Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Aisee kweli mkuu hapo lazima wakuu leo usiku wakae kikao kujadili nini cha kufanya,labda ndipo umuhimu wa wakina Balozi Mahiga waliohudumu huko US/UN miaka na miaka utaonekana lkn wakimuachia huyu kabudi aliyezoea tu kufundisha darasani aje aongee na Media kuhusu jambo hili,then pia wajiandae kisaikolojia.
dodge
 
Hatimaye tunakwenda kuwa Taifa linaloruhusu Ushoga na kuibiwa rasilimali zetu kama kawaida.

Wapinzani wakiongozwa na ZitoKabwe, Maria Sarungi na Fatma Karume ndio waasisi wa Taifa jipya lenye kuruhusu ushoga na utumwa wa kuibiwa Rasilimali na mabeberu.
 
Aiseee....Mike Pompeo kuandika habari mbaya kuhusu mtu kama Makonda ni kitu cha hatari sana. Makonda has to be careful. Na anaemkingikia kifua inabidi awe makini zaidi.....Ngoja tuone!


Sent using Jamii Forums mobile app
Am shook myself

kwa nafasi yake in the US and the World kumdili Bashite waziwazi aiseee..where are we going🥺
 
Marekani ndio nani kwanza na kwa utakatifu gani alio nao kwa kuziamulia nchi mbali mbali Duniani zenye misingi yao binafsi? Eti tuheshimu utawala wa sheria na haki za binadamu ikiwemo uhuru wa kujieleza na kukusanyika. Kwa utakatifu gani walio nao?
Serikali inazuia mikusanyiko ya vyama vya siasa wakati usio kuwa wa campaign ili kuzuia uvunjifu wa amani nchini, leo hii Marekani anakurupuka anataka mikusanyiko iwepo hata kama haijaruhusiwa na sio kipindi cha campaign na amani ikivunjika nchini mambo yakiharibika nchini hawa jamaa hamto wasikia kokote wakituimbia suala la amani zaidi ya kutucheka,
Na mpango wao wa NWO wanataka wawe na say juu ya taifa lolote ili wapate nguvu ya kuitawala Dunia kirahisi,
Huyu mmarekani muovu kabisa huyu, hawezi akaja kukuimbia wimbo wa haki za binanamu kakujulia wapi na kwa utakatifu gani alio nao, asilimia 100% ya maamuzi ya hawa jamaa juu ya taifa lolote Duniani ni kwa lengo la kubomoa sio kujenga, hata kama mtaona faida mwanzoni baada ya kuyatekeleza maagizo yao mwishoni ni hasara,
Namuombea maisha marefu na afya Rais wetu Dk. John Magufuli ni mwamba, hata kama wakituzuia kwenda huko kwao Marekani kwani Marekani ni Mbinguni? Wapuuzi tu hawa,
 
Utakuta mtu ana furahia Makonda kuzuiliwa kuingia US yeye hata Kitambulisho cha nida hana. [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
😆😆😆
Raia wa Twitter huko wanaongea kiswahili tu
Sijui personally Makonda anajiskia aje maana kwa zile comments the Hate is real...ajichunguze tu dhamiri yake Mimi ningekufa kwa hizo comments watu wanashukuru kwa mabaya yanayokupata ujue na kifo wanamuombea
 
Ndo ujue mashoga wanalindwa kuliko hata watoto wa Zitto Kabwe na WB wanaojifungulia mashuleni

Hizo propoganda za Makonda usije ukafa naye. Wewe jali familia yako ma maslahi ya nchi siasa hazitakusaidia. Hakuna watu wanaojua US kuliko sisi tunaoishi hapa achaneni na habari za mitandao. Sababu zote ziko kwenye barua
 
Leo naposti kwa uhuru najua sitapotezwa.
Asante Lissu, Asante Roma, Asante Kabendera, Asante Magoti.
RIP Ben Saanane, RIP Mawazo nafsi zenu hazijapotea bure.
Hakuna mabaya yasiyo na mwisho wake, wapo wapi akina chiluba, Abacha, Gadafi, Sadam Hussein, Bokasa , Iddy Amin Dada na yule msaidizi wake aliyeitwa maliyamungu aliyekuwa na roho mbaya kama ya Daud Bashite.
 
Washenzi sana hao bwn Pasco.....
wamemuua Suleimani wa Iran kwa kukiuka haki za binaadam....
alafu wanajifanya wanajua kunyooshea vidole wenzao....shenz sana
 

Biashara zote Duniani ni $$$ tuamue watoto wetu au bashite
 
Consult your Google by writing "who is USA" halafu rudia kusoma comment yako ulioandika.
Labda nikuulize Kuna mikutano inayofanyika bila kufuata Taratibu husika??
Hebu tuliza akili na utafakari kwa kina ndugu

Halafu ni serikali sio serikari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…