PICHA: Naombeni kujua huu ni ugonjwa gani unaotutesa hivi mimi na familia yangu

pole mkuu hiyo ni Syphilis is a systemic disease wahi kituo cha afya utapona tu

Mkuu hebu nijibu kule bwana nmekuuliza swali, badala yake umekimbilia kuipa presha familia ya jamaa kuwa ina kaswende 😂😂😂
 
Huu ugonjwa ulitutokea wate mm na mke na watoto Ila nimetumia dawa mbalimbali lakini huu mwezi wa tatu naona tunaendelea kujikuna

Hasa kwa watoto wangu hasa pia usiku wanajikuna Sana tulienda hospitali hawakutupima Ila tu tuliambiwa dawa za kununua za kuchua.

Kama Kuna mtu anisaidie maana watoto ndo zaidi inawaathiri,

Ulianzia kwa mtoto Kisha kwamama na mm wa mwisho.

Sasahivi ndo najaribu dawa ya kimasaiView attachment 3190231View attachment 3190232View attachment 3190233
img_20250101_204446_420-jpg.3190234
Scabies Hiyo. Kiswahili wanaita Ukurutu

Tumia Scaboma (Lindane) Lotion. Kwa watu wazima na watoto juu ya mwaka mmoja

Familia nzima ifue nguo zote, mashuka pamoja na kuvacuum kitanda.

Scabies ni infestation, ukitibu pekee bila kufanya usafi wa hali ya juu, itarudi tena
 
Huu ugonjwa ulitutokea wate mm na mke na watoto Ila nimetumia dawa mbalimbali lakini huu mwezi wa tatu naona tunaendelea kujikuna

Hasa kwa watoto wangu hasa pia usiku wanajikuna Sana tulienda hospitali hawakutupima Ila tu tuliambiwa dawa za kununua za kuchua.

Kama Kuna mtu anisaidie maana watoto ndo zaidi inawaathiri,

Ulianzia kwa mtoto Kisha kwamama na mm wa mwisho.

Sasahivi ndo najaribu dawa ya kimasaiView attachment 3190231View attachment 3190232View attachment 3190233
img_20250101_204446_420-jpg.3190234
Kapimeni kaswende. Sijasema mna kaswende.
 
Kiongozi kabla hujaingia gharama, kimbia duka la dawa chap kanunue dawa ya maji inaitwa BBE nunua hata vichupa vitatu. Hakikishga imeandikwa BBE juu wasikudanganye sijui chukua mbadala au sijui kuna nzuri zaidi; waambie unataka BBE kama hana wewe tafuta duka jingine (hiyo infection ni Scabies)

Nakumbuka tulipata sakata kama hilo enzi hizo nikiwa shule ya bweni; kuna wanafunzi walitokea huko makwao vijijini (kipindi kile tulichanganywa nchi nzima) wakaja na huo msala, hakuna rangi tuliacha kuona....
Huwezi kuamini pamoja na kutumia dawa za kila aina tulikuja kuponeshwa na BBE
Oga na maji ya moto jikaushe halafu paka mwili mzima... isiingie kwenye macho

Anza nayo ikikataa ndio uchukue hatua zaidi....
 
Huu ugonjwa ulitutokea wate mm na mke na watoto Ila nimetumia dawa mbalimbali lakini huu mwezi wa tatu naona tunaendelea kujikuna

Hasa kwa watoto wangu hasa pia usiku wanajikuna Sana tulienda hospitali hawakutupima Ila tu tuliambiwa dawa za kununua za kuchua.

Kama Kuna mtu anisaidie maana watoto ndo zaidi inawaathiri,

Ulianzia kwa mtoto Kisha kwamama na mm wa mwisho.

Sasahivi ndo najaribu dawa ya kimasaiView attachment 3190231View attachment 3190232View attachment 3190233
img_20250101_204446_420-jpg.3190234
Scabies hii mkuu,mdau aliekwambia BBE yupo sawa, ila zingatia kuoga na kubadilisha nguo mashuka kila baada ya kupaka, izo nguo zifue na kuzipiga pass kabla ya kuzivaa ,au kuzitumia.

Yupo mmja kati yenu alieanza kupata na ameambukiza familia nzima
 
Nilipata binti wa kazi kutoka Malawi alivyofika nikaona muda wote anajiparua ngwala ngwalaa, nikamtazama nikamkuta na huo ugonjwa km wenu.!!
Nikampeleka hospital wakamfanyia vipimo wakamchoma sindano lakini tatizo likawa bado..!

Akaanza kupoteza hamu ya kula ulimi nao ukapatwa hivyo vipere, tukarudi tena wakampa dawa za antibiotique na BBE ya kupaka.. ikawa bado.!

Kuna mmama akaniambia kanunue kiberiti upele achanganye kwenye mafuta ya mgando apake asubuhi na jioni akitoka kuoga.!! Huwezi amini binti yangu alipona kwa dawa ya buku tu.!! Unaweza kujaribu na wewe.!
 
Huu ugonjwa ulitutokea wate mm na mke na watoto Ila nimetumia dawa mbalimbali lakini huu mwezi wa tatu naona tunaendelea kujikuna

Hasa kwa watoto wangu hasa pia usiku wanajikuna Sana tulienda hospitali hawakutupima Ila tu tuliambiwa dawa za kununua za kuchua.

Kama Kuna mtu anisaidie maana watoto ndo zaidi inawaathiri,

Ulianzia kwa mtoto Kisha kwamama na mm wa mwisho.

Sasahivi ndo najaribu dawa ya kimasaiView attachment 3190231View attachment 3190232View attachment 3190233
img_20250101_204446_420-jpg.3190234
Poleni sana. Huo ugonjwa unajulika kitaalamu kama SCABIES, kwa kiswahili unaitwa UKURUTU. Huwa unasababishwa na mdudu anaeitwa sarcoptes scabiei.

Ni very contagious, yaani unaambukiza sana, thus why makundi yanayoathirika zaidi ni watoto (kwa sababu watoto wanatabia ya kucheza wengi kwa pamoja), sehemu zenye mkusanyiko mkubwa wa watu kwa mfano jela au mabwenini.

Dalili yake kubwa ni muwasho hasa usiku, kwa sababu hawa wadudu wana tabia inayofanana na parasites (minyoo) inayoitwa diurnal variation, simple explanation ni kwamba wanakuwa active zaidi usiku, jambo linalopelekea mtu kukosa usingizi.

Tiba yake ya kwanza ni USAFI: Kwa maana ufanyike usafi wa nyumba nzima, ikiwemo nguo na mashuka.. vyote vifuliwe kwa maji ya moto, vianikwe juani na mwisho vipigwe pasi na moto mkali, lengo likiwa ni kuuwa wadudu wote waliopo kwenye mavazi/malazi ktk sehemu mnayoishi.

Kucha zikatwe, kuanzia watoto mpaka kwa wazazi. Kwa sababu unapojikuna unawaamisha wadudu kutoka sehemu moja ya mwili kwenda kuchani kisha kuwasambaza sehemu nyengine ya mwili au kumwambuliza mwengine.

Mwisho kabisa kuna dawa ya kupata mnayopaswa kutumia familia nzima, inaitwa BBE. Maelekezo ya namna ya kupata mtapewa hospitali/dispensary.

Kama muwasho ni mkali sana, kunaweza kukawa na ungezeko la dawa kama hydrocortisone au cetrizine hydrochloride.

Good luck!
 
Huu ugonjwa ulitutokea wate mm na mke na watoto Ila nimetumia dawa mbalimbali lakini huu mwezi wa tatu naona tunaendelea kujikuna

Hasa kwa watoto wangu hasa pia usiku wanajikuna Sana tulienda hospitali hawakutupima Ila tu tuliambiwa dawa za kununua za kuchua.

Kama Kuna mtu anisaidie maana watoto ndo zaidi inawaathiri,

Ulianzia kwa mtoto Kisha kwamama na mm wa mwisho.

Sasahivi ndo najaribu dawa ya kimasaiView attachment 3190231View attachment 3190232View attachment 3190233
img_20250101_204446_420-jpg.3190234
Tetekuanga hiyo kanunue B.B.E mjipake ila mvumilie liharufu lake
 
Back
Top Bottom