Wakati Benjamin William Mkapa akiwa Mhariri wa Magazeti ya Serikali, akiwa katika kazi yake, alisikia maneno ya waziri mmoja, Oscar Kambona, akimsengenya rais, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Benjamin Mkapa hakupanda kwenye jukwaa lolote la kisiasa na kutoa habari hizo. Alimfuata rais Nyerere na kumpa hizo habari. Nyerere akamuhoji akitaka kujua uhakika wa habari hizo, kwa sababu aliona itakuwa vigumu sana kwa Kambona kumsema yeye Nyerere vibaya, akizingatia urafiki wao wa muda mrefu.
Kama mwanafalsafa aliyefuata methali ya Kirusi "Trust but verify", Nyerere alimuamini Kambona, lakini akataka kuhakiki mambo na kuweka watu waliomfuatilia, ambao walikuja kuthibitisha maneno aliyoyasema Mkapa kwa Nyerere.
Kilichofuata ni historia. Kambona alikimbia nchi na kwenda uhamishoni Uingereza alikokaa kwa miaka mingi sana.
Historia hii inatufundisha nini?
Kukosana viongozi kushawahi kutokea nchi hii, ila hakukutangazwa kwenye hotuba. Kutangaza kwenye hotuba ilikuwa ni papara inayoonesha kukosa mahesabu kama aliyokuwa nayo Benjamin William Mkapa.
Hii ndiyo tofauti ya mtu kama Mkapa aliyepanda ngazi mpaka kuwa rais na mtu kama Makonda ambaye anatafuta kiki za muda bila ya kuusoma mchezo wa muda mrefu.