Mimi nina hakika CCM hatuwezi kuhalalisha uchaguzi Mkuu kwa kutumia CHAUMA na ACT Wazalendo.
Jumuiya za ndani ya nchi na za kimataifa zinakitambua CHADEMA kuwa ndiyo Chama kikuu Cha upinzani.
Jumuiya hizo pia zinatambua kuwa taratibu za uchaguzi haziko sawa.
Ikumbukwe kuwa Magufuli,pamoja na ubabe wake,lakini alihakikisha Chadema kinashiriki uchaguzi Mkuu.Hii ni kwa sababu katika nchi yoyote jambo linaloangaliwa kwa unzito mkubwa na wananchi na Jumuiya za kimataifa ni uchaguzi Mkuu.
Tujiulize kama nchi tunaweza kumudu uchaguzi utakaogharimu fedha yote halafu ustambuliwe na Watanzania walio wengi na Jumuiya ya kimataifa.Ni sawa na kupanda shamba kubwa na usivune chochote.
Madhara yake ni kutengwa na Jumuiya ya kimataifa,kukosa uwekezaji,kukosa misaada na mikopo.Hatuwezi kumudu kujiendesha bila misaada au mikopo.
Mapato yetu bado yako chini mno.