Picha za Ikulu, Mitandao, na Maadili: Ni nani aliyevunja kanuni?
AIBU KUU KWA TAIFA, NA TAASISI YA URAIS KUINGIZWA KTK KASHFA NZITO NA VYOMBO VYETU

Wakulaumiwa bila kupepesa macho ni

  • mnikulu
  • Kurugenzi ya mawasiliano ikulu
  • chief protocol Officer foreign,
  • Ofisi Binafsi ya Rais OBR,
  • uhamiaji,
  • Idara ya usalama wa taifa TISS
Idara hizi nyeti na maofisa wake wanapaswa kulaumiwa kwa kuruhusu mhuni kutoka Zimbabwe kuingia nchini na kumpatia miadi aonane na Rais. Waliweza kufukuza wanaharakati kutoka Kenya kuhudhuria kesi ya uhaini ya Tundu Lissu lakini wameshindwa kumfukuza mhuni wa Zimbabwe.

JamiiForums imetumika kama mbuzi wa kafara kwa makosa makubwa yaliyofanywa na watu walio karibu na taasisi ya urais kuhakikisha mkuu wao hawekwi katika mazingira ya kumpunguzia heshima .

1757188975340.jpeg

Zimbabwean businessman & socialite. Wicknell Chivayo 'biggie / bonge ' is a Zimbabwean businessman and socialite who was convicted in 2004
 
Picha na juma nature, peter wa royo tua, bashte zote zimekaa kimahaba mahaba tu, na ile anamnywesha wine raisi sjui msumbiji kuitumia glass yake.
Ummy haki aseme huyu mama chapombe wa kupindukia
Haha labda ndio maana Bashite anapeta kwenye awamu hii wenzake wote insiders wa awamu ya tano wamewekwa pembeni. Inaonekana ana mahusiano ya karibu sana na Samia.
 
AIBU KUU KWA TAIFA, NA TAASISI YA URAIS KUINGIZWA KTK KASHFA NZITO NA VYOMBO VYETU

Wakulaumiwa bila kupepesa macho ni

  • mnikulu
  • chief protocol Officer foreign,
  • Ofisi Binafsi ya Rais OBR,
  • uhamiaji,
  • Idara ya usalama wa taifa TISS
Idara hizi nyeti na maofisa wake kwa kuruhusu mhuni kutoka Zimbabwe kuingia nchini na kumpatia miadi aonane na Rais.
Tiss ndio imeoza, Na haipo kwa maslahi ya taifa.
 
Kusambaa kwa picha za Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wa kiume Ikulu kumezua gumzo kubwa mitandaoni, likizua maswali mazito kuhusu heshima ya Ofisi ya Rais na maadili ya jamii.
View attachment 3467069
Hoja ya msingi si tu uwepo wa mgeni huyo, bali zaidi namna alivyovaa na mkao wake, ambao baadhi ya wananchi wameutafsiri kama "utovu wa nidhamu" na ukosefu wa heshima kwa taasisi kuu ya nchi.
View attachment 3467073
Uchambuzi wa kina unaonesha kuwa, wakati hakuna mwongozo rasmi wa Ikulu unaoainisha mavazi ya wageni, umma ulijaza pengo hilo kwa kutumia kanuni zisizoandikwa za jamii.
View attachment 3467071
Jamii ya Kitanzania, hususan maeneo yenye utamaduni wa kihafidhina kama Zanzibar, inathamini sana uvaaji wa staha na unyenyekevu. Matarajio haya ya kijamii yakawa ndio kipimo kilichotumika kuhukumu picha hizo. Hali hii inaonyesha mgongano wa kimantiki ambapo matarajio ya umma yanakinzana na ukweli wa kutokuwepo kwa sheria rasmi za itifaki.
View attachment 3467072
Mgogoro huu uliongezeka pale serikali ilipojibu kwa kulaani usambazaji wa picha hizo, badala ya kutoa ufafanuzi kuhusu mgeni husika au muktadha wa mkutano. Ofisi ya Rais hutoa taarifa za mara kwa mara kuhusu shughuli zake na wageni rasmi, kama vile upokeaji wa mabalozi, lakini katika tukio hili kulikuwa na ukimya.
View attachment 3467073
Majibu ya serikali yalionekana kushughulikia "tatizo lisilo sahihi." Badala ya kutoa ufafanuzi juu ya maswali ya "kwa nini picha hizi zimepigwa na mgeni amevaa hivi?", serikali ilijibu, "kwa nini mnasambaza picha hizi?" Bwana Chivaro pia alipakiwa picha hizi kwenye akaunti zake za Twitter na Instagram je na yeye wamemkemea pia? Au ndio DOUBLE STANDARDS?
View attachment 3467074
Ukimya huu au majibu yasiyokidhi, katika enzi ya dijitali, huchochea uvumi na kujenga hisia kuwa kuna kitu kinafichwa, hivyo kuongeza kasi ya mjadala.
View attachment 3467071
Tukio hili linaathiri taswira ya Rais, ikionyesha mvutano kati ya uongozi wa kisasa na matarajio ya waajiri wake ambao ni watanzania.
View attachment 3467069
Picha zinazomuonesha akishirikiana kwa urahisi na wananchi, kama vile kupiga picha za kawaida, zimekuwa ni jambo la kawaida. Hata hivyo, picha hii imesababisha baadhi ya wananchi kuhoji mwelekeo wa uongozi, wakiamini kuwa heshima ya Urais inahusiana moja kwa moja na maadili ya mtu binafsi na familia.
View attachment 3467074
Serikali inatumia nguvu kuwaaminisha kuwa tatizo sio Rais kupiga picha bali ni watu waliosambaza huku Chivaro ambaye pia kazichapisha hajapokea malalamiko yoyote? DOUBLE STANDARDS KILA WAKATI.
Ndio maana Serikali inaogopa watu kuelimika, hizi picha zilikuwepo ila baada ya Elimu ya Polepole, watu tukazirudia
 
Back
Top Bottom