😀😃😃😃😄😄 Kanisa ni msamaha na sio biashara
 
Barua anayotumia Wakili kibatala ni feki

Ndio maaba hadi waziri kaikana

Barua halali waliyopelekewa Kanisani kwa Gwajima walikataa kupokea

Hiyo ya mitandaoni sio yenyewe

Waliyokataa kupokea ndio yenyewe
 
haya ndio madhara ya kuwa na askari wenye uwezo mdogo kiakili walikurupuka kwenda kufunga na kuzuia watu eneo la kanisa bila kujua uhalali wa barua
Barua halali iliyopelekwa na mamlaka halali walikataa kupokea .Hiyo ya mitandaoni anayotumia huyo wakili ni feki

Barua halali ni ile walikataa kupokea
Mkuu wa wilaya huyu hapa akiongea kuwa walipelekewa wakakataa kupokea
Ndio ikatungwa na wahuni hiyo inayozunguka mitandaoni na wakili kaibeba kichwa kichwa.Ndio maana hata waziri kaikana hiyo ya mitandaoni

Msikilize mkuu wa wilaya akiongea kuhusu Barua official waliyokataa kupokea

View: https://youtu.be/Kc0xJhHm-zg?si=GUUX0WJbpoese6uI
 
Sawa mahakama walitoa uamuzi gani jana kuhusu hiyo barua?
 
Lucas Mwashambwa aione kwenye box lake la ngonjera, mpumbavu yule
 
Wajitie hamnazo hivyo hivyo,barua iko addressed kwa mkuu wa hayo makanisa,na ujumbe umefika...waende juma pili tuone kama kweli wao ni vizibo
Lini unaenda kuwasaidia nduguzo huko Iran!?
Hujajiunga bado na walinzi wa mapinduzi!!?
Wahi ukawatetee upate bikira 72.
 
WAZIRI BASHUNGWA AKIRI: BARUA ILIYOFUNGIA KANISA LA GWAJIMA SIO HALALI

Wadau,
Pokeeni nakala ya majibu kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani kwenda kwa wakili wa Kanisa la Askofu Dkt. Josephat Gwajima.

Majibu haya yanathibitisha jambo zito sana: Kanisa halijapewa barua rasmi ya kufungwa. Barua iliyosambaa mitandaoni imekanushwa na Serikali kuwa sio ya kwao. Waziri mwenye dhamana hawezi kueleza wazi chanzo chake, wala kuelewa kinachoendelea kwenye sakata hilo.

Kwa hali hii, ninathibitisha bila kupepesa: kuna serikali kivuli nchini — Serikali ya KIHUNI, inayoendeshwa KIHUNI.

Polisi walio chini ya wizara ya waziri huyo wanaonekana kutekeleza maagizo ambayo hayajatolewa na Serikali halali. Inawezekana maagizo hayo yanatoka kwa “copy” ya Serikali — kundi lisilo halali lililojipa mamlaka ya kuendesha nchi kama serikali kivuli.

Kwa nini waziri hajui kinachoendelea kwenye jambo sensitive la kiwango hiki? Hii ni dalili ya wazi kwamba kuna nguvu ya kihuni imejipenyeza ndani ya mfumo wa dola, na inaendesha baadhi ya maamuzi kwa niaba ya Serikali bila ridhaa yake. Serikali ya kihuni ina nguvu kuliko serikali tuliyoichagua. Wahuni wanaogopwa na wenye mamlaka.

Kwa sasa, hali hii ni tishio kubwa kwa Taifa.

MASWALI MAZITO YANAYOIBUKA:

#1. Nani aliandika na kusambaza barua hiyo ya kufungia kanisa?

#2. Kwa mamlaka gani hatua hiyo ilichukuliwa pasipo taratibu za kisheria?

#3. Kwa nini Waziri hana majibu ya msingi juu ya tukio linalotokea ndani ya wizara yake?

#4. Je, kuna kundi la watu wanaojiendesha kama Serikali, wakichukua hatua kubwa bila idhini ya Serikali halali?

Inavyoonekana, kuna hali ya sintofahamu ya kiuongozi nchini. Kuna nguvu za kihuni zinazojificha nyuma ya kivuli cha dola, zikijiendesha kwa jina la Serikali lakini kwa malengo yasiyojulikana wala kudhibitiwa.

Hili ni tishio la wazi kwa demokrasia, haki za raia, na uhuru wa kuabudu. Ni lazima Watanzania wote wenye uchungu na nchi hii waamke, waulize maswali, na kudai uwajibikaji wa kweli kutoka kwa wale waliopewa mamlaka kwa mujibu wa Katiba.

TUNATAKA MAJIBU RASMI.

Hatukubali kuongozwa na serikali kivuli iliyo mikononi mwa wahuni.
Uongozi wa Taifa hili hauwezi kuachwa kwenye mikono ya watu wasio na dhamira ya kulinda haki, amani, na utawala wa sheria.
 
Attachments

Kwenye jamii zinazojitambua kama ni kweli hayo ni majibu ya Bashungwa basi alipaswa kwa haraka sana kuachia ofisi ya umma!
 
Kwahiyo wale askari wanaozuia shughuli za kanisa wanatekekeza amri haramu ya serikali?
 
Haya aliyasema Ndugai kuwa Nchi ilishapigwa mnada. Kilichofuatiwa aliambiwa ni marufuku kulivaa lile joho lenye blue blue.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…