Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Serikali ya Marekani imemzuia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuingi nchini humo kutokana na kuhusika kwake kwenye uvunjifu wa Haki za Binadamu unaohusisha kunyima haki ya kuishi, uhuru na ulinzi wa watu.

Katika uongozi wake, Makonda ameonesha uonevu kwa wapinzani, kuminya uhuru wa kujieleza na kukusanyika na matendo maovu dhidi ya makundi maalum.

Marekani ina hofu kuhusu uvunjifu wa Haki za Binadamu na kupuuzwa kwa utawala wa sheria nchini Tanzania.

Kifungu namba 7031(c) kinampa uwezo Waziri wa Mambo ya nje kuweka zuio kama hili endapo mhusika amefanya ufisadi mkubwa au uvunjifu wa Haki za Binadamu. Pia kinamruhusu kuweka zuio kwa familia yake hivyo mke wa Makonda, Bi. Mary Felix Massenge amezuiwa pia.

Serikali ya Marekani inaikumbusha Serikali ya Tanzania kuheshimu utawala wa Sheria na Haki za Binadamu ikiwemo uhuru wa kujieleza na kukusanyika.

View attachment 1342609
Mimi kwa hili bado ni Tomaso.
Ila kama ni kweli goti langu limepigwa nitainua mikono yangu juu kuelekea mbingini niseme;
"ASANTE YESU"
BUSHIRI HUKO SUDANI ALIKUTWA NA US DOLLAR MIL 133. Tusipo amini katika mambo yaliyotuzunguka hakika hatutathibitika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiukweli upepo umebadilika ghafla baada ya taarifa ya RC Makonda kupewa marufuku ya kuingia nchi ya mabwanyenye, Marekani.

Kabla ya taarifa hizi habari ya mjini ilikuwa ni Zitto na Kangi Lugola na kwa week end hii nina hakika wameshasahaulika.

Maendeleo hayana vyama!
Najua kesho kutwa lazma kuna clip zitavuja.. Zitavuja Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna lolote wenye maamuzi ni watz tu wasio hao mabeberu na wasaliti
CCM wakienda kuomba misaada huwaita wazungu ni wafadhili lakini hao hao wazungu wakikataa udikiteta wa CCM hukimbilia kuwaita mabeberu
 
Amka wewe acha kuota saa hizi. Unalalaje unajisahau unaota mandoto ya hivyo?
Huu ndio wakati muafaka kwa Watanzania kusimama na rais, maana anatafutwa kwa namna zote, wanataka wamdhoofishe ili waendelee kubeba madini maana yeye ndiye mzalendo wa kwanza kupambana dhidi yao, alifanya kitu ambacho hakijawahi kufanywa na kiongozi yeyote Afrika, leo hii Waafrika wote wanamtegemea kuona kama atashinda kwenye haya mapambano, ili na wao waliamshe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila wamechelewa sana BASHITE katuumiza watanganyika sana.
Kila nikimuangalia Magufuli nashindwa kumuelewa kabisa, ubabe wake wote amekua Rais DHAIFU kwa hiki kiumbe.
La moja, Ni ndege wenye bawa moja, warukao pamoja!!!
 
Wataalam..tueleweshane kidogo. Nimepitia baadhi ya comments za hii post nimepata maswali kadhaa.

P Makonda kuzuiliwa kwenda US ina ina impact kwa TZ kama nchi au kwa Paul himself?

Kwa WaTZ wanao support hio adhabu ya mtu alie temper na huma rights.. wakitaja uonevu..kuminya democracy etc (as guesses maana pompeo hajawa specific), "wako tayari hayo yanayoshutumiwa kufanyika yawe rectified plus other things kama gay & lesbian rights ziwe practiced in TZ?.."

Maana kwao US human rights sio kuruhusu democracy tu.. sijui uhuru wa kujieleza.. kwao it also comes with rights to be anything you want.. including gay and lesbian.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I concur,jamaa alishawahi hadi kumdindia PM kwny ile inshu ya Shisha hapo nilianza kumuelewa vzr.

Ofcourse DAB ni zaidi ya tumuonavyo..thats' obvious
Ni vile tu hatujafunuliwa what he is really capable of

dodge
 
Asante mabeberu,Sasa Tz inafuatiliwa kwa kina sana na hawa mnaowaita mabeberu huu uchaguzi wa mwaka huu ccm wkicheza rafu tujiandae kuingia Zimbabwe direct maana naona donor countries wameamua,ukiona Marekani kafanya hivyo ujue washirika wake wanafuata.
 
Back
Top Bottom