Nyoosha maelekezo kaka shida ni nipone
Hahaha Mkuu Pole bana ,tatizo ni dogo Wala usipanick.
Tatizo lako Hilo dogo linaitwa SCABIES .
Huwapata zaidi watu walio kwenye eneo lenye uhaba wa Maji , na msongamano wa watu wengi na usafi duni kwa wanadamu na mazingira Kwa ujumla.
Hivo matibabu yake kwanza ni lazima yaanzie kwenye vichocheo vya tatizo Hilo pamoja matibabu husika ya tatizo .
Nunua Dawa zifuatazo.
1//Tetmosol Soap ( SABUNI ya Tetmosol) utakalokua Unatumia Kuoga, hivo Kila mwanafamilia awe nasabuni yake . Ukikoswa Haina shida.
2//Nunua dawa inaitwa Benzyl Benzoate Emulsion 10% BBE , ni Chupa yenye dawa asili ya kimiminika,, kabla ya kuitumia, KILA MMOJA AOGE KWA MAJI VUGUVUGU na ATUMIE SABUNI YA TETMOSOL KAMA UMEIPATA, , Kisha tumia Taulo safi ,ujifute maji mwili wote.
Baada ya hapo, PAKAA DAWA MWILI MZIMA , kuanzia miguuni Hadi Shingoni na kichwan nyuma ya masikio ,,ISIPOKUA USONI, USIPAKE DAWA HIYO USONI AU MDOMONI, AU UKENI AU HAJA KUBWANI, " ILA WAWEZA IPAKAA KWENYE UUME ULIOATHIRIWA.
Dawa hiyo unaipakaa mara Moja tu Ndani ya Masaa 24 tu basi.
3// Nunua Dawa inaitwa CALAMINE LOTION 8% au 15 % , hii utaipakaa Kila baada ya Masaa nane Kila siku mpaka muwasho utakapokua umeisha.
4//Kwakua hali hiyo inamuda mrefu ni wazi mmeshapata machafuko wa Damu, na hivo mnatakiwa mpate Dawa za Antibiotics kulingana nanyi angalau Kwa siku Tano.
5// Kwakua Ina muda mrefu, itakua vema pia mkipata dawa hizi za vidonge
---mojawapo ya Cetirizine , au Loratidine
Pamoja na Prednisolone Kwa dozi ya siku zisizopungua 5 na dozi ziendane na mtumiaji.
SASA , Ile ya kupakaa nmesema unaipakaa mara Moja tu Kwa siku Moja, inamaana kesho yake unaoga vizuri unaendelea kuoga Kwa SABUNI yako, kupakaa CALAMINE LOTION na dawa nyingine za kumeza.
IKIFIKA SIKU YA 4 , RUDIA TENA KUIPAKAA DAWA BBE HIYO KAMA MWANZO...Kwann urudie?? Ule mpakao wa mara ya kwanza Huwa HAUNA UWEZO WA KUUA MAYAI , hivo baada ya mpako wa kwanza Yale Mayai hujiangua na kuendeleza tatizo, Ivo MPAKO wa Pili ni lazima ., yaan Kwa Ufupi unaweza pakaa siku ya 1 Kisha ya 4 na malizia ya 7.
Mengineyo.
Toa nguo zenu zote nje, mashuka ,makava ya magoro , makava ya makochi .
Chemsha Maji ya moto,.Kisha loweka hizo zote kwenye maji hayo ya moto baadae uanikie juani .
Nunua Dawa za kuua wadudu ,hata hizi RUNGU AU HIT ,Puliza Ndani kote hasahasa kwenye Kona za nyumba, uvungu wakitanda , makochi n.k .
UTAPONA WEWE NA FAMILIA YAKO NA HAKUTAKUA TENA NA MAAMBUKIZI HAYO .