Nimeshangazwa sana kuona Leo hii RC Makonda kashindwa kujitokeza kujibu tuhuma nzito zilizotolewa na Marekani dhidi yake.
Kuhusu kuzuiwa kwenda US hata mimi namuunga mkono kupotezea kwani sio lazima kwenda huko maana mie binafsi huu ni mwaka wa NNE sijakanyaga US na sioni tatizo maisha yana songa, lakini tuhuma nzito kama kukatisha maisha ya watu hasa wapinzani kisiasa sio za kukaa kimya.
Jee hajui kuwa sasa hivi wenye ndugu zao walio potea kwa hisia kuwa sababu ni za kisiasa wamesha muweka kuwa yeye ndio kawateketeza? Maana US hawana sababu ya kumzushia Makonda tuhuma nzito kama hizo.
Hajui kuwa tuhuma hizo nzito zinamuweka mashakani maana hakuna atakaye jitokeza kumsemea zaidi yake mwenyewe na watu tayari wamemuweka kwenye kundi la wauaji?
Ajitokeze akane au atamke kuwa alikuwa naye anatumwa tuu.
View attachment 1343146
Sent using
Jamii Forums mobile app