Picha ya uso wa mtu aliekata tamaa ya kuishi baada ya kuhukumiwa miaka 22 Jela

Jomba umesema kweli asee hao watu sio kabisa. Aheri ukutanishwa na kipigo na mateso ya mjeda kuliko maliasili.

Hao jamaa ukiingia anga zao kama hawatakuua basi watakuachia ulemavu wa maisha.

Nilishakwepa mishale yao mingi sana mpaka ikabidi nihame pori. Nikikuta mahali kuna nyamapori iliyowindwa kijangili aisee sikai kabisa hapo maana wakija hapo hawajali kama ni wewe uliua au kama hujala wala nini. Wote mliokutwa lazima muisome.
 
Mkuu hiyo picha ya Chini imeleta kicheko kwenye uzi wa huzuni.
 
Hakuna bana ni sawa na useme ukamate wale wahadzabe kwa nyamapori wakati shughuli yao kuu ya kiuchumi ni uwindaji na wanakaa porini. Sheria imewakuta hao
 
kuna kitu kinaitwa sheria hufuata mkondo wake
Sheria imetoa options na mwanya mkubwa wa huruma kwa busara za hakimu kutokana na hali halisi ya mkosaji. Mfano huyo dada clearly sio jangili, na inaonekana ni masikini wa kutupa ambae alikuwa anatafutoa watoto chakula tu na sio kwamba alikuwa anafanya biashara kama biashara
 
Kwahiyo mnataka sheria zianze kufanya kazi kwa kuoneana huruma na kuangalia sura ya mtu?
 
hii ndio mana halisi ya sheria ni msimeno ndugu
 
Kwani mahakama imetoa option ya kulipa au umejitungia hukuma yako tu
 
Kwani mahakama imetoa option ya kulipa au umejitungia hukuma yako tu
naona bichwa lako gumu. nimesema, sheria inataka kuwe na option ya fine, kama fine isipotolewa, kunatakiwa kuwepo na sababu ya msingi ama la, hiyo ni sababu nzuri ya kumkatia rufaa, among others.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…