Tanzania chini ya Uongo thabiti wa Mwl.Nyerere Ilimwaga damu ya watu wake(Wanajeshi walioenda kupiga Nchi zingine? Ilitumia Rasilimali Fedha na muda Kwa Ajili ya kufundisha na kusaidia Nchi mbalimbali ambazo zilikuwa zinapambana na Wakoloni.
On top of that tulihifadhi Hadi Wakimbizi wao na kuwalisha Bure lakini juhudi zetu hizo hazijawahi kutambuliwa na kuthaminiwa vya kutosha hapa Afrika.
Baada ya miaka Mingi baadae eti Leo AU ndio Wanakumbuka kujenga Sanamu ya Mwl.Nyerere kumpa heshima ambayo alistahili miaka Mingi iliyopita.
Nelson Mandela Kwa msukumo wa Wazungu ndio anaabudiwa hapa Afrika wakati hakuna chochote Cha maana alichosaidia Afrika zaidi ya kuwasamehe Wazungu.
Nchi ambazo Tanzania imezisaidia Moja kwa Moja ni South Africa,Namibia,Angola, Mozambique, Zimbabwe, Zambia, DR Congo, Uganda, Burundi na Rwanda.
Hata Sasa tunaendelea kuzisaidoa Nchi nyingi tuu kwenye masuala mbalimbali.
View attachment 2907859View attachment 2907860View attachment 2907861
My Take
Tanzania tunastahili Zaidi na ilitakiwa hata AU HQ iwe Tanzania sio Ethiopia.
Ni vyema AU Secretariet ikafikiria kuweka Makao Makuu ya baadhi ya taasisi zake Tanznaia Ili kuenzi mchango wa Nchi yetu.
Hakuna Nchi nyingine iliyojitolea kuzidi Tanzania.