Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Katika sababu zilizotajwa kwa Makonda kuzuiliwa kwenda Marekani ni "kuwanyima watu haki ya kuishi na usalama wao" Hi ni sentensi nzito kwa watu wanaofikiria mambo kwa umakini, kwa kuwa unapomnyima mtu haki ya kuishi ina maana huyo mtu haishi tena, hayuko hai tena kwa kuwa umeondoa haki yake ya kuishi, au umemnyima haki yake ya kuwa hai - umemuua. Hilo ndilo wanalosema USA juu ya Makonda.

Watu wengi wanafikiria kwamba Makonda amezuiliwa kwenda USA kutokana na msimamo wake juu ya suala la ushoga, lakini ni wazi kutokana na kauli ya USA kwamba kuna zaidi ya hilo. Je kuna mambo ambayo Watanzania tumefumbwa kwa muda mrefu sana na serikali yetu lakini USA wana taarifa zote?

Kumekuwa na taarifa nyingi kuhusiana na watu kuuwawa, kutekwa na majaribio ya kuuwawa ncini ambazo serikali haijawa wazi sana kuzieleza au kuonyesha kuwa inayafanyia kwa uzito upelelezi wa hayo matukio. Kuna dalili basi, kwamba hawa USA wana ufahamu wa haya mambo kuliko tunavyofikiria.

Ipo siku ukweli wote utawekwa wazi. Lakini kwa sasa, Makonda kutuhumiwa kwamba amekuwa akiwanyima watu haki ya kuishi ni jambo kubwa sana!

Reference:Makonda apigwa 'stop' kuingia Marekani

 
Acha cherry picking mimi nimetoa mfano kuwa mbona ameingia nchi masikini pia ambazo hazima rasilimali kama Kosovo au Guatemala?

Kwahiyo nimekipa task nipe mfano wa nchi yenye rasilimalia ambayo US ameingia bila vita kupiganwa na ikaharibika?? Nipe mfano wa hizo nchi.

Maana mmi hoja yangu ni kwamba nchi zinaharibiwa na vita sio eti marekani..... Mbona Egypt iko imara licha ya pressure ya US jamaa kuachia ngazi?? Vipi CUBA mbona licha ya pingamizi la US wamebaki imara hadi leo?? Yote sababu huko vita hazikupiganwa za wenyewe kwa wenyewe ila vita ndio huleta maafa.

Libya na Iraq huko sababu vita zimepiganwa so Is machafuko venezuela. Ila marekani ikikuwekea pressure alafu ukiamua kujiuzuru kirafiki kabisa kama Yahya Jammeh nchi yako itaharibikaje?? Hapa ndio sikuelewi kabisa.

Issue ni VITA.....VITA....VITA..
 
sisi ni matajiri sana, hata U.S.A akitaka vita na sisi tutampiga yeye na washirika wake wote.
hatujawahi kushindwa kwenye medani ya vita
Wewe waache tu wamarekani, tutawapiga shangazi zao mpaka wanyooke😂😂😂😂
 
Kwa hiyo unataka a'abide na demokrasia za ushoga?
 
The trending news is that letter, which I personally have not established its authenticity, said to have originated from the US foreign office. I am taking time to imagine what exactly has the Dar RC done to a level of being classified a human right violator in the country. Nothing, except two possibilities: war against drug dealers and homosexuality.

Self scrutiny exonerates drug dealers war, which is also a menace in the US unless, US feels fine when practiced in Africa or say, in any black race nation. Then to the second, likely to be the reason is homosexuality. This is somehow laughable! Africans, Tanzanians will never support you on this in any near future civilizations.

If truly US think Makonda is wrong by going against homosexuality, that will be an overwhelmingly yes vote to him from Tanzanians. We love such people! To the US, that will be a big misjudgment of our thinking. It is saying to hell with your Washington if the pre-requisite is homosexuality. Let's get the US confirmation.
 
USA wamelianzisha wenyewe sasa tusilaumiane,
Wanachopaswa waelewe kwa sasa sisi si dhaifu tena chini ya mwamba dokta JPM,
Kwanza wanampa tuhuma nzito Makonda bila kuweka ushahidi, huo ni umbea tu kama umbea mwingine,

Hatutawanyenyekea hata kidogo, ni heri kuwa masikini jeuri kuliko kunyanyaswa, yaani marekani atuamulie sisi namna ya kuishi? Yeye kama nani?
Hii nchi ni huru na inajiendesha yenyewe,

Hata aibu hana taifa kama USA eti anaweka ligi na TZ?

Sasa ni jino kwa jino, tunaomba Rais na wewe ujibu mapigo tuone sasa kama vipi hata uhusiano na Us uishe, kwanza hawa watu ni magaidi tu kazi yao kuvuruga nchi za watu,

Tuko nyuma yako JpM
Pole sana Makonda
Kwanza kabudi alihaidi atahakikisha anapambana kuiondolea vikwazo zimbabwe, na kwa hili ninaimani hatashindwa!

Tuko nyuma yako Kabudi

USA asituchezee na akiendelea ile military base yake iliyopo kenya tutaisambaratisha na kuifutilia mbali
 
Kuna nini Rwanda zaidi ya masokwe? Mambo yote yapo DRC north east, kaone balaa lake huko sasa, hata Rwanda ni mnufaika..
Ona sasa!! ww umesema nchi ikikua kiuchumi wanaimaliza sasa Rwanda mbona hawaimalizi?? Umehamisha magoli tena.......

Ni hivi mkitenda haki mnawanyima hata US kupata sababu ya kuwaingilia siasa zenu. Kingine muache kuwalilia misaada ndio maana wanatuingilia ila mkiwa huru watawaingilia au kuwapangia mambo??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…