Kuna video inasambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha mirindimo mikali ya risasi huko Ngorongoro huku wanananchi wa jamii ya kimasai wakikimbia huku na kule kunusuru maisha yao.
Video hiyo imezua taharuki kubwa mitandaoni kiasi kwamba wengi wa walioiona hiyo video wameshangazwa sana na nguvu kubwa inayotumika dhidi ya wananchi wa jamii ya kimasai
Ifahamike tu kuwa serikali imeonyesha nia ya kuwaondoa Wamasai katika eneo hilo la Ngorongoro kwa vigezo vya uhifadhi. Hata hivyo Wamasai wanapinga vikali suala hilo kwa kusema kuwa, Enzi za Mkoloni walikubali kuachia maeneo yao ya Serengeti ili kuwezesha Serengeti iwe mbuga ya wanyama tupu. Walihamishiwa ngorongoro kwa makubaliano kuwa safari ijayo maslahi ya binadamu yakigongana na maslahi ya watu basi maslahi ya watu yatapewa kipaumbele.
Wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya kwanza serikali ilitunga sheria ya uhifadhi ya Ngorongoro, na sheria hiyo ikasema wazi kuwa mojawapo wa malengo ya mamlaka hiyo ya uhifadhi wa ngorongoro ni kulinda maslahi ya wamasai waishio katika uhifadhi.
Tatizo la migogoro ya Serikali na Wamasai linarudi nyuma toka zama za kashfa ya Loliondo na kuna minong'ono kuwa yule mwarabu aliyepewa eneo la Loliondo anataka apewe eneo kubwa zaidi na hivyo ndo maana Wamasai wanafanyiwa visa wafukuzwe au waondoke wenyewe.
Hili suala ni zito sana, Ikumbukwe kuwa Hayati Magufuli katika utawala wake alikataa kuwafukuza wamasai huko Ngorongoro, lakini serikali hii ya awamu ya Sita naona inatumia kila mbinu kuwaondoa Wamasai katika maeneo yao.
Hapa Chini ni clip ya video ikionyesha Wamasai wakikimbia kunusuru maisha yao dhidi ya bunduki na risasi.
View attachment 2256280