Paul Makonda aitwa kwenye Kamati ya Maadili ya CCM

Paul Makonda aitwa kwenye Kamati ya Maadili ya CCM

Safari ya Maarim kupanga njama unazani ilikuwa ni ndogo? Kuliko ya kolimba? Ndio sababu ya jumbe kukaa kizuizini!
Safari ya Maalim Sefu na wenzake, Hamad Rashid, Hamis Shaaban Mloo, Soud Yusuf Mgeni na mwingine mmoja, mwaka 1988, ilikuwa ngumu kuliko safari za wanachama wengine wote walioitwa kwenye vikao vya aina hiyo (Ukiondoa kikao kilichomfuta uanachama marehemu mzee Aboud Jumbe mwaka 1984)
Makonda hana chaguo lingine, lazima afike kwenye mahojiano.
 
Naona Kuna kundi kubwa sana la kumshambilia makonda binafsi na sio utendaji yaani Bado watu wanatamani mafisadi yabembelezwe? Na kibaya zaidi naona upepo wa Arusha unabadilika lema amepotea gafla hii inaonyesha makonda maadui wake wameongezeka lakini tukumbuke mti wenye matunda ndio hupigwa mawe
 
Safari njema makonda shikilia hapo hapo inawezekana unamabaya yako lakini pia mazuri yako ni mengi wewe sio malaika nakumbuka hata ukiwa mkuu wa wilaya dar ulitupimia viwanja vyetu nyakasangwe na kufurusha Yale matapeli yaliyokua yanasema yanamiliki mashamba matapeli yaliyolelewa na Mr msoga mpaka Leo tunaishi Kwa amani
 
Wenye chama Chao wameona
THIS IS TOO MUCH. hatuwezi kuvumilia, wakati tunaanzisha chama Makonda alikua havai kaptura, leo anaendesha Range kwa pesa zetu anatuletea ujinga. Hata ukuu wa mkoa haumfai.
FB_IMG_1713724739823.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha , Ndugu Paulo Makonda ameitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi .

Ameelekezwa kufika kwenye Kamati hiyo , tarehe 22/04/2024

=====

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemuita Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kwenye Kamati ya Maadili.

Makonda anatarajiwa kufika mbele ya Kamati hiyo Jumatatu, Aprili 22, 2024 asubuhi na kukutana na wajumbe wa kamati hiyo.

Hata hivyo, Mwananchi inafahamu kuwa Makonda alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Aprili 20, 2024 majira ya asubuhi, lakini haikuelezwa sababu za kusogezwa mbele.

Barua ya wito wa CCM kwa Makonda haikueleza sababu za kumuita huku ikieleza kwamba, kuna masuala mbalimbali kati yake na wajumbe wanakwenda kujadili.

Lakini, wito huo huenda unahusishwa na kauli ya Makonda aliyoitoa wakati wa kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Waziri mkuu wa zamani, Edward Sokoine iliyofanyika Monduli, Arusha ambako Makonda alidai kuwa viongozi wakiwemo mawaziri wamekuwa wakilipa watu kumtukana Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mitandao ya kijamii.

Makonda alitoa onyo kwa viongozi hao akisema kama wakiendelea atawataja hadharani na kwamba, hayuko tayari kuona Rais Samia akitukanwa.


Chanzo: Mwananchi online

Pia soma:


Self destructive machine = Makonda. ( Huwa anajiharibiaga mwenyewe bila sababu)
 
Naona Kuna kundi kubwa sana la kumshambilia makonda binafsi na sio utendaji yaani Bado watu wanatamani mafisadi yabembelezwe? Na kibaya zaidi naona upepo wa Arusha unabadilika lema amepotea gafla hii inaonyesha makonda maadui wake wameongezeka lakini tukumbuke mti wenye matunda ndio hupigwa mawe
Popote alipo Makondaa hakuna kenge wa kuropoka
 
Hivi kuna mtanzania wa kusikiliza Nchimbi , Makala au Jokate ? kwanza hawa wangekuwa silaha ya ccm unadhani Mngekataa katiba mpya na Tume Huru ?

Silaha pekee ya ccm ni Polisi na vyombo vya dola
Aahaaaa

Hao wote hawana mvuto
 
Kamati ya maadili wenyewe ni mafisadi

Hawana credits za kumhoji mzalendo makonda
Hapo ndio vichwa panzi kama hao wanaojaza mameseji humu wanashindwa kuhoji hao waadilifu wa hiyo kamati ni malaika kutoka mbinguni? Au ni hawahawa mafisadi na wapiga Dili ndio wanajigeuza kamati ya maadili pale maslahi yao yanapoguswa?
 
Back
Top Bottom