Picha ya uso wa mtu aliekata tamaa ya kuishi baada ya kuhukumiwa miaka 22 Jela

Picha ya uso wa mtu aliekata tamaa ya kuishi baada ya kuhukumiwa miaka 22 Jela

roho inakuuma kwa huyu ni sahihi, ila ni kwasababu umemwona. huko gerezani kuna wengi na wana hali mbaya kuliko huyu wamefungwa. maliasili ni wakatili sana, na ujue wengi wa watu hawa, ukiondoa wale wa pembe za ndovu, ukiona ni nyama ya kawaida tu hii jua huyo ni mtu masikini kabisa na ni mwanakijiji. wapo wengi sana gerezani na wapo huko kwasababu hawana hela ya kuweka wakili awatetee, hawana hela ya kuhonga wapelelezi na hakimu, matajiri majangili wote wapo nje. shukrani kwa Mungu huyo Tanzania imemuona ila wapo wengi sana wenye hali hiyo ya kimasikini wanaenda gerezani huko. maliasili ni wakatili,wanawapiga sana hao watu, wananyanyasa sana watu, ukitaka kujua uliza mtu yeyote anayekaa karibu na mbuga au game researve kama sisi ambao ndugu zetu ndio wapo huko, hawa watu hawana huruma , kuna maeneo wana historia za kupoteza kabisa watu kwasababu tu ya mnyamapori. maeneo ya chunya huko wana kesi kibao, maeneo ya mbingu kilombero huko, maeneo yanayozunguka ruaha ni shida.
Jomba umesema kweli asee hao watu sio kabisa. Aheri ukutanishwa na kipigo na mateso ya mjeda kuliko maliasili.

Hao jamaa ukiingia anga zao kama hawatakuua basi watakuachia ulemavu wa maisha.

Nilishakwepa mishale yao mingi sana mpaka ikabidi nihame pori. Nikikuta mahali kuna nyamapori iliyowindwa kijangili aisee sikai kabisa hapo maana wakija hapo hawajali kama ni wewe uliua au kama hujala wala nini. Wote mliokutwa lazima muisome.
 
Mkuu hiyo picha ya Chini imeleta kicheko kwenye uzi wa huzuni.
 
hiyo nyama aliyokamatwa nayo thamani yake ni 900,000, kwanini tusichangishe mchango ili tulipe faini atoke? manake kwa upande mwengine hizo sheria tumezitunga wenyewe, na yeye sio kwamba hafahamu kwamba wanyamapori ni msala. sisi tuliozaliwa maporini tunajua tangu utoto wetu nyamapori ilitungiwa hadi jina kwasababu serikali ikikukuta nayo ni msala, hivyo ukikutwa nayo hata kama una njaa ni msala kwasababu sheria inafuata mkondo, haiangalii tajiri wala masikini. cha muhimu hapo ni aidha kuifuta hiyo sheria ili tuvamie tule swala wote, au la tumchangie huyo mama alipe faini kwasababu kosa aliloshitakiwa nalo lina option ya faini, hata kama ameenda gerezani tukienda kulipa faini anatoka hata kesho.
Hakuna bana ni sawa na useme ukamate wale wahadzabe kwa nyamapori wakati shughuli yao kuu ya kiuchumi ni uwindaji na wanakaa porini. Sheria imewakuta hao
 
kuna kitu kinaitwa sheria hufuata mkondo wake
Sheria imetoa options na mwanya mkubwa wa huruma kwa busara za hakimu kutokana na hali halisi ya mkosaji. Mfano huyo dada clearly sio jangili, na inaonekana ni masikini wa kutupa ambae alikuwa anatafutoa watoto chakula tu na sio kwamba alikuwa anafanya biashara kama biashara
 
Kwahiyo mnataka sheria zianze kufanya kazi kwa kuoneana huruma na kuangalia sura ya mtu?
 
Sheria imetoa options na mwanya mkubwa wa huruma kwa busara za hakimu kutokana na hali halisi ya mkosaji. Mfano huyo dada clearly sio jangili, na inaonekana ni masikini wa kutupa ambae alikuwa anatafutoa watoto chakula tu na sio kwamba alikuwa anafanya biashara kama biashara
hii ndio mana halisi ya sheria ni msimeno ndugu
 
hiyo nyama aliyokamatwa nayo thamani yake ni 900,000, kwanini tusichangishe mchango ili tulipe faini atoke? manake kwa upande mwengine hizo sheria tumezitunga wenyewe, na yeye sio kwamba hafahamu kwamba wanyamapori ni msala. sisi tuliozaliwa maporini tunajua tangu utoto wetu nyamapori ilitungiwa hadi jina kwasababu serikali ikikukuta nayo ni msala, hivyo ukikutwa nayo hata kama una njaa ni msala kwasababu sheria inafuata mkondo, haiangalii tajiri wala masikini. cha muhimu hapo ni aidha kuifuta hiyo sheria ili tuvamie tule swala wote, au la tumchangie huyo mama alipe faini kwasababu kosa aliloshitakiwa nalo lina option ya faini, hata kama ameenda gerezani tukienda kulipa faini anatoka hata kesho.
Kwani mahakama imetoa option ya kulipa au umejitungia hukuma yako tu
 
Kwani mahakama imetoa option ya kulipa au umejitungia hukuma yako tu
naona bichwa lako gumu. nimesema, sheria inataka kuwe na option ya fine, kama fine isipotolewa, kunatakiwa kuwepo na sababu ya msingi ama la, hiyo ni sababu nzuri ya kumkatia rufaa, among others.
 
Back
Top Bottom