PICHA: Rais Samia aongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu ya Dar es salaam

PICHA: Rais Samia aongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu ya Dar es salaam

Akhsante sana kwa kudhihirisha utaahira wako leo.
Unajua maana ya gharama!???
Mafuta ya gari.
Posho za safari.
Viongozi wetu wanajadili mambo ya muhimu na msingi halafu wewe unaanza kuleta na kuwaza habari za posho. Inaonyesha wewe unawaza tumbo lako tu.
 
Hayo maji mbona sionagi wakinywa
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge.

Ameongoza Kikao kizito cha Baraza la Mawaziri Ikulu ya Dar. Ambapo hii inakuja akiwa Ametoka kufanya ziara nzito na yenye mafanikio makubwa sana kanda ya ziwa kwa Mikoa ya Simiyu na Mwanza. Ambapo akiwa katika ziara hiyo aliweza kuzindua miradi mbalimbali mikubwa ya maendeleo ambayo imeleta nuru na Tabasamu kwa wananchi wa kanda ya ziwa.

Ambapo miradi hiyo ni ile ya Maji, Miundombinu,Elimu N.k.pamoja na kuzindua kiwanda . Lakini pia Alikagua miradi mbalimbali na kutembelea maeneo mbalimbali pamoja na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara. ambayo ilishuhudia mafuriko ya watu waliofurika kwa wingi kuwahi kushuhudiwa hapa Nchini. Hii yote ikitokana na kukubalika ,kupendwa na kuaminika mbele ya watanzania.

Sasa pasipo kupumzika wala kukaa Rais wetu Mpendwa Ameendelea na kuchapa kazi kwa kufanya na kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri. Ambapo ni katika vikao vya aina hiyo mambo mazito yenye kutoa muelekeo wa Nchi na masuala mbalimbali hujadiliwa. Hii ndio raha ya kuwa na kiongozi anayejua wajibu wake,aliyejitolea Maisha yake kwa ajili ya kuwatumikia watu.

Hii ndio Faida ya kuwa na kiongozi ambaye ametanguliza mbele maslahi ya wananchi. ndio maana anafanya kazi usiku na mchana paspo kupumzika wala kusema hizi ni siku za mapumziko. Muda wote Mama yetu yupo kazini. Kwake Maisha yake ni kwa ajili ya kuleta majawabu na majibu kwa watu,ni kwa ajili ya kuinua maisha ya watu, ni kwa ajili ya Kugusa Maisha ya watu na kuleta matokeo chanya. Muda wote Rais wetu Mpendwa anapanga mipango kwa ajili ya kuboresha Maisha ya watanzania.

Kwake ikulu ni Sehemu ya kutoa njia na kutoa maelekezo ya namna ya kutatua kero za wananchi,ikulu kwake ni Sehemu ya kuwashia taa ya kuangaza njia za watanzania katika uchumi wao na maisha yao. Kwake Ikulu ni Ofisi ya watanzania wote kwa ajili ya kotoa huduma na kuwapelekea Watanzania mahali walipo. Moyo wake muda wote upo kwa watanzania. Huo na hiyo ndio maana halisi ya Utumishi kwa ajili ya watu. View attachment 3379031

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
ngwa
 
Viongozi wetu wanajadili mambo ya muhimu na msingi halafu wewe unaanza kuleta na kuwaza habari za posho. Inaonyesha wewe unawaza tumbo lako tu.
Pole, hujawahi kuwa kwenye uga wa huo ujue pesa zinapigwaje.

Hao wote hapo wametoka na posho za maana kama hujui.

Mpaka ufikie level za Katibu Mkuu wa wizara ndiyo utajua haya mambo kijana, wewe endelea kuwaimbia mapambio wenzako wanapiga pesa.
 
Wewe endelea kutanguliza na kuwaza njaa za tumbo lako tu. Serikali yetu ipo kwa ajili ya kuwatumikia watanzania na siyo kuwaza posho.
 
Ila jamaa umesifu kuliko hata mwenezi

Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge.
 
Mpina ni chama gani? Kwanini mnakuwa na akili za kinyumbu kiasi hicho?

Juzi ulisema ujapenda kauli yake ya mwanamke
But umeona uungwaji mkono wa wanainchi wake?

That's means wao wameona hakuna kosa mbunge wao amefanya
 
Wewe endelea kutanguliza na kuwaza njaa za tumbo lako tu. Serikali yetu ipo kwa ajili ya kuwatumikia watanzania na siyo kuwaza posho.
Watanzania wapi hao unaowasemea?
 
Attachments

  • Screenshot_20250619_205609.jpg
    Screenshot_20250619_205609.jpg
    342.3 KB · Views: 15
Ila jamaa umesifu kuliko hata mwenezi

Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge.
Nimeongea ukweli na siyo kusifia
 
Back
Top Bottom