Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Penina Methody (27) ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kinachodhaniwa ni panga, chanzo kikidaiwa ni wivu wa mapenzi.
Tukio hilo linalodaiwa kufanywa na mtu anayedaiwa ni mpenzi wake limetokea jana Alhamisi, Mei 23, 2024 Goba Centre, Wilaya ya Kinondoni anapofanyia biashara zake Penina.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema leo Ijumaa Mei 24 2024 kuwa watatoa taarifa kamili kuhusu tukio hilo.
Akisimulia tukio hilo mmoja wa bodaboda aliyekuwa akimbeba Penina amesema siku nne kabla ya kuuawa, Penina na mwanamume mmoja walipigana kwa kurushiana chupa.
Chanzo: mwananchi_official
Nilikuwa sijaona Picha yako ila kwa kuiona kupitia Mwananchi sasa naanza Kuelewa kwanini Msukuma Kakudedisha.