Paul Makonda na Mrisho Gambo wako katika vita kubwa Arusha

Paul Makonda na Mrisho Gambo wako katika vita kubwa Arusha

Heshima sana wanajamvi.

Mkuu wa Arusha Mh Makobda aka Bashite na Mbunge wa sasa Arusha Mjini Mrisho Gambo wapo katika vita kubwa ya kuomba ridhaa ya chama ya kuwania ubunge wa Arusha Mjini kupitia CCM.

Makonda kupitia harakati mbali mbali ikiwemo kuandaa utatuzi wa kero za kisheria hasa masuala ardhi.

Makonda kupitia sanaa ya hali ya juu kaandaa utaratibu wa kutoa matibabu na huduma za afya.

Mipango yote hii ina lengo ta kujijenga kwaajili ya uchaguzi mkuu 2025.

Wakati haya yakiendelea kambi ya Mbunge wa sasa Mrisho Gambo imeapa itapambana kufa na kupona kugakikisha Mrisho anatetea kiti cha ubunge kwa gharama zozote.

CCM kupitia kamati zake tayari wameshatuma taarifa za mtifuano huo na kushauri suluhu pekee ni kuanzisha majimbo mawili ya uchaguzi katika jiji la Arusha.

Ngongo kwasasa Kisiwani Mafia.
Makonda ni mtu wa kufuta ugomvi wakati wote, ingawa gambo naye wacha anyooshwe alipo kuwa mkuu wa mkoa arusha alijitutumua sana
 
CCM kupitia kamati zake tayari wameshatuma taarifa za mtifuano huo na kushauri suluhu pekee ni kuanzisha majimbo mawili ya uchaguzi katika jiji la Arusha.
Yaani majimbo mawili Arusha ili Makonda na Gambo wote wapate pa Kugombea, halafu wananchi wabebeshwe gharama za mishahara yao🤔😚

Hii CCM haitakuwa seriaz kuja na pendekezo hilo. Kwani wote wawili wasipokuwa wabunge nini kitakosekana Arusha?

Ila pia wakichagua Makonda itawafaa zaidi wanaArusha
 
Tatizo ni viwango vya elimu, viwango vikifanana ubishi kidogo. Vikitofautiana ubishi hautaisha.
 
Back
Top Bottom