PICHA: Naombeni kujua huu ni ugonjwa gani unaotutesa hivi mimi na familia yangu

PICHA: Naombeni kujua huu ni ugonjwa gani unaotutesa hivi mimi na familia yangu

Huu ugonjwa ulitutokea wate mimi na mke na watoto Ila nimetumia dawa mbalimbali lakini huu mwezi wa tatu naona tunaendelea kujikuna

Hasa kwa watoto wangu hasa pia usiku wanajikuna Sana tulienda hospitali hawakutupima Ila tu tuliambiwa dawa za kununua za kuchua.

Kama Kuna mtu anisaidie maana watoto ndo zaidi inawaathiri,

Ulianzia kwa mtoto Kisha kwamama na mimi wa mwisho.

Sasahivi ndo najaribu dawa ya kimasaiView attachment 3190231View attachment 3190232View attachment 3190233
img_20250101_204446_420-jpg.3190234
Ni mimi sijaelewa hapo au mkuu ulimaanisha dawa ya tube na si kuchua.

Tatizo la ngozi lipo sensitive sana mkuu kwann usiende Moja kwa Moja kwa daktari wa masuala ya ngozi,ili ajue tatizo nn kupitia vipimo.

Kama ni allergy mtajua kitu mnachotumia kwa kula au kwa vyovyote kinacholeta allergy.

Pia Kuna maambuzi ambayo Mmoja wenu huenda ametoka nayo nje,pengine ni watoto au na nyie wazazi,tunatembea mazingira tofauti na kukutana na watu tofauti.

Ni ushauri wangu tu.
 
Hao ni scabies wataanza kuwatafuna hadi sehemu za siri. Hao wadudu usiku ndio kama wanaamka ndio muwasho unazidi.
Unaweza kupata hao wadudu kwa kufanya mapenzi bila kinga ukaondoka na vimelea, au kumkaribisha mtu mwenye hao wadudu akalala nyumbani kwako au kushare nguo.

Dawa ni utafute kwanza sabuni ya tertemosol (jina sina hakika na spelling) Kisha nenda Duka la madawa lolote Ununue dawa inaitwa BBE ni sh 2000 tu.

Kisha muoge vizuri na maji moto asubuhi na usiku mkienda kulala kisha mnajipaka hiyo BBE mwili mzima na kwenye vipele isiingie machoni au mdomoni maana inawasha sana.

Cha kuzingatia usafi usafi usafi hakikisha shemeji anafanya usafi wa maana kuanzia hayo mashuka nguo mnazo vaa hadi kwenye viti maana hao vimelea wamejaa humo bila usafi Hao vimelea hawawezi kuisha suuza mashuka hata kwa maji moto, tumia sabuni kufanya usafi, hakikisha nguo mnazo vaaa hasa za ndani mnapiga pasi ndio mnazi vaa.

Ukifanya hivyo tatizo litakwisha huo ugonjwa ulitaka kunimalizia pesa kwenye mahospital makubwa nikudhani ni magonjwa ya zinaa kumbe ni hao scabies nilipona ndani ya siku mbili baada ya kufanya hayo hapo juu
 
Hiyo ni pumu ya ngozi inayoelekea kwenye aleji. Utatumia mimea ya kunywa na kupaka ukichanganya na mafuta ya zaituni. Kwa ushauri zaidi 0713 039 875
 
Scabies. Pamoja na yoooote utakayofanya hakikisha bafuni kunakuwa safi unyevuunyevu na ndo mnazotumia kuogea kama hamna shower hakikisha ni safi. Tibu maji ya kuoga ni vyema kuoga maji ya vuguvugu. Then jikaushe vizuri.
 
Kama upo Arusha.. nenda haraka avinta care medical centre- ipo matunda ( panda daladala za moshono mwambie akushushe matunda). Kama unatokea USA RIVER shuka philips mwambie toyo akupeleke avinta care hapa matunda

Pont zingine tofauti na hizo hapo juu shuka stand ya daladala kilombero chukua daladala za moshono

nb.. barabara ya vijana road kama utatumia google map point avinta care

Ukifika. Muulizie daktari bingwa wa ngozi anaitwa dr consolata hata kwa bima unamuona
 
Je,hivi pia vinaweza kutibiwa Kwa dawa Gani?? Vipo mikononi,kifuani na vichache mgongoni.
Vinatokeza kama chunusi.
 

Attachments

  • PXL_20250102_061741750.jpg
    PXL_20250102_061741750.jpg
    438.2 KB · Views: 3
Huu ugonjwa ulitutokea wate mimi na mke na watoto Ila nimetumia dawa mbalimbali lakini huu mwezi wa tatu naona tunaendelea kujikuna

Hasa kwa watoto wangu hasa pia usiku wanajikuna Sana tulienda hospitali hawakutupima Ila tu tuliambiwa dawa za kununua za kuchua.

Kama Kuna mtu anisaidie maana watoto ndo zaidi inawaathiri,

Ulianzia kwa mtoto Kisha kwamama na mimi wa mwisho.

Sasahivi ndo najaribu dawa ya kimasaiView attachment 3190231View attachment 3190232View attachment 3190233
img_20250101_204446_420-jpg.3190234
Tumia dawa moja inaitwa SAFI ni bidhaa kutoka kwenye kampuni ya Hamdard india inafaa sana kwenye magonjwa ya ngozi inasafisha damu niliwahi kutumia nikapata matokeo mazuri
 
Huu mwezi wa 3? Familia yote? mmetumia dawa sana? Mkuu Nenda kanisani kama upo DSM pale mwenge mpakani kwa Prophet Nyakia.Utapona wewe na familia yako na kuambiwa chanzo.
Nimeona na kushuhudia watu wakipona.
Kuna kitu hakipo sawa kwenye huo ugonjwa umepigana na mwilini umeshindwa Basi nenda ukatatuliwe kwa mambo ya rohoni.

Usidharau hii.!
Acha ujinga basi....
 
Ninafikili ungeangalia maji unayotumia kuoga unayachota wapi,


Kama umechimba kisima je kipo umbali gani na choo??
 
Back
Top Bottom