Hapana waseme sababu nyingine lakini kwa hii wanatudanganya watanzania.
Over deteriorating respect for human rights???
Zipii.??
Kwa hiyo huu ukandamizwaji wa haki za binadamu kaufanya makonda peke yake Kama mkuu wa mkoa ndio Mana yeye kapewa ban???
Uvunjifu gani alio ufanya, kaua, kanyonga mtu, kafunga mtu jela, kateka mtu ama nini hasa, Kama ni hivo kwanini hawakuweka ushahidi hata wa hayo aliyo yafanya???
Waseme tu ukweli na sio kutufanya wajinga kiasi hiki, Kama kweli huku kuna uvunjifu wa haki za binadamu na hakuna utawala wa sheria basi wangeanza na Rais na sio mkuu wa mkoa. Hili jambo linashangaza sana hili.
Au ni kwasababu aliwapinga walipotao matamko kuwa kutakuwa na mashambulizi ya kigaidi maeneo ya masaki bila kushirikisha serikali (huu ndo utawala wa sheria wanao utaka)na kusema watalii wasije tz.?
Au ni kwasababu aliwapinga pale walipokuwa wanalazimisha kuaminisha watu kuwa Tanzania kuna EBORA tena mgonjwa kagundulika temeke Dar es salaam?
Nadhani Wana kitu binafsi na Makonda na hii habari ya human rights ni kisingizio tu.