Maadili ya CCM

Ni kama kichwa Cha Uzi huu kinavyojieleza

Kamati za Maadili za CCM na Chadema siyo za Mchezo Mchezo ni sawa na Patakatifu pa patakatifu mtuhumiwa lazima afungwe kamba mguuni

Aidha tuishukuru CCM kwa kuanzisha Kombe jipya la Muungano Ili Makolo FC wasitoke mikono mitupu mwaka huu 😄😄🔥
Walau POPOMA aambulie hilo la Muungano.
 
Mwacheni Makonda afanye kazi yake

Huyu siyo wa kumpa uhuru wa kufanya anayoyataka, hakawii kurudi kwenye mambo yake ya kuua watu, kuteka na kupora mali za watu. Huyu ni shetani ambaye hakustahili kupewa nafasi hata ya ubalozi wa nyumba 10. Wenye akili wote na wenye hekima wanamshangaa aliyemteua na kumpa nafasi ya uongozi mtu aliyetakiwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kujibu tuhuma mbalimbali.

Akiendelea kumkumbatia, anaweza kuondoka naye siku umma ukiamka.

Kisasi cha damu alizozimwaga, tunaomba zikawe juu yake na kizazi chake muovu huyu.

RIP Sanane, RIP Azory. Mungu muweza wa yote uwapunguzie majonzi wanafamilia wa hawa ndugu zetu ambao shetani aliwapoteza.
 
nadhani hii ni alart kwa mama, ajue makonda ana hasara kwa chama chake na uongozi wake kuliko faida. hivyo yeye mwenyewe achague, abaki na makonda apoteze sapoti ya watanzania wengi, au apoteze makonda abaki na watanzania.

Naona Samia ameamua kupotomoka na Makonda wake. Ni ngumu sana kuelewa kuna nini kati ya mtawala na muuaji hadi kushikamana.

Ndege wafananao huruka pamoja. Je, ina maana Samia na Makonda, kuna namna wanafanana?
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Ndugu Paulo Makonda ameitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi.

Ameelekezwa kufika kwenye Kamati hiyo tarehe 22/04/2024.
Aende huko kwebye kamati awaeleze vizuri waliotaka kumuua kwa drone ni akina nani. Pia aeleze watu aliowapoteza akiwa RC wa Dar aliwatupa wapi ili ndugu zao wawazike

Bila kusahau kutaja mawaziri wanaomtukana Rais. Alisema angewataja Jumatatu iliyopita lakini hadi leo hajamtaja hata mmoja✍️
 
Dah nimekumbuka Kolimba na CCM siyo Mama Yangu. Makonda uwe makini sana tena sana, maji, mike, kiti etc Mungu akulinde.

Huyo ni muuaji mzoefu, huna haja ya kumpa tahadhari, amebobea kwenye mambo hayo. Anafahamu namna ambayo huwa wanafanya.
 
Dereva anakula per diem tu hapo
Dere atakuwa yuko kwenye maombi ili jambo lipite salama bila kuleta athari maana Dere kashajipata kwa huyo Bashi.te, safari hazikauki
 
Kombe hilo jipya la muungano halina tofauti na lile la mapinduzi. Tena la mapinduzi naweza kusema lina hadhi zaidi kwa kuwa linashirikisha timu za nje ya JMT.

Sasa siju hili jipya litashirikisha hata timu zipi!? Ninachotambua tutasikia sehemu maarufu zinapotoka, mathalani Mchambawima, Kizimkazi, n.k.
Zinashiriki timu 4 tu 😄

Simba, Azam, KMKM na Kikwajuni
 
Kumekucha na makucha yake. Watoto wa mjini hawataki mchezo. Makonda akileta za kuleta atapewa ONYO kisha ONYO KALI, litafuatiwa na KARIPIO. Akiendelea atakula umeme.
1. ONYO
2. ONYO KALI
3. KARIPIO
4. UMEME

Daahh hatua ndefu mazee....
 
Kamati ya maadili wenyewe ni mafisadi

Hawana credits za kumhoji mzalendo makonda

Hivi jitu linaloua watu, kutrka na kupora mali za watu, lina uzalendo gani? Huyu ni jambazi. Bahati mbaya tu nchi yetu inaendeshwa kimagumashi. Hili jitu lilistahili kuwa jela.
 
Mkenge mlioingia utakuja kuwaacha midomo wazi

Jiulize kwann watu wametawanyika wengine musoma, wengine kule (nchimb) wengine kule (jokt) huku (ally) nk

Siasa ni sayansi! Subiri ujue kitakacho kuja tokea
Kinatochusaidia ni wizi wa kura tu, hakuna kingine kabisa.
 
Ni kama kichwa Cha Uzi huu kinavyojieleza

Kamati za Maadili za CCM na Chadema siyo za Mchezo Mchezo ni sawa na Patakatifu pa patakatifu mtuhumiwa lazima afungwe kamba mguuni

Aidha tuishukuru CCM kwa kuanzisha Kombe jipya la Muungano Ili Makolo FC wasitoke mikono mitupu mwaka huu 😄😄🔥
Hapo unapoanza kutunanga sisi tusitoke mikono mitupu ndo umekosea sana.

Mtuache.

Kuhusu Kondaboy, hizo kuitwa kamatini ni drama
 
Zinashiriki timu 4 tu 😄

Simba, Azam, KMKM na Kikwajuni
Hii ni aibu kwa Simba.

Japo limetengenezwa kwa ajili yake, sasa itokee tena Azam wamkande atoke kapa dah!

Kuhusu drama za CCM wanasema anayewindwa hasa ni Luhaga Mpina. Na watu wa conspiracies wanasema kwamba CCM wana wasiwasi maana hawajui uchaguzi utakuwaje katika mazingira ya tume hii mpya ya uchaguzi na sheria mpya za uchaguzi. Kwa hivyo kuna mkakati wa kumfanya Makonda na Lissu wagombee urais kama wapinzani. Wao watagawana kura na Mama ataibuka mshindi kirahisi sana. Lissu atagombea kupitia CHADEMA na Makonda kupitia ACT....

Siasa ni Sayansi!
 
Attachments

  • Screenshot_20240421_110137_WhatsApp.jpg
    Screenshot_20240421_110137_WhatsApp.jpg
    283.6 KB · Views: 3
Makonda pamoja na mapungufu yake yote..bado ni karata turufu sana kwa serikali ya mama Samia..Kikubwa Mungu amlinde ni kiongozi mzuri sana wa kulingoza Taifa letu siku za usoni..Maadui ni wengi ila kikubwa watu wenye uthubutu wa kufanya maamuzi magumu Kama Makonda ni wachache..Tumuombee na kumshauri Ila tusimtukane, tusimsimange, Wala kumkatisha tamaa..Makonda ni kiongozi bora ajae kwa maoni yangu..Mama Samia ninakuomba Makonda ni kiongozi bora usimwache..wanaomsema vibaya ni wanafiki tu na watu wasiomtakia mema.

Labda kama unaishi kwenye ufalme wa shetani, ndiyo unaweza kumsifia mtu muuaji, mtekaji, mpotezaji watu na mporaji mali za watu, kuwa ni kiongozi bora. Atakuwa kiongozi bora kwenye huo ushetani wenu.

Muuaji na jambazi kupewa nafasi ya kuwaongoza watu wema, ni kufuru kubwa dhidi ya Mungu wetu wa haki na dhihaka kwa wanadamu wote wema. Laana ya kufuru na dhihaka hizi, zikatembee na jambazi hili na wale wenye kulikumbatia.

RIP Ben, RIP Azory, Neema ya Mungu iendelee kumlinda Lisu na wengine wote ambao jambazi hili liliwafikia.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Ndugu Paulo Makonda ameitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi.

Ameelekezwa kufika kwenye Kamati hiyo tarehe 22/04/2024.

=====

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemuita Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kwenye Kamati ya Maadili.

Makonda anatarajiwa kufika mbele ya Kamati hiyo Jumatatu, Aprili 22, 2024 asubuhi na kukutana na wajumbe wa kamati hiyo.

Hata hivyo, Mwananchi inafahamu kuwa Makonda alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Aprili 20, 2024 majira ya asubuhi, lakini haikuelezwa sababu za kusogezwa mbele.

Barua ya wito wa CCM kwa Makonda haikueleza sababu za kumuita huku ikieleza kwamba, kuna masuala mbalimbali kati yake na wajumbe wanakwenda kujadili.

Lakini, wito huo huenda unahusishwa na kauli ya Makonda aliyoitoa wakati wa kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Waziri mkuu wa zamani, Edward Sokoine iliyofanyika Monduli, Arusha ambako Makonda alidai kuwa viongozi wakiwemo mawaziri wamekuwa wakilipa watu kumtukana Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mitandao ya kijamii.

Makonda alitoa onyo kwa viongozi hao akisema kama wakiendelea atawataja hadharani na kwamba, hayuko tayari kuona Rais Samia akitukanwa.

Chanzo: Mwananchi online

Pia soma:
Makonda alirudishwa katikati ya uwanja wa kisiasa na mama Samia.
Mama aliamua kusahau madudu aliyofanya wakati wa Magufuli.
Makonda hakumbuki kuwa aliumiza watu kwa kauli na vitendo.
Tukumbuke alidiriki kumwita hadi Ridhiwani Kikwete kuwa ni don la madawa ya kulevya, wakati hana ushahidi.

Sasa hili la kuwatyhumu viongizi wenzake hadharani, as if yeye Makonda yuko juu yao matokeo yake sasa tunaysona.

Viongozi wenzake sasa wanamfunga kengele shingoni.
Na hili linaweza kuwa tukio la mwanzo wa mwisho wa Makonda.
CCM ikimpiga pini, hata mama Samia hatamsaidia.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Ndugu Paulo Makonda ameitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi.

Ameelekezwa kufika kwenye Kamati hiyo tarehe 22/04/2024.

=====

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemuita Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kwenye Kamati ya Maadili.

Makonda anatarajiwa kufika mbele ya Kamati hiyo Jumatatu, Aprili 22, 2024 asubuhi na kukutana na wajumbe wa kamati hiyo.

Hata hivyo, Mwananchi inafahamu kuwa Makonda alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Aprili 20, 2024 majira ya asubuhi, lakini haikuelezwa sababu za kusogezwa mbele.

Barua ya wito wa CCM kwa Makonda haikueleza sababu za kumuita huku ikieleza kwamba, kuna masuala mbalimbali kati yake na wajumbe wanakwenda kujadili.

Lakini, wito huo huenda unahusishwa na kauli ya Makonda aliyoitoa wakati wa kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Waziri mkuu wa zamani, Edward Sokoine iliyofanyika Monduli, Arusha ambako Makonda alidai kuwa viongozi wakiwemo mawaziri wamekuwa wakilipa watu kumtukana Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mitandao ya kijamii.

Makonda alitoa onyo kwa viongozi hao akisema kama wakiendelea atawataja hadharani na kwamba, hayuko tayari kuona Rais Samia akitukanwa.

Chanzo: Mwananchi online

Pia soma:
Huyu ccm hawatampenda,ana akili.
 
Back
Top Bottom