Pendekezo: Dkt. Hassan Abassi afukuzwe kazi kwa kiburi cha kukataa amri halali ya Rais wa Nchi

Bado udini upo Tanzania ,Dr Abbas yupo sahihi raid hajatamka magazeti na pia waliyofungiwa ni kwa mujibu wa Sheria Sasa mnataka yeye avunje Sheria.kwani nchi inaongozwa kwa tamko la raisi au Sheria ?
 
Huyu nyumbu ndie alikuwa kiherehere wa kufungia vyombo vya habari. Na sasa anaongea kama nani?
Maana sio waziri wahii wizara.
Tuna muomba Mh. Rais amzengue.
 
Nilikuwa wa kwanza kupendekeza Abbass ahamishwe Wizara ya Habari
 
Sasa ni zamu ya Rais Samia Suluhu Hassan kuamua awe upande gani...

Wa Wahafidhina wa CCM kama huyu Abbas na kundi lililo nyuma yake au upande wa sauti za wananchi...

Yaani hapa taratibu mitego na mishale inaanza kuachiliwa kwa huyu Rais mama Samia S.H. Akikaa vibaya, asipokuwa bold, atanasa na taratibu kuanza kupotea...

Maamuzi sahihi ni kuendelea ku - maintain mwanzo mzuri wa uongozi wake na itakuwa ni ushindi kwake...

Maamuzi mabaya yakiongozwa na ushauri potovu wa wasaidizi wake kama huyu Abass, atakuwa anaenda kinyume na matakwa ya watu...

Atafuata njia ya Mwendazake John P. Magufuli ya kufa kiroho na kimwili kwa sbb ya kupuuza sauti za umma/watu/wananchi...

Mungu Yehova na amsaidie mama huyu kwa kumpa HEKIMA na BUSARA sawasawa na Mfalme Sulemani alivyopewa na Bwana Mungu ktk kutawala na kuamua kwake...
 
Abasi kwanza sio msemaji wa Serikali na wala sio Waziri wa Habari. Kiherehere sana huyu kiumbe. Mama fukuza huyu mtu.
Si ndiye Katibu mkuu wa wizara inayoshughulikia habari?

Ofcoz, kwa upotoshaji huu waziri (boss) wake achukue hatua haraka kumrekebisha Katibu mkuu wake Vnginevyo watapotea wote, yeye waziri na Katibu wake..!
 
Atumbiliwe tuzalishe kigogo mwingine!
 

Ukimwona mwambie ajifunze taratibu za utendaji

Hicho alichokiandika hapo alitakiwa kukisema kabla Rais hajaongea na hapo tungemuelewa... hii inamjengea sura ya kupingana na Rais kitu ambacho sio sawa

Kama hajui protokali aelewe kwamba rais na hata mkuu mwingine mwenye mamlaka ya mwisho akishaongea ndio amemaliza, labda rais mwenyewe arudi kuongea vinginevyo
 
Bado udini upo Tanzania ,Dr Abbas yupo sahihi raid hajatamka magazeti na pia waliyofungiwa ni kwa mujibu wa Sheria Sasa mnataka yeye avunje Sheria.kwani nchi inaongozwa kwa tamko la raisi au Sheria ?
umeandika hapa as if umeshuka leo kutoka London au umezaliwa leo, kwani hayo matamko si ndio trend yetu TZ
 
Ngoja tuone.

PhD inaposhindwa kutafsiri maana ya vyombo vya habari.

PhD inasema gazeti siyo chombo cha habari.

PhD inambishia Rais ambaye ni taasisi.

PhD inachanganya itikadi na maswala ya kiserikali.

Ngoja tuone.

Ukinizingua Nakuzingua!
Kweli wewe umebadilika na unaenda na wakati!
 
umeandika hapa as if umeshuka leo kutoka London au umezaliwa leo, kwani hayo matamko si ndio trend yetu TZ
Tatizo tulilonalo wa tz ni kumuhukumu mtu tusiyempenda kosa Hilo Hilo likifanywa na tunayempenda tunapongeza hii ndio shida.Katibu mkuu katekeleza agizo la rais kwa mujibu lilivyotoka bado mnamlaumu .Swali fikirishi he Kuna vyombo vilifungiwa bila kufata Sheria?na Kama Sheria ni kandamizi je tatizo ni lamsimamiaji wa Sheria au watunzi wa Sheria? na pia siku zote mmekuwa mkiimba wimbo kuwa Rais afate Sheria na hayuko juu ya Sheria Sasa mmesahau Kama vyombo vya habari vilivyofungiwa ni kwa mujibu wa Sheria?tunatatizo kubwa Sana watz la ubinafsi na kupenda maslahi binafsi
 
huyu naye poyoyo tu bado haamini kwamba jiwe hatunaye tena; kwa hiyo tuseme yale maneno ya mama yalikuwa unabii sasa yeye ndo anatafsiri
 

Leo Mama D naona umelala vizuri na mumeo...

Ni ngumu kuamini kuwa this time unakosoa maamuzi ya mwanaCCM mwenzako Abass...!!

That's absolutely very good mama..

Haya ni mabadiliko mazuri ya kifikra. Kongole..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…