Paul Makonda aitwa kwenye Kamati ya Maadili ya CCM

Paul Makonda aitwa kwenye Kamati ya Maadili ya CCM

Hiyo project ya Train ni White Elephant, Hakuna kitu hapo.
Kama bwawa la Nyerere vile ndio maana unachat Kwa raha bila kuhofu umeme kukatika hivi wewe umewahi kujiuliza wasingewasha zile mashine Leo nchi ingekuaje bila umeme? Hebu wakati mwingine punguza uchawa
 
Kama kuna m
Mkuu wa Mkoa wa Arusha , Ndugu Paulo Makonda ameitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi .

Ameelekezwa kufika kwenye Kamati hiyo , tarehe 22/04/2024

=====

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemuita Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kwenye Kamati ya Maadili.

Makonda anatarajiwa kufika mbele ya Kamati hiyo Jumatatu, Aprili 22, 2024 asubuhi na kukutana na wajumbe wa kamati hiyo.

Hata hivyo, Mwananchi inafahamu kuwa Makonda alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Aprili 20, 2024 majira ya asubuhi, lakini haikuelezwa sababu za kusogezwa mbele.

Barua ya wito wa CCM kwa Makonda haikueleza sababu za kumuita huku ikieleza kwamba, kuna masuala mbalimbali kati yake na wajumbe wanakwenda kujadili.

Lakini, wito huo huenda unahusishwa na kauli ya Makonda aliyoitoa wakati wa kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Waziri mkuu wa zamani, Edward Sokoine iliyofanyika Monduli, Arusha ambako Makonda alidai kuwa viongozi wakiwemo mawaziri wamekuwa wakilipa watu kumtukana Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mitandao ya kijamii.

Makonda alitoa onyo kwa viongozi hao akisema kama wakiendelea atawataja hadharani na kwamba, hayuko tayari kuona Rais Samia akitukanwa.


Chanzo: Mwananchi online

Pia soma:
Akosa Rais Samia anayafanya basi ni kumkumbatia sana huyu Makonda!! Hana mwisho mzuri kwa chama na viongozi wenzake huyu hahitajiki kuwa kwenye ngazi yoyote ya maamuzi katika jamii!! Wanaokua karibu na Rais Samia hebu wamshauri kwa hekima amuweke pembeni huyu mtu!! Anavisasai sana moyoni na maamuzi ya ghafla sana, siku akipata madaraka makubwa kama ya Urais hawezi kutuingiza vitani na majirani zetu kurahisi sana. Shime sheme huyu mtu hatufai katika nchi yetu!!
 
Usanii tu, so long anayafanya na samia anambadilisha kazi na vituo, ujue hii kamati inapoteza muda tu.
Makonda ana sifa za mauaji, utekaji, upotezaji watu, how come Samia anamuita tena serikalini na kumpamba kuwa amekichangamsha chama?
Upotezaji muda tu...............................KAMATI KULENI POSHO ZA VIKAO ANYWAY
 
Wanajichanganya tu, Kamati ya maadili ccm haina nguvu labda angeitwa Ikulu tungepata matumaini fulani hivi, kwamba labda ataonywa. Huko maadili kuna nani wa kumtisha Makonda na Magufuli aliishafariki?
 
Kuna mtu kaandika eti haya ni mambo ya ndani CCM yasiingiliwe, haiwezekani kuachwa.
Bashite kilaza kalituhumu baraza la mawaziri ambalo ndio timu yetu ya taifa inayofanya kazi na Rais kuliongoza taifa, jee ni sawa wakaishi na kufanya kazi hawaaminiani usaliti ndani yao?
Alichofanya Makonda ni kama kumtuhumu Rais na vyombo vyake vya usalama kuwa HAWAWEZI KAZI HADI WANATEUA WAHAINI NA WASALITI bila kujua na nchi haiko salama.
Kwamba waziri anayeweza kulipa watu wamtukane Rais wanashindwaje kuuza siri za nchi kwa maadui ili wanufaike?
Ni kwa vile nchi hii imejaa woga na unafiki, lakini kwingine hao mawaziri wangesha mtaka Rais wajiuzulu wote maana hawaaminiki kwa raia tena kama wasaliti au amuwajibishe Bashite.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Kwana kabisa nilishangaa siku ile anaingia Arusha na mapokezi makubwa alafu inaandaliwa gari ya Mkuu wa Mkoa, na Bensera ikiwapo inapepea, unaiacha gari na kumpakuza mwanao na yeye kupanda gari nyingine, imekaaje ile ki protoko? Gar ye nye benderabya mwakilishi wa Rais wa mkoa na bendera inapepea anakaa mtoto na muhusika anapanda gari nyingine? Huyu mtu kweli achunguzwe akili!!
 
Kumekucha na makucha yake. Watoto wa mjini hawataki mchezo. Makonda akileta za kuleta atapewa ONYO kisha ONYO KALI, litafuatiwa na KARIPIO. Akiendelea atakula umeme.
Makonda asichokijua ni kwamba Regime ya sasa sio ile..Saiv mtu anakuchekea huku anakuwekea kisu. Utaumia jamaa na wewe bila kukaa Serikalini utaenda wapi mtu imezoea kufokafoka kutishia watu na mkwara.
 
Kwana kabisa nilishangaa siku ile anaingia Arusha na mapokezi makubwa alafu inaandaliwa gari ya Mkuu wa Mkoa, na Bensera ikiwapo inapepea, unaiacha gari na kumpakuza mwanao na yeye kupanda gari nyingine, imekaaje ile ki protoko? Gar ye nye benderabya mwakilishi wa Rais wa mkoa na bendera inapepea anakaa mtoto na muhusika anapanda gari nyingine? Huyu mtu kweli achunguzwe akili!!
 
Hakuna Jipya Hapo Nawaambia CCM Kama Inapora Kura Na Kuwakumbatia COVID 19 La Makonda Msilipe Airtime
 
Kwana kabisa nilishangaa siku ile anaingia Arusha na mapokezi makubwa alafu inaandaliwa gari ya Mkuu wa Mkoa, na Bensera ikiwapo inapepea, unaiacha gari na kumpakuza mwanao na yeye kupanda gari nyingine, imekaaje ile ki protoko? Gar ye nye benderabya mwakilishi wa Rais wa mkoa na bendera inapepea anakaa mtoto na muhusika anapanda gari nyingine? Huyu mtu kweli achunguzwe akili!!
Makonda anasumbua sana vichwa vya mafisadi! Hahaha ngoja tuone!
 
imeishaahiooo nikokwammassawe wakala.leos 22apr tupe mrejesho wa kikao jion
 
Huyu mama naye sijui ni takataka ya wapi, hili jitu halifai hata kuongoza mtaa analing'ang'ania la nini? Halina maadili ya utumishi hata kidogo! Na linaonesha limetoka familia hohehahe sana!
Maadili ya utumishi ndio hayo mnayosema kwamba hatakiwi kupiga kelele “wakati wa kula”?
 
Back
Top Bottom