Picha zinatisha: Ni picha za Wamasai waliojeruhiwa na wengine damu zinavuja

Picha zinatisha: Ni picha za Wamasai waliojeruhiwa na wengine damu zinavuja

Kati ya viongozi wa hovyo hii nchi ni huyo PM.
Huyu mwamba sijui anatumiwa na mamlaka au niaje aisee, hiyo ishu ya ngorongoro yeye keshamwagiwa zigo la nnya tayari na hana jinsi ya kutoka.

Ikiwa ni kweli hayo yanaendelea huko umasaini na madhara yakatokea aisee huyu PM atadhihirisha huo uhovyo wake tangu alipoudanganya umma mbele ya madhabahu kua mtu mzima kumbe kafa.

Hajui kuwa wanampeleka front kumzibia njia ya come 202530
 
#kazi iendeleeView attachment 2256641
FB_IMG_1654876840627.jpg
 
Kwahio na mtu kama huyu anaangukia kwenye category ipi ?

Mtetezi ?, Mpasha habari ? au Mchochozi ?

Kweli hii nchi inaelekea pabaya sana na tunapoenda mabaya ya JPM (propaganda na kuitana wasaliti na kuzibana midomo) nadhani ndipo tunapoelekea yaani mabaya ya kule kuchanganya na mabaya mengine ni recipe for disaster....

Ila anyway ngoja watu wafiche ugonjwa hata kama upo ili Royal Tour isiingie doa.... (kweli hili Bunge linageuka kuwa mtetea serikali na sio wananchi)
 
Napenda amani, lakini hawa wametuulia sana ndugu zetu wakulima kinyama na kishenzi kabisa kule morogoro.
 
Uoga wetu unatuponza sana, siku uoga ukitutoka hawa jama ndio watajua hawajui.
 
Wafanye haraka Mwarabu anataka Kuwinda Wanyama huko Ngorongoro!

Na Mwarabu kwa Jeuri anatengeneza Hifadhi yake Arabuni, baada ya miaka 20, Wazungu wote wataishia Arabuni kuona Wanyama...!
 
Huna macho makali boya wewe, umeangalia kwa mrengo wa kisiasa. Sasa watakula kichapo non stop, ambianeni mapema.
Unafurahia watu kuumizwa, unanufaika nini? Watu wana mashaka wakikumbuka Loliondo hadi kifo cha mwandishi habari Stan Katabalo,
Kama ulikuwa hujazaliwa hujui, hivyo usikaze sana fuvu,
Sio kila kinachofanywa na serikali ni kizuri au ni kibaya
 
Picha za kutisha [emoji23][emoji23][emoji23] nini kinatisha hapo mkuu?..

Kwanini aliyepost picha hizi hakutaka kuonesha sura za wahusika? (Ingesaidia kutrace ni kina nani,wanaishi wapi, na tukio lenyewe).

Anyway, naungana nawe kwenye hilo ombi la kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kulitolea ufafanuzi ili ukweli ujulikane na kama hawa waliojeruhiwa ni wananchi wa Tanzania na wamenyanyaswa,haki itendeke. Kama hizi picha hazihusiani kwa vyovyote na usalama na uhuru wa wananchi wetu basi wanaolenga kutengeneza taharuki kupitia picha hizi wasakwe na wachukuliwe hatua.

Nami naungana nawe kwa Aya hiyo ya mwisho. Ili ukweli usiwe na shaka la aina yoyote, uchunguzi ufanyike ambao ni rahisi kwa kuwa waliojeruhiwa (kama picha zinavyoonesha) wapo hai, watatoa ushahidi
 
Salaam Wakuu,

Kuna picha zinazoonesha Wananchi wa Tanzania Jamii ya Wamasai wakiwa na majeraha. Haijajulikana picha zimepigwa wapi saa ngapi.

Naamini Vyombo vya Usalama vitatolea ufafanuzi ili kuondoa taharuki katika Jamii.

MY TAKE:
Damu ya Mtu haiendi bure.

Pia soma:

Wamasai Ngorongoro: Spika ataka 'aliyechukua clip' ashughulikiwe, taasisi zilizosajiliwa nchini kufata

Bungeni: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa asema hakuna mgogoro kati ya Wafugaji na Serikali https://www.jamiiforums.com/threads/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-rais-magufuli-ni-mzima-na-anachapa-kazi-wanataka-atoke-atoke-aende-wapi-kariakoo-au-magomeni.1846134/
 
Kuna video inasambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha mirindimo mikali ya risasi huko Ngorongoro huku wanananchi wa jamii ya kimasai wakikimbia huku na kule kunusuru maisha yao.

Video hiyo imezua taharuki kubwa mitandaoni kiasi kwamba wengi wa walioiona hiyo video wameshangazwa sana na nguvu kubwa inayotumika dhidi ya wananchi wa jamii ya kimasai

Ifahamike tu kuwa serikali imeonyesha nia ya kuwaondoa Wamasai katika eneo hilo la Ngorongoro kwa vigezo vya uhifadhi. Hata hivyo Wamasai wanapinga vikali suala hilo kwa kusema kuwa, Enzi za Mkoloni walikubali kuachia maeneo yao ya Serengeti ili kuwezesha Serengeti iwe mbuga ya wanyama tupu. Walihamishiwa ngorongoro kwa makubaliano kuwa safari ijayo maslahi ya binadamu yakigongana na maslahi ya watu basi maslahi ya watu yatapewa kipaumbele.
Wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya kwanza serikali ilitunga sheria ya uhifadhi ya Ngorongoro, na sheria hiyo ikasema wazi kuwa mojawapo wa malengo ya mamlaka hiyo ya uhifadhi wa ngorongoro ni kulinda maslahi ya wamasai waishio katika uhifadhi.

Tatizo la migogoro ya Serikali na Wamasai linarudi nyuma toka zama za kashfa ya Loliondo na kuna minong'ono kuwa yule mwarabu aliyepewa eneo la Loliondo anataka apewe eneo kubwa zaidi na hivyo ndo maana Wamasai wanafanyiwa visa wafukuzwe au waondoke wenyewe.

Hili suala ni zito sana, Ikumbukwe kuwa Hayati Magufuli katika utawala wake alikataa kuwafukuza wamasai huko Ngorongoro, lakini serikali hii ya awamu ya Sita naona inatumia kila mbinu kuwaondoa Wamasai katika maeneo yao.

Hapa Chini ni clip ya video ikionyesha Wamasai wakikimbia kunusuru maisha yao dhidi ya bunduki na risasi.

View attachment 2256280
Serikali haiweziku bow down mara mbili kwa watu wapumbavu
 
Back
Top Bottom