Picha: Sanamu ya Nyerere Makao Makuu Umoja wa Afrika, ni yeye au lah?

Ila nduguzangu kukunja chuma ilete uso halisi sio mchezo, nampongeza mfuaji..
 
Yeah huyu ni mwalim katika miaka ya 30 to 45 alikuwa hivi......haina ubishi tume kutengeneza sabamu hii ilihusisha fanilia....wengi watoto juzi wana taswura Nyerere akiwa above 60.....
 
Hapana,malacela
 
Hangaikeni na SANAMU, mimi sipo.

Sijui hizi sanamu ndio zinaleta UMEME au SUKARI n.k.?
 
Ile sanamu haiakisi taswira ya Mwl.J.K.Nyerere hata kwa kidogo.Sifahamu kama kulikuwa na ulazima wa kuichonga tena voluntarily ilhali hatuna msanii sahihi?
Je,Familia yake imeshirikishwa kikamilfu?Je,gharama zake zililipwa na nani kuanzia scratch hadi uzinduzi?
Tunajazwa upepo huku tukitabasamu!
 
Ni vituko vya dunia sijui familia yake mtawambia nini , na udhalilishaji huu, ccm ni shida sana
 
Aisee, afadhali leo nimeipata kujua kuna watu wana fikra kama zinazoniumiza kichwa namimi.

Nidhahiri kuwa Kuna mashujaa branded walipewa heshima kubwa kuliko walivostahili barani Africa, ilihali mashujaa halisi kama Mwl.Julius Nyerere hawakupata heshima waliostahili kutokana na mchango wao mkubwa uliotukuka barani hapa. Naheshimu juhudi za Nelson Mandela lakini Kwa mtazamo wangu, mchango wake hauwezi kulinganishwa na watu kama Nyerere. Nidhahiri mkoloni hakuondoka Africa na kisasi alilipiza Kwa kuzima nyota za wababe zake especially Julius Nyerere "Ni Shujaa Halisi"
 
Hizi ndiyo hoja za kujadili sasa na siyo perfection ya sanamu ya Nyerere.

Tatizo la Watanzania ni kwamba hakuna wanaojadili kwa nini jina la Nyerere linapata status ya sanamu, instead wamejikita kwenye trivial issues za appearance ya sculpture. Hapo ndiyo tunafeli sana.

Ningegemea watu wa flow namna Nyerere alivyojitoa kupambana na akina Ian Smith wa Rhodesia, akina Verwood na John Voster wa South Africa na King Olivera Salazar wa Portugal.

Tuna kizazi ambacho kimezoea mambo ya futuhi na udaku tu
 
Taswira ya Sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyowekwa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika
Kuna namna fulani Jamaa walikua wanaelekea kumpatia Ila nahisi kuna mpuuzi alikua anawalazimisha wawahi kumaliza ukitaka kuangalia vizuri angalia Sura Ina mapungufu madogo sana kutokea Nyerere halisi yaan madogo sana wakiongeza wino tu inakaa sawa
 
Ndugu yangu umeona kama nilivoona Mimi, mpaka nimesema Kuna namna nyota ya Nyerere inazimwa Kwa namna yoyote. Kwanini watu wasifocus na maana halisi ya heshima hiyo zaidi ni muonekano wa sanamu, real!! Young generation wengi Africa wanajua Nelson Mandela ndio Hero lakini Kuna True Hero's wamefunikwa kwasababu maalum.
 

sina tatizo sana na muonekano wa Nyerere
shida ni sanamu limetupwa vichakani nyuma ya jengo

unless unambie jengo la African Union mbele kuna pori
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…