Paul Makonda kuitetemesha na kuitikisa mikoa kumi mfululizo bila kupumzika

Paul Makonda kuitetemesha na kuitikisa mikoa kumi mfululizo bila kupumzika

Hivyo vyama ambavyo unasema sijavitaja nimekuachi wewe uvitaje na kuviimba kama kasuku.
Hujiewi Wewe, unasifia Chama tu pasipo kuwa na hoja za msingi, hiki unachokifanya ni uhayawani wa kiwango cha SGR, Mpuuzi tu wewe kwani umekuwa ni reporter wa Chama humu JF. Tafuta njia nyingine ya kukisifia Chama na Watu. Ningekuona wa maana sana tungekuwa na njia mbadala za kujibu kero na uharibifu unaofanywa na Chama chako. Unayo yaripoti humu Millard Ayo, radio,Vituo vya TV na magazeti vinatosha. Wewe tafuta njia nyingine. Amelaaniwa mtu amtegemeae Binadamu mwenzake na wewe ndio una laana kubwa sana yaani mpaka umpambe Kiongozi na kumtolea taarifa kwa kila anachokifanya. Njaa na shida haziondoki kwa kujipendekeza kwa Chama chako na viongozi wa Chama.
Badirika wewe.
 
Aisee!! Umemtukana sana Erythrocyte.

Ni aheri mtu akutukane tusi jingine lolote kuliko akuambie una akili na unafiki kama Mwashambwa.
Hao wote ni wawendawazimu
 
Hujiewi Wewe, unasifia Chama tu pasipo kuwa na hoja za msingi, hiki unachokifanya ni uhayawani wa kiwango cha SGR, Mpuuzi tu wewe kwani umekuwa ni reporter wa Chama humu JF. Tafuta njia nyingine ya kukisifia Chama na Watu. Ningekuona wa maana sana tungekuwa na njia mbadala za kujibu kero na uharibifu unaofanywa na Chama chako. Unayo yaripoti humu Millard Ayo, radio,Vituo vya TV na magazeti vinatosha. Wewe tafuta njia nyingine. Amelaaniwa mtu amtegemeae Binadamu mwenzake na wewe ndio una laana kubwa sana yaani mpaka umpambe Kiongozi na kumtolea taarifa kwa kila anachokifanya. Njaa na shida haziondoki kwa kujipendekeza kwa Chama chako na viongozi wa Chama.
Badirika wewe.
Uharibifu upi unaouzungumzia wewe? Kero za wananchi zinaendelea kujibiwa na kupatiwa majibu stahiki kila uchwao.ndio maana watanzania wanaendelea kuwa na imani kubwa sana na CCM na Serikali yake kwa kuwa imekidhi matarajio yao na kukata kiu yao.mimi ni mwana CCM na Nina wajibu wa kukisemea chama changu na viongozi wangu kwa yote wayafanyayo katika kuwaletea maendeleo wananchi pamoja na kujibu kero za wananchi kwa kuwapa majibu stahiki.
 
Natarajia kuona na wenzetu wa vyama vingine wakiendelea na operation kama za Comrade Makonda.
Ni vizuri pia baadhi ya issues ziwe solved na mamlaka zinazohusika Ili kupunguza malalamiko na kuondoa kasumba ya Wanasiasa kujisifu/kujipatia umaarufu kupitia matatizo ya Wananchi.
Vyama vingine kama CHADEMA vilishakata pumzi muda mrefu sana.havina hata hela ya mafuta kwa ajili ya kufika mikoani .ndio maana unaona vimebaki mifukoni tu kama shilingi.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Fahamu ya kuwa Ndugu Paul Makonda Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Taifa,yule mwamba wa siasa za majukwaani na ambaye anachukuliwa kama sauti ya wanyonge na ambaye alitangaziwa Mwisho na maadui zake lakini Mungu akatangaza Mwanzo,ambaye kwake zege halilali,na ambaye anatajwa kama kijana jasiri sana katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kusini mwa Afrika.

Ambaye akizungumza na kuanza ziara basi nchi yote husimama,vyombo vyote vya habari hushindana kupamba picha zake kurasa za mbele na mitandao yote hutekwa na habari zake na ambaye amekuwa kiboko ya CHADEMA anakwenda kuitikisa na Kuitetemesha mikoa kumi mfululizo kwa ziara ambayo inasubiriwa kwa hamu sana na mamilioni ya watanzania ambao walikuwa wanamsubiri kwa hamu kuwafikia huko waliko ili wamueleze kero zao kusudi azipeleke serikalini.

Sasa kama ulikuwa na shughuli yako au biashara yako unataka kuitangaza kupitia vyombo vya habari au mitandao ya kijamii,basi nakushauri usipoteze muda ,ni bora usubili huyu mwamba amalize ziara yake ,maana kwa sasa anakwenda kuiteka nchi yote kimijadala na watu wote wanakwenda kutega masikio yao kusikiliza nini anazungumza na nini kinajiri katika ziara zake.

Kama wewe ni msanii na ulipanga kutoa wimbo wako basi ni bora uuweke kwanza pembeni mpaka Mheshimiwa amalize ziara zake,maana akishaingia mitaani huyu basi wimbo utakuwa ni mmoja tu ambao ni Makonda na utekelezaji wa ilani ya CCM tu.

Endeleeni kutulia Watanzania wenzangu maana najuwa mlimkumbuka sana na mlikuwa na hamu ya kumsikiliza mwamba akiunguruma kama Simba majukwaani.sasa amewasikia na anakuja kwa kishindo.

Watendaji wa serikali na wateule wa Mheshimiwa Rais andaeni majibu ya kila kitu juu ya kazi mnazofanya na kusimamia katika utekelezaji wa ilani ya CCM Katika maeneo yenu.Maana huyu mwamba huwezi kujuwa atakupiga wapi.kumbuka huyu ni msemaji wa chama na mjumbe katika vikao vyote muhimu vya CCM. sasa wewe lete nyodo zako huko uone kitakachokupata atakaporejea kupeleka mrejesho kwa chama juu ya aliyoyabaini mikoani huko na akina nani wanakichonganisha chama na wananchi au wanatesa wananchi au hawatoi huduma stahiki kwa wananchi au wanapuuza wananchi au hawawasikilizi wananchi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.

Chief manyama
IMG_4385.jpg
 
Uharibifu upi unaouzungumzia wewe? Kero za wananchi zinaendelea kujibiwa na kupatiwa majibu stahiki kila uchwao.ndio maana watanzania wanaendelea kuwa na imani kubwa sana na CCM na Serikali yake kwa kuwa imekidhi matarajio yao na kukata kiu yao.mimi ni mwana CCM na Nina wajibu wa kukisemea chama changu na viongozi wangu kwa yote wayafanyayo katika kuwaletea maendeleo wananchi pamoja na kujibu kero za wananchi kwa kuwapa majibu stahiki.
😂😂😂😂
Kero zipo wewe acha kujiaibisha leo asubuhi nilikuwa nasikiliza radio Tumaini kuna shule ina Wanafunzi 1500 kila Mwanafunzi anaambiwa aende na Jaba la Maji, Mfagio wa chelewa, Panga na matofali matano wewe huoni huu ni upigaji na mradi wa watu ? Na happ hapo tunaambiwa elimu ni bure?
Yaani ukiwa na akili timamu huwezi ukaingia humu ukawa unasifia Serikali ya Chama cha Maponduzi.
 
Kwa hiyo kama elimu bure unataka hadi mfagio mwanao asipeleke shuleni??? Vitu vingine vidogo vidogo kama hivyo ni vya kawaida tu. Sasa wewe mfagio wa elfu moja nao unaona ni mzigo na gharama kubwa kununua?
 
Wenzio tulivuka mwaka na utimamu wetu .

Wewe hata akili kidogo ulizokua nazo uliziacha 2023.

Uzi una maoni 81 ila robo tatu ni negative na unajidai huoni kwa kuvaa miwani ya mbao.

Huyo zero brain akatetemeshe mikoa hiyo kwa kipi wakati watu wana mgao wa umeme, maji na gharama za maisha zikiwa juu nadhani utakua unaota , yaani 7k ndio inawavua utu hivyo ni dalili tosha hali sio nzuri Tanzania.
 
Endelea tu ndugu yangu kutingisha tako manake ,,upinzani wenyewe wa nchi hii ni mapopoma tu
 
Kwa hiyo kama elimu bure unataka hadi mfagio mwanao asipeleke shuleni??? Vitu vingine vidogo vidogo kama hivyo ni vya kawaida tu. Sasa wewe mfagio wa elfu moja nao unaona ni mzigo na gharama kubwa kununua?
Mifagio 1500 ya nn ?
Matofali 5x1500 yanaenda wapi ?
Majaba 1500 yanaenda wapi?
Mapanga 1500 yanaenda wapi ?
Hiyo ni kila mwaka huoni huo ni Wizi chini ya Serikali ya CCM
Kero zipo acha kujizima data
 
Lucas mwashambwa Kero nyingine ni hii hapa

MARA: Wafanyakazi zaidi ya 200 wa Mgodi wa Dhahabu wa Cata Mining Limited uliopo Kijiji cha Katalyo Wilayani #Butiama wamefanya mgomo na kulala katika ofisi za mgodi huo, wakishinikiza uongozi uwalipe malimbikizo ya mishahara na kuwaingizia malipo ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)

Kupitia barua yao ya wazi kwenda kwa Waziri wa Nishati wamedai hawajalipwa mishahara ya Novemba na Desemba 2023, pia wamekatwa makato ya #NSSF kwa miaka 7 lakini hayafiki katika akaunti zao na wanapofuatilia NSSF - Mara hawapewi ushirikiano

Alipotafutwa Mkuu wa Utumishi wa Mgodi, Richard Bendera hakupatikana kuzungumzia madai hayo

Soma Wafanyakazi mgodi wa CATA Mining Mara, waanza mgomo kushinikiza kulipwa mishahara, michango NSSF

#JFUwajibikaji #CivilRights #HumanRights #KemeaRushwa #Accountability #JamiiForums
 
Serikali yetu Sikivu imeshaipata taarifa hiyo na wote wenye kustahili haki watapata haki zao.jasho la mnyonge halipotei bure.
 
Mifagio 1500 ya nn ?
Matofali 5x1500 yanaenda wapi ?
Majaba 1500 yanaenda wapi?
Mapanga 1500 yanaenda wapi ?
Hiyo ni kila mwaka huoni huo ni Wizi chini ya Serikali ya CCM
Kero zipo acha kujizima data
Kwa hiyo unataka wakienda shuleni kwa mara ya kwanza wasiende na vifaa halafu wakatumie vifaa alivyoleta nani?
 
Wenzio tulivuka mwaka na utimamu wetu .

Wewe hata akili kidogo ulizokua nazo uliziacha 2023.

Uzi una maoni 81 ila robo tatu ni negative na unajidai huoni kwa kuvaa miwani ya mbao.

Huyo zero brain akatetemeshe mikoa hiyo kwa kipi wakati watu wana mgao wa umeme, maji na gharama za maisha zikiwa juu nadhani utakua unaota , yaani 7k ndio inawavua utu hivyo ni dalili tosha hali sio nzuri Tanzania.
Usiangalie wangapi wanapinga maana hata galileo alipingwa sana na watu ila mwisho ilikuja kufahamika kuwa alikuwa sahihi na walio wengi ndio walipotoka.
 
Weka ushahidi acha kuchafua watu hapa wewe. Marekani siyo Mungu.hao hao Marekani ndio walimuua Saddam Husseni kwa kisingizio kiwa anamiliki silaha za nyukilia.je uliziona au kuonyeshwa silaha hizo? Marekani waliuonyesha ulimwengu shehena ya silaha hizo? Vipi kuhusu muamari Gadaffi si hao hao walimuua kwa visingizio vya uongo baada ya kuona maono yake yanahatarisha maslahi yao na uwepo wao katika bara la Afrika? Hujawahi kusikia hata Barack Obama akikili Hadharani kuwa walifanya makosa kumuua Gadaffi? Sasa unaanzia wapi kuwaona kama miungu watu na kuwaamini kwa kila kitu? Za kuambiwa changanya na za kwako ndugu yangu.usiwe na akili kama kasuku au nyumbu.
Ndioaana unatukanwa sana na hata ukiropoti mods hawakutilii maanani wewe mjinga
 
Chawa on air!

Tuache kwanza tuko kusherehekea kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya chawa mwandamizi Kujamwi!

Tuache kwanza tupo Site kupiga picha za jumba la Kichawa!

Vipi Wa jina yako lini kuzinduliwa???
 
Back
Top Bottom