Picha nzito ya historia ya evolution ya mtu mweupe. Sisi bado tupo na maswali ya namna ya kufanya zindiko zuri la utumbo wa samaki ili kupata wateja.

Picha nzito ya historia ya evolution ya mtu mweupe. Sisi bado tupo na maswali ya namna ya kufanya zindiko zuri la utumbo wa samaki ili kupata wateja.

Nafasi bado ipo.

Tukisema “tumechelewa kufanya mambo makubwa kama taifa” tunajifungia kwenye historia kana kwamba kila fursa ilikuwa na deadline.

Angalia Marekani mwanzoni mwa miaka ya 1900. Kulikuwa na tatizo kubwa la afya ya kinywa na tabia ya watu kutopiga mswaki. Haikutosha kusema “watu hawana utamaduni wa usafi.” Walitambua tatizo, wakatengeneza bidhaa, wakaelewa psychology ya tabia, na wakafanya kampeni zilizosaidia kubadili habit ya jamii.

Hapa ndipo hoja ya Yuval Noah Harari kuhusu “marriage with science” inapokuwa interesting: jamii inaweza kukutana na tatizo, ikakubali kwamba haijui, kisha ikaamua kulichunguza kisayansi na kujenga uwezo wa kulitatua.

Kwa hiyo swali si:

“Kwa nini Tanzania tumechelewa?”

Swali ni:

Ni matatizo gani makubwa tunayoyaona leo ambayo dunia bado haijayatatua vizuri—na tunaweza kuyageuza kuwa systems, businesses, technologies na institutions?


Kuchelewa si mwisho wa mchezo.

Wakati mwingine kuwa nyuma kwenye jambo fulani maana yake ni kwamba bado una nafasi ya kujifunza kutoka kwa waliokwenda mbele—na kuruka baadhi ya hatua walizopitia.

Nafasi bado ipo.
SIKU MOJA IWE HIVI
 
Watu wengi wanafikiri ni rahisi kutengeneza program za ndege za kivita,makombora ya masafa marefu na madude mengine mengi ya kivita.
Ukiona Iran au North Korea wakitengeneza hayo madude ni kwa kutumia ubabe wao binafsi,wamekubali vitisho vya vikwazo.
Hata baadhi ya nchi za ulaya hazina uwezo mkubwa wa kutengeneza hizo ndege ila badala yake zinanunua toka US.
Bado US anataka aonekane yeye ndiye Giant kwenye teknolojia yote
 
Back
Top Bottom