Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Acha uongo kawadanganye walugaluga wenzako huko

Kambona na Mkapa wapi nawapi?
Hata Mimi nimewaza sana kwamba wakati kambona yupo madarakani mbona kama mkapa alikuwa TEENAGER early Twenties mleta hii stori atutajie mwaka tufanye hesabu vinginevyo utakuwa uongo mchafu
 
Hata Mimi nimewaza sana kwamba wakati kambona yupo madarakani mbona kama mkapa alikuwa TEENAGER early Twenties mleta hii stori atutajie mwaka tufanye hesabu vinginevyo utakuwa uongo mchafu
Ametoa source.
 
Wakati Benjamin William Mkapa akiwa Mhariri wa Magazeti ya Serikali, akiwa katika kazi yake, alisikia maneno ya waziri mmoja, Oscar Kambona, akimsengenya rais, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Benjamin Mkapa hakupanda kwenye jukwaa lolote la kisiasa na kutoa habari hizo. Alimfuata rais Nyerere na kumpa hizo habari. Nyerere akamuhoji akitaka kujua uhakika wa habari hizo, kwa sababu aliona itakuwa vigumu sana kwa Kambona kumsema yeye Nyerere vibaya, akizingatia urafiki wao wa muda mrefu.

Kama mwanafalsafa aliyefuata methali ya Kirusi "Trust but verify", Nyerere alimuamini Kambona, lakini akataka kuhakiki mambo na kuweka watu waliomfuatilia, ambao walikuja kuthibitisha maneno aliyoyasema Mkapa kwa Nyerere.

Kilichofuata ni historia. Kambona alikimbia nchi na kwenda uhamishoni Uingereza alikokaa kwa miaka mingi sana.

Historia hii inatufundisha nini?

Kukosana viongozi kushawahi kutokea nchi hii, ila hakukutangazwa kwenye hotuba. Kutangaza kwenye hotuba ilikuwa ni papara inayoonesha kukosa mahesabu kama aliyokuwa nayo Benjamin William Mkapa.

Hii ndiyo tofauti ya mtu kama Mkapa aliyepanda ngazi mpaka kuwa rais na mtu kama Makonda ambaye anatafuta kiki za muda bila ya kuusoma mchezo wa muda mrefu.
Unaweza kuwa Sawa ila kuna mambo kadhaa inabidi ujue..yawezekana aliyesemwa tayari anajua ila alitafuta namna ya kufikisha ujumbe Kwa watesi wake bila kuwadhuru..hapo umesema Nyerere alipogundua ikawa historia yeye na kambona..huyu alitaka kuwastopisha tu bila kuwafanyia ubaya wowote.
 
Kama alitaka kuwasimamisha kwa nini asiwaaambie au kuandaa kikao cha ndani kati yao mawaziri na rais?

Wewe bado huelewi kuwa hizi ni siasa for public consumption, sio tatizo la viongozi kutoelewana?

Hujaelewa kuwa hii ni kampeni ya 2025 ishaanza, ndiyo maana unasikia hizi habari na zile za Mabeyo?
 
MAKONDA MCHONGANISHI SANA ANEUMIZA WATU WENGI KIPINDI CHA UTAWALA KATILI WA MAGUFULI HAFAI KUWA KIONGOZI
Kama kweli Makunda ni mtu mwema na hasa alikuwa na lengo lakumsaidia Mama angefuata hatua hizi:
1: Angewafuata wale wote wanaomtukana na wanaolipa fedha Kwa watukanaji nakuwaambia siyo tabia njema kumtukana Rais , kama kunajambo wamwabie ili ajirekebishe.
2: Angemfuata Rais nakumwambia wazi wazi kuwa flani anamlipa Hela flani ili wakutukane, na watukanaji ni flani na flani waite waonye.
3: Angeweza pia kuwaambia watu wa intelligence wawafuatilie na wakomeshe tabia hiyo
 
Makonda anataka yeye ndiye awe chawa mkuu wa Rais Samia, anamlazimisha Rais amsikilize yeye sana kwamba yeye ndiye msema kweli, Mimi kwenye serikali yangu sitahitaji machawa wala watu wakujipendekeza kwangu” Hashim Rungwe

Huwezi kupata mtu wa kufanya nae kazi ambaye hajipendekezi kwako kama bosi. Hiyo ni kudanganya wasiojua.
 
Paul makonda lazima alikwea kizimba. Wengi hatujui nini kinahojiwaga na muhojiwa anapaswa kutwii vipi. Ila kwa Paul lazima atakuwa na kujiona ni mteule.

Kiufupi ajitathimini sio kila nyakati unapaswa kufanya kila kitu.

Nahisi saa 3 za mahojiano alipata kibano kwa maneno na kuona anaweza akafanya apendavyo.

Binafsi sion kama anafanya sawa au sisawa ila ana hulka ambayo sidhani kama ataicha... tabia zingine ni za kuzaliwa nazo. Huwez tegemea mtu akaiacha kirahisi.

Kimsingi tume ilipaswa kumuita tangu alivyoanza kuwapigia simu mawaziri.....

Moja wa mawaziri aliowapigia simu hadharani akitoa oda ni Mama wa afya bi Ummy...Huyu wa ardhi jamaa wa ukonga. Na baadhi wachache aliowamudu. Hakuweza kumpigia mH waziri mkuu na makamu mzee mpango. Ila nahisi alitamani apande juu juu zaidi yao.wote isipokuwa Mama pekee.

Kwa hiyo siamini kuwa atakuja badilika japo masaa aliyowekwa si kitu chepesi. Alitoka jasho
 
Waha ndio chawa wakuu kuanzia kwa CMG mpaka wa Wasafi utawakuta... na yeye anajisogeza taratibu kila apato nafasi
 
Paul makonda lazima alikwea kizimba. Wengi hatujui nini kinahojiwaga na muhojiwa anapaswa kutwii vipi. Ila kwa Paul lazima atakuwa na kujiona ni mteule.

Kiufupi ajitathimini sio kila nyakati unapaswa kufanya kila kitu.

Nahisi saa 3 za mahojiano alipata kibano kwa maneno na kuona anaweza akafanya apendavyo.

Binafsi sion kama anafanya sawa au sisawa ila ana hulka ambayo sidhani kama ataicha... tabia zingine ni za kuzaliwa nazo. Huwez tegemea mtu akaiacha kirahisi.

Kimsingi tume ilipaswa kumuita tangu alivyoanza kuwapigia simu mawaziri.....

Moja wa mawaziri aliowapigia simu hadharani akitoa oda ni Mama wa afya bi Ummy...Huyu wa ardhi jamaa wa ukonga. Na baadhi wachache aliowamudu. Hakuweza kumpigia mH waziri mkuu na makamu mzee mpango. Ila nahisi alitamani apande juu juu zaidi yao.wote isipokuwa Mama pekee.

Kwa hiyo siamini kuwa atakuja badilika japo masaa aliyowekwa si kitu chepesi. Alitoka jasho
ndani ya masaa ma 3 kikaangoni alikuwa akiwasiliana na maza kwa sms
 
Back
Top Bottom