Picha zinatisha: Ni picha za Wamasai waliojeruhiwa na wengine damu zinavuja

Kuna video inasambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha mirindimo mikali ya risasi huko Ngorongoro huku wanananchi wa jamii ya kimasai wakikimbia huku na kule kunusuru maisha yao.

Video hiyo imezua taharuki kubwa mitandaoni kiasi kwamba wengi wa walioiona hiyo video wameshangazwa sana na nguvu kubwa inayotumika dhidi ya wananchi wa jamii ya kimasai

Ifahamike tu kuwa serikali imeonyesha nia ya kuwaondoa Wamasai katika eneo hilo la Ngorongoro kwa vigezo vya uhifadhi. Hata hivyo Wamasai wanapinga vikali suala hilo kwa kusema kuwa, Enzi za Mkoloni walikubali kuachia maeneo yao ya Serengeti ili kuwezesha Serengeti iwe mbuga ya wanyama tupu. Walihamishiwa ngorongoro kwa makubaliano kuwa safari ijayo maslahi ya binadamu yakigongana na maslahi ya watu basi maslahi ya watu yatapewa kipaumbele.
Wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya kwanza serikali ilitunga sheria ya uhifadhi ya Ngorongoro, na sheria hiyo ikasema wazi kuwa mojawapo wa malengo ya mamlaka hiyo ya uhifadhi wa ngorongoro ni kulinda maslahi ya wamasai waishio katika uhifadhi.

Tatizo la migogoro ya Serikali na Wamasai linarudi nyuma toka zama za kashfa ya Loliondo na kuna minong'ono kuwa yule mwarabu aliyepewa eneo la Loliondo anataka apewe eneo kubwa zaidi na hivyo ndo maana Wamasai wanafanyiwa visa wafukuzwe au waondoke wenyewe.

Hili suala ni zito sana, Ikumbukwe kuwa Hayati Magufuli katika utawala wake alikataa kuwafukuza wamasai huko Ngorongoro, lakini serikali hii ya awamu ya Sita naona inatumia kila mbinu kuwaondoa Wamasai katika maeneo yao.

Hapa Chini ni clip ya video ikionyesha Wamasai wakikimbia kunusuru maisha yao dhidi ya bunduki na risasi.

View attachment 2256280
Kalai la zege unatumiwa tu na wajanja wachache.
 
Wanyooshwe na washughulikiwe,wameambiwa waondoke kwa hiari kulinda hifadhi hawataki eti wanashika sime kupambana na Serikali..

Waliowajaza upepo wako kwenye keyboard walq hawajaenda front kuwasaidia.
 
Kuna video inasambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha mirindimo mikali ya risasi huko Ngorongoro huku wanananchi wa jamii ya kimasai wakikimbia huku na kule kunusuru maisha yao.

Video hiyo imezua taharuki kubwa mitandaoni kiasi kwamba wengi wa walioiona hiyo video wameshangazwa sana na nguvu kubwa inayotumika dhidi ya wananchi wa jamii ya kimasai

Ifahamike tu kuwa serikali imeonyesha nia ya kuwaondoa Wamasai katika eneo hilo la Ngorongoro kwa vigezo vya uhifadhi. Hata hivyo Wamasai wanapinga vikali suala hilo kwa kusema kuwa, Enzi za Mkoloni walikubali kuachia maeneo yao ya Serengeti ili kuwezesha Serengeti iwe mbuga ya wanyama tupu. Walihamishiwa ngorongoro kwa makubaliano kuwa safari ijayo maslahi ya binadamu yakigongana na maslahi ya watu basi maslahi ya watu yatapewa kipaumbele.
Wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya kwanza serikali ilitunga sheria ya uhifadhi ya Ngorongoro, na sheria hiyo ikasema wazi kuwa mojawapo wa malengo ya mamlaka hiyo ya uhifadhi wa ngorongoro ni kulinda maslahi ya wamasai waishio katika uhifadhi.

Tatizo la migogoro ya Serikali na Wamasai linarudi nyuma toka zama za kashfa ya Loliondo na kuna minong'ono kuwa yule mwarabu aliyepewa eneo la Loliondo anataka apewe eneo kubwa zaidi na hivyo ndo maana Wamasai wanafanyiwa visa wafukuzwe au waondoke wenyewe.

Hili suala ni zito sana, Ikumbukwe kuwa Hayati Magufuli katika utawala wake alikataa kuwafukuza wamasai huko Ngorongoro, lakini serikali hii ya awamu ya Sita naona inatumia kila mbinu kuwaondoa Wamasai katika maeneo yao.

Hapa Chini ni clip ya video ikionyesha Wamasai wakikimbia kunusuru maisha yao dhidi ya bunduki na risasi.

View attachment 2256280
Magufuli ni nani wewe MWEHU??
 
Hakuna mwenye haki na ardhi yetu zaidi ya watanzania wengine,ardhi ni mali ya Umma,acha Serikali ifanye maendeleo kupitia rasilimali zake,wamasai wasitumike kuwachonganisha na Serikali
 
Leo hii wanyama ni Bora kuliko binadamu. Kama serikali ili kubali na wakukubaliana watoke serengeti kuja ngorongoro iweje tena watake kuwapeleka handeni.

Serikali wao ndio wakaunde mbuga mpya waweke wanyama
 
[emoji24][emoji24][emoji24]Rais Samia, Rais Samia hawa ni Watanzania wana haki ya kuishi, pesa zisitufanye tusahau utu wa ndugu zetu jamani Watanzania.
 
W
Picha za kutisha [emoji23][emoji23][emoji23] nini kinatisha hapo mkuu?

Na ni kitu gani kinaonesha kuwa hizo ni picha za wamasai? (Sio wamasai peke yao wanavaa hizo bangili na kujifunika hayo mashuka). Haijulikani zimepigwa wapi, na zimepigwa lini(yawezekana zimepigwa Tanzania, Kenya, nk), sasa hiyo taharuki inatoka wapi kiurahisi namna hiyo?

Kwanini aliyepost picha hizi hakutaka kuonesha sura za wahusika? (Ingesaidia kutrace ni kina nani,wanaishi wapi, na tukio lenyewe).

Anyway, naungana nawe kwenye hilo ombi la kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kulitolea ufafanuzi ili ukweli ujulikane na kama hawa waliojeruhiwa ni wananchi wa Tanzania na wamenyanyaswa,haki itendeke. Kama hizi picha hazihusiani kwa vyovyote na usalama na uhuru wa wananchi wetu basi wanaolenga kutengeneza taharuki kupitia picha hizi wasakwe na wachukuliwe hatua.
Wazo zuri
 
Back
Top Bottom