Polepole: Kuna mtu alikuja kuniambia kuwa kiongozi wa awamu ya 5 atakufa

Polepole: Kuna mtu alikuja kuniambia kuwa kiongozi wa awamu ya 5 atakufa

Yani hapo ndipo mwisho wa uelewa wako?

Nakwambia hivi, hata kama anayoongea Polepole ni mambo muhimu ya taifa, na hata kama mambo muhimu ya taifa hayaishi kuongelewa kwa siku moja, Polepole angeweza kuongea mambo anayotaka kuongea on this spwcific subject katika press conference na Q&A session ya mara moja.

Kufikiri vinginevyo ni logical non sequitur.

Mambo muhimu ya taifa yataendelea kuwa discussed tu.

Ila Polepole angeweza kuweka points muhimu zote akaongea siku moja akamaliza yake akawaachia wengine.

Anadunduliza hivi habari kwa sababu anataka attention na mtaji wa kisiasa.

Ukishasikia mwanasiasa anasema ana mengi hajayatoa, wakimfanya hivi atatoa zaidi, ujue huyo hana lengo la kutoa ukweli ana lengo la kucheza mind games na kujipatia insurance policy kwenye siasa zake.

Hiyo ametunyima habari muhimu za kitaifa kwa sababu zake binafsi.
Polepole yupo kama mtu mwenye podcast ana jukwaa lake, anachagua mada, anapanga flow ya mazungumzo, na anazungumza na Watanzania anaowaona kama hadhira yake , wanaopenda kusikiliza, wanasikiliza , wasiotaka, wanaacha , kwenye podcast hakuna sharti la kusema mtu aongee mara moja amalize kila kitu...

Pia akizungumza leo, kesho atajibiwa na wanasiasa wengine kupitia vyombo vya habari ,social medias n.k ,ni kawaida kabisa yeye kurudi tena kujibu wanaompinga au kumzungumzia , hii ndiyo dynamics ya mjadala wa kisiasa, si Tanzania tu, hivyo huwezi kusema tu aite press aongee amalize, Rostam si alimjibu hapa juzi, si tumeona Polepole ametoka kumjibu... kwa hio ulitaka akae kimya kisa kazungumza siku ya kwanza na waandishi habari zote?

Kingine siasa kote duniani ni mchezo wa akili na mikakati , mind games, mwanasiasa anapanga muda, namna, na mazingira na nini azungumze ili kuimarisha ushawishi wake, kuna kosa hapo?
Kumkataza Polepole asitumie mbinu yake hio ya kuzungumza na waTanzania ni sawa na kumkataza mcheza mpira wa miguu asifanye dribbling.....
 
Hoja za kitoto hujazijibu mkuu? Huwa unakunywa pombe? Ok pombe ikiisha KICHWANI tutaendelea kwa SASA pumzika mkuu. Feel sorry kama NME kosa Mimi mkuu Asante kwa kunchallenge


Hoja zakitoto sababu mnashindwa kujibu hoja za polepole mmebaki tu kusema kwenye serikali iliyopita nayeye alikuwemo.
Hoja zakitoto sababu mnashindwa kujibu hoja za polepole mnabaki na hoja kuwa kwenye serikali iliyopita na yeye alikuwemo.
Ok, alikuwemo kama nani? Alikuwa ni Rais?
Makamu wa Rais? Waziri mkuu? Au waziri wa mambo ya ndani?.nk.....
alikuwa mkubwa kuliko Samia?
Kuliko majaliwa?
Kuliko Mpango,?
Hoja zenu zinaonesha polepole kawashika makalio hapakaliki.
 
Ukweli magurufuri aliuawa,,,na mipango ilihusisha usalama wataifa na wafanya baishara wakubwa akina taifa gas,,mkwele etc so nikweli anachosema polepole.Tusimpuuze...sbb angalia mfumo wa Vigo ukivyokuwa unakwenda,,alianza mkaba ambaye alikuwq kigingi
Ushaidi ndo hamna sasa zinabaki kua story
 
Mtu kashajouzulu ubalozi na kusema rais hafai akae kando anaogopa vigogo bado?

Kama anaogopa vigogo si angekaa kimya na ubalozi wake.
Ana avoid kuchoma madaraja yote, but i guess kwa siri ambazo ametoa nje hadi sasa its too late.
Japokuwa wanaompa bado wame ndani ya vyombo
 
Another ad hominem logical fallacy.

Hujaweza kujenga hoja kuonesha kwa nini mimi siasa za Bongo sizielewi.

Na hapa I am not necessarily talking aboit siasa za Bongo. I am talking about governance, truth, integrity.

Ila wewe guluguja ngumbaru hujui tofauti. You are like a fish in watwr, you don't know anything else.

Boya linaweza kuwa kitu muhimu sana katika kumuokoa mtu anayezama ila wewe mjinga umekaririshwa boya ni kitu kibaya.

Bloody fool.
Narudia tena, Wewe ni boya!
Kwahiyo unajiona unajua kuliko Polepole ambaye anaongea yale anayoyajua?
Polepole kaitumikia ccm kwa vyeo tofauti na mwisho kang'atuka akiwa balozi af wewe mchambisha vibabu vya kizungu uliyekimbia kwenu na hujawahi kufanya hata kazi mojawapo ya alizofanya Polepole unakuja kuharisha hapa.
Baba zenu wameharibu hii Nchi mwisho wao ndio huu.. Poleploe atazidi kuwaweka wazi huku nyie vifaranga mkibaki kulia lia.
Kila lenye mwanzo lina mwisho!
 
Polepole yupo kama mtu mwenye podcast ana jukwaa lake, anachagua mada, anapanga flow ya mazungumzo, na anazungumza na Watanzania anaowaona kama hadhira yake , wanaopenda kusikiliza, wanasikiliza , wasiotaka, wanaacha , kwenye podcast hakuna sharti la kusema mtu aongee mara moja amalize kila kitu...

Pia akizungumza leo, kesho atajibiwa na wanasiasa wengine kupitia vyombo vya habari ,social medias n.k ,ni kawaida kabisa yeye kurudi tena kujibu wanaompinga au kumzungumzia , hii ndiyo dynamics ya mjadala wa kisiasa, si Tanzania tu, hivyo huwezi kusema tu aite press aongee amalize, Rostam si alimjibu hapa juzi, si tumeona Polepole ametoka kumjibu... kwa hio ulitaka akae kimya kisa kazungumza siku ya kwanza na waandishi habari zote?

Kingine siasa kote duniani ni mchezo wa akili na mikakati , mind games, mwanasiasa anapanga muda, namna, na mazingira na nini azungumze ili kuimarisha ushawishi wake, kuna kosa hapo?
Kumkataza Polepole asitumie mbinu yake hio ya kuzungumza na waTanzania ni sawa na kumkataza mcheza mpira wa miguu asifanye dribbling.....
Bado hujaelewa hoja yangu na pengine huna uwezo wa kuelewa.

Sijasema kuna sharti lolote la Polepole kuongea mara moja.

Sijasema akizungumza leo na kesho hatajibiwa na wanasiasa wengine.

Sijasema siasa si mchezo wa akili na mikakati.

In fact nimesema sizungumzii siasa nazungumzia governance, integrity.

This is a political power struggle. Polepole is doling out information in a piecemeal fashion for political reasons.

Unapewa habari ndo ndo ndo kwa sababu za kisiasa na mtu ambaye angeweza kukupa habari zote mara moja kama angekuwa na nia ya kuweka ukweli wazi.

Hatuwezi kuelewana. Siasa ndiyo tatizo hapa, mimi najaribu kutoka kwenye siasa kwenda kwenye kupata ukweli. Wewe unanirudisha kwenye siasa.

Tupo kwenye planes mbili tofauti kabisa.

Mimi nazungumzia governance na integrity, wewe unazungumzia siasa.
 
Ana avoid kuchoma madaraja yote, but i guess kwa siri ambazo ametoa nje hadi sasa its too late.
Japokuwa wanaompa bado wame ndani ya vyombo
Kuogopa at this stage? That is a contradiction.

Si amesema ana Mungu wake wa rohoni haogopi yeye? Sasa anaogopa nini?

Kamsema wazi rais kuwa hafai kuendelea, baada ya kusema hilo anaogopa nini ?

Kuna beef gani kubwa zaidi ya kusema rais hafai akae pembeni?
 
Narudia tena, Wewe ni boya!
Kwahiyo unajiona unajua kuliko Polepole ambaye anaongea yale anayoyajua?
Polepole kaitumikia ccm kwa vyeo tofauti na mwisho kang'atuka akiwa balozi af wewe mchambisha vibabu vya kizungu uliyekimbia kwenu na hujawahi kufanya hata kazi mojawapo ya alizofanya Polepole unakuja kuharisha hapa.
Baba zenu wameharibu hii Nchi mwisho wao ndio huu.. Poleploe atazidi kuwaweka wazi huku nyie vifaranga mkibaki kulia lia.
Kila lenye mwanzo lina mwisho!
Sitakujibu, nitaorodhesha fallacies ulizoandika tu.

1.Ad hominem fallacy

2. Argument from authority fallacy

3. Logical non sequitur fallacy.

4. Logical non sequitur fallacy.

5. Strawman argument fallacy.

6. False dichotomy fallacy


Hatuo katika level moja. Hujastahili kuweza kujadiliana nami kwa sababu huwezi kujenga hoja kimantiki unarusha tuhuma kihisia.

Inaonekana una dalili za matatizo ya afya ya akili na mimi sitaki kukuzidishia matatizo yako.

Nakupeleka ignore list kuanzia hapa sitaona unachoandika.
 

JamiiForums





GE2025 Makosa ya kiuongozi aliyoyafanya Rais Samia na kujikuta anapoteza uungwaji mkono wa wananchi kwa wingi na kasi ya kutisha​



Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
1 of 5Next Last
Jump to newSubscribe
•••

Missile of the Nation​

JF-Expert Member​

Rais Samia alipoingia madarakani kwa kiwango kikubwa alipokelewa vizuri sana na watanzania. Wengi walimuona kama hewa mpya, walimuona tumaini jipya baada ya maisha ya mbilingebilinge ya utawala wa awamu ya tano. Samia alitetewa, kukingiwa kifua dhidi ya critics mbalimbali, akapewa jina la mama ili kuinua soft power yake na kumpa moral authority ya "umama". Na yeye kwa wakati huu akiwa bado hajakizoea kiti, au kuamini kuwa bado yeye ni rais aliendelea kuongea lugha za kiungwana, kujaribu kuunganisha watu, kuonyesha anataka maridhiano ya kitaifa. Akafuta kesi nyingi tu za watu, na kujitahidi kuwapa kifuta machozi walionyang'anywa fedha zao kipindi cha utawala wa rais Magufuli. Hapa ndipo watu waliposema "mama anaupiga mwingi". Sasa sijui mdudu gani akaja akatibua muenendo mzuri wa Samia na kuanza kuufanya umma unze kumgeuka. Nitaeleza baadhi ya mambo yaliyofanya watu waanze kumgeuka.

1. Operesheni ondoa wamachinga Dar es salaam
Kama mnavyofahamu mtangulizi wake yaani JPM yeye aliamua kuwekeza nguvu zake za uongozi kupata uungwaji mkono kutoka kwa watu wa chini. Kwa hiyo kuna makundi ya wananchi aliamua kuyaacha tu yafanye shughuli zao. Bila kujali uzuri au ubaya, uhalali au uharamu wa hatua hizo lakini aliamua tu kuwaacha waendeshe biashara zao mabarabarani. Na pia kama mnavyojua,Ishu ya wamachinga ni kaa la moto toka enzi za mzee Mkapa, na Kikwete. Hawa walikuwa wakifanya operesheni ndogondogo za hapa na pale kudeal na wamachinga wakizidi eneo fulani na haswa kariakoo. Sasa alipokuja Samia, labda akadhani yeye anaweza kumaliza tatizo kwa kudeal na wamachinga physically tena kwa harakaharaka badala ya kudeal na matatizo yanayosababisha umachinga uwepo. Operesheni ile ya almost Jiji zima la Dar iliumiza wamachinga sana, ikaibua hasira kwa wamachinga, na hapa ndo vile vilio vya watu kwenye video wakimkumbuka Magufuli vilipoanza kwa kasi. Mama akawa amejijengea foundation ya kuchukiwa na watu wa chini na naamini hajarecover vya kutosha tangu operesheni ile. Hili la kuwapanga wamachinga linatakiwa lofanywe lakini si kwa operesheni za maguvu wakati huna alternative ya kuwapa watu wanaotegemea msosi wao wa kila siku kwa kubangaiza.

2. Tozo
Akiwa sasa amekaa kwenye kiti, akiwa ameanza kukizoea, Samia akaja na ishu ya Tozo, wananchi wakapiga kelele sana, kelele zilikuwa nyingi sana, mwanzoni aliingilia kati kuutuliza umma, lakini baadae waziri mwenye dhamana akakomaa na tozo, wananchi wakalalamika sana, Samia akaweka pamba masikioni. Waziri wake wa fedha akasema asiyetaka tozo ahamie burundi. Samia na serikali yake hawakuishia hapo, wakaleta kodi ya jengo kwenye LUKU, yaani mpangaji wa nyumba kila akinunua umeme, eti akatwe yeye hela kumlipia mtu mwenye jengo lake. Wananchi wakalalamika Samia akapiga kimya, ila Chuki ya umma ikawa inaendelea kufukuta dhidi yake.

3. Kero za wananchi, Kukatika kwa maji hovyo na umeme hovyo
Kuanzia mwaka 2021 miezi ya mwishoni kumekuwepo na shida ya maji isiyoisha, migao isiyoeleweka, kila mwaka stori za serikali zikawa ni hizohizo mara ooh tunajenga bwawa la Kidunda, mara ooh subirini Bwawa la Nyerere likamilike. Leo bwawa la Nyerere limekamilika, umeme bado siyo wa uhakika na migao ya maji ipo kama kawaida, na wananchi mamilioni huko mikoani hawana maji safi na salama ya kutumia. Kipindi cha Magufuli siyo kwamba migao ya maji na umeme haikuwepo, ilikuwepo lakini kipindi cha Samia ilizidi hata maradufu. Wananchi wakaanza kusema kuwa mbona kipindi cha Magufuli mambo hayakuwa hivi?

4. Kesi ya Ugaidi dhidi ya Mbowe
Sasa miongoni mwa vitu vilivyofanya huyu mama achukiwe na umma ni hii kesi ya Mbowe. Umma ulitafsiri kesi ile kuwa ni ya mchongo, kwamba ni kesi ya Uongo. Watu wakaanza kusema kuwa kumbe huyu mama siyo mtenda haki na muungwana kama tulivyodhani hapo mwanzo. Hii kesi ilimuharibia Taswira huyu mama mbele ya umma kwa kiwango cha kutisha, hajawahi kurecover vizuri baada ya hapo. Kwa kweli namshangaa Mbowe ambaye baada ya kutoka Jela huku akiwa na mtaji mkubwa sana wa kisiasa alienda kuuza mtaji huo kiurahisi rahisi tu kwa Samia, wakati angejua thamani ya mtaji aliokuwa nao leo ndo angekuwa mwanasiasa maarufu na mwenye ushawishi kuliko mwanasiasa yeyote nchini. Pole zake.

5. Suala la mkataba wa Bandari
Ule mkataba ulipingwa na umma, na haukuridhiwa na umma hata kidogo. Ule mkataba siyo mzuri hata kidogo. Wananchi waliugomea katakata. Lakini Samia ili kulinda political career yake akaamua maadamu ameshaharibu basi mbwai iwe mbwai hageuki jiwe. Matokeo yake imekodishwa umma haukusikilizwa. Sasa chuki na hasira ya umma ndo anakutana nayo mitaani. Kwa maoni yangu huwezi kuwa rais wa watu, halafu watu wanakwambia hawataki mkataba huo uendelee wewe ukashupaza shingo, hawatokufarahia hata kidogo.

6. Kuanza kuminya Freedoms za watu
Sasa Samia baada ya kuona umma umeanza kuja juu, kumkosoa vikali akaja na ile strategy iliyofeli ya Madikteta ya kujaribu kufungia mitandao ili watu wasipate taarifa au wasiikosoe serikali. Kwa hiyo mtandao kama clubhouse ukafungiwa, na baadae mtandao wa twitter nao ukafungiwa, na siku hizi Polepole akiongea eti wanazima youtube na facebook. Sasa vitu vyote hivi accumulatively vinajenga chuki kubwa ya wananchi kwa serikali yake na yeye kiujumla. Kama angekubali kukosolewa na akatengeneza timu nzuri ya kujibu hoja kwa hoja kungeuwa hakuna haja ya kurudisha watu nyuma huko ambako tumeshatoka.Watu hawataki turejee tena huko.

7. Safari za nje ya nchi
Wakati huo umma unamkumbuka Magufuli ambaye alishawaaminisha kuwa safari hizi hazina tija kivile. Wakati mwingine umma unawaona wasanii kwenye madege wanalipiwa safari na serikali wakiwa wameandamana na delegetion za serikali. ukirudi huko unaanza kununua Magoli ya Simba na Yanga wakati wanaoenda kuangalia mpira mtaani kwao kuna shida ya maji ya kunywa. Hao mashabiki wanafurahia kushinda mechi zao lakini usidhani eti watakupenda kwa sababu umenunua goli. Yaani they don't associate ushindi wao na pesa ulizowapa hadi wafikie hatua wasamehe ukosefu wa huduma bora hospitali wakushangilie wewe. Sasa haya mambo yalijenga taswira mbaya kwa rais na kufanya umma usimuangalie vizuri.

8. Mambo ya utekaji na kupotea kwa watu
Hii ishu ya wananchi kutekwa na kupotezwa, huku serikali ikijivua responsibility, lakini umma siyo mjinga, wanaona wanaotkwa na kupotezwa ni wale wenye muelekeo wa kuikosoa serikali, basi wananchi wanasema fumbo mfumbie mjinga mwerevu hulin'gamua. Sasa imagine eti akatekwa katoto kadogo kama Deusdedith Soka, anatekwa mtu kama Mdude Nyagali, Akina Mbise, bila kusahau listi ya watu kibao waliotekwa toka mwaka 2021, serikali ipo haichukui hatua madhubuti, hii inawafanya watu waconclude. Umma ukasababisha umchukie Samia mno tena mno. Yeyote aliyempa strategy ya kutawala kwa hofu, akiamini kuwa kwa kufanya hivyo labda watu watamuogopa kama walivyomuogopa Magufuli alimuharibia uungwaji mkono wa kisiasa mbele ya umma kwa kiwango kisicho na mfano. Tena kilichochagiza hali hii ni tukio la kuumizwa kwa Father Kitima na namna alivyodeal na Ishu ya Askofu Gwajima. Damage kwa namna walivyodeal na hizi issues ilikuwa damaging sana.

9. Kesi ya Lissu na Kutumia Mahakama kisiasa
Siku hizi Samia na Serikali yake wakishindwa kujibu hoja za wananchi, au wakipata kibano kikali cha kisiasa, badala ya kujibu hoja, au kufanya siasa basi mahakama inatumika kuwatoa kwenye kitanzi. Mahakama sasa imegeuka kama jumuia ndani ya Jumuia za CCM. Haitendi haki hata kidogo. Na ushahidi wa kwamba haitendi haki ni kuwa hatuoni haki ikitendeka katika maamuzi yake. Akina Mwabukusi, Dr Slaa na Mdude walivyokuwa wakitetea bandari wakapigwa kesi ya uhaini. Leo tunaona Lissu naye kapigwa kesi ya Uhaini. Lakini kila mwenye macho anaona wazi kuwa hamna kitu hapa ni mchongo mchongo tu. Kwamba tumekushindwa jukwaani ngoja tudeal na wewe kwenye kizimba!. Kwamba tumeishindwa CDM huko mitaani sasa tuwazuie kupitia kesi za mchongo. Haya mambo yanajenga chuki kali kwa umma, yanamfanya Samia aonekane ni dhaifu mno kiuongozi na yanamharibia taswira yake ndani na nje.
Mwanzoni nilizungumzia jinsi kesi ya Mbowe ilivyomharibia Samia heshima. Hii ya Lissu sasa ndo funga kazi, watu wanaona kesi yake inavyoendeshwa, wanaona waziwazi abuse ya power, chuki haiendi kwa mahakimu, chuki inarudi kwa yule aliyeifungua. yaani hii kesi imemharibia heshima Samia FIVE TIMES kuliko hata ile ya Mbowe.

10. Uteuzi wake wa kugombea urais ulivyofanyika na mbeleko ya kisiasa
Samia amepanda ngazi nyingi za uongozi kwa kushikwa mkono na wala si kwa kupambana nginjanginja, alishikwa mkono na maraisi waliopita, wakampa nafasi hizi na zile, mwaka 2015 akapewa nafasi ya umakamu wa Magufuli kingekewa tu kwa sababu wazee walisema awekwe yeye, hakuwa mwanasiasa prominent nchini, Mwaka 2021 akaukwaa urais baada ya kifo cha JPM, Sasa safari hii watu walitegemea apate urais kwa kusimama ndani ya taratibu, kanuni na katiba ya chama lakini mentality ileile ya "Kamlete", "mbeleko" ikatumika. Sasa hii inaibua chuki ndani ya CCM na hata nje ya CCM wanapoona mbona mtu anataka uarais sana hadi kufikia hatua za kanuni na taratibu za chama zinavunjwa?, hii nguvu yote ya kukwepa ushindani ya nini?

Kiufupi hayo ni baadhi ya mambo ninayoyaona yamepelekea Samia kuchukiwa na kukosa ushawishi wa umma kwa kiwango kikubwa sana.

Thanks Quote Reply
Report
  • Thanks
  • Nzuri
  • Dislike
Reactions:Nkuba25, Al Zagawi, Milindi and 41 others
[IMG alt="MrKanteChelsea"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/551/551161.jpg?1636059183[/IMG]

MrKanteChelsea​

JF-Expert Member​

So sad

Thanks Quote Reply
Report
  • Thanks
Reactions:Harmful and Bila bila
[IMG alt="Mshana Jr"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/98/98741.jpg?1538933508[/IMG]

Mshana Jr​

Platinum Member​

Rais Samia alipoingia madarakani kwa kiwango kikubwa alipokelewa vizuri sana na watanzania. Wengi walimuona kama hewa mpya, walimuona tumaini jipya baada ya maisha ya mbilingebilinge ya utawala wa awamu ya tano. Samia alitetewa, kukingiwa kifua dhidi ya critics mbalimbali, akapewa jina la mama ili kuinua soft power na kumpa moral authority ya "umama". Na yeye kwa wakati huu akiwa bado hajakizoea kiti, au kuamini kuwa bado yeye ni rais aliendelea kuongea lugha za kiungwana, kujaribu kuunganisha watu, kuonyesha anataka maridhiano ya kitaifa. Akafuta kesi nyingi tu za watu, na kujitahidi kuwafuta kifuta jacho walionyang'anywa fedha zao kipindi cha utawala wa rais Magufuli. Hapa ndipo watu waliposema "mama anaupiga mwingi". Sasa sijui mdudu gani akaja akatibu muenendo mzuri wa Samia na kuanza kuufanya umma unze kumgeuka. Nitaeleza baadhi ya mambo yaliyofanya watu waanze kumgeuka.

1. Operesheni ondoa wamachinga Dar es salaam
Kama mnavyofahamu mtangulizi wake yaani JPM yeye aliamua kuwekeza nguvu zake za uongozi kupata uungwaji kutoka watu wa chini. Kwa hiyo kuna makundi ya wananchi aliamua kuyaacha tu yafanye shughuli zao. Bila kujali uzuri au ubaya, uhalali au uharamu wa hatua hizo lakini aliamua tu kuwaacha yaendeshe biashara zao mabarabarani. Kama mnavyojua,Ishu ya wamachinga ni kaa la moto toka enzi za mzee Mkapa, na Kikwete. Hawa walikuwa wakifanya oeresheni ndogondogo za hapa na pale kudeal na wamachinga wakizidi eneo fulani na haswa kariakoo. Sasa alipokuja Samia, labda akadhani yeye anaweza kumaliza tatizo kwa kudeal na wamachinga physically badala ya kudeal na matatizo yanayosababisha umachinga uwepo. Operesheni ile ya almost Jiji zima la Dar iliumiza wamachinga sana, ikaibua hasira kwa wamachinga, na hapa ndo vile vilio vya watu kwenye video wakimkumbuka Magufuli vilipoanza kwa kasi. Mama akawa amejijengea foundation ya kuchukiwa na watu wa chini na naamini hajarecover vya kutosha tangu operesheni ile. Hili la kuwapanga wamachinga linatakiwa lofanywe lakini si kwa opersheni za Maguvu wakati huna alternative ya kuwapa watu wanaotegemea msosi wao wa kila siku kwa kubangaiza.

2. Tozo
Akiwa sasa amekaa kwenye kiti, akiwa ameanza kukizoea, Samia akaja na ishu yake ya Tozo, wananchi wakapiga kelele sana, kelele zilikuwa nyingi sana, mwanzoni aliingilia kati kuutuliza umma, lakini baadae waziri mwenye dhamana akakomaa na tozo, wananchi wakalalamika sana, Samia akaweka pamba masikioni. Waziri wake wa fedha akasema asiyetaka fedha ahamie burundi. Samia na serikali yake hawakuishia hapo, wakaleta kodi ya jengo kwenye LUKU, yaani mpangaji wa nyumba kila akinunua umeme, eti akatwe yeye hela kumlipia mtu mwenye jengo lake. Wananchi wakalalamika Samia akapiga kimya, ila Chuki ya umma ikawa inaendelea kufukuta dhidi yake.

3. Kero za wananchi, Kukatika kwa maji hovyo na umeme hovyo
Kuanzia mwaka 2021 miezi ya mwishoni kumekuwepo na shida ya maji isiyoisha, migao isiyoeleweka, kila mwaka stori za serikali zikawa ni hizohizo mara ooh tunajenga bwawa la Kinunda, mara ooh subirini Bwawa la Nyerere likamilike. Leo bwawa la Nyerere limekamilika, umeme bado siyo wa uhakika na migao ya maji ipo kama kawaida, na wananchi mamilioni huko mikoani hawana maji safi na salama ya kutumia. Kipindi cha Magufuli siyo kwama migao ya maji na umeme haikuwepo, ilikuwepo lakini kipindi cha Samia ilizidi hata maradufu. Wananchi wakaanza kusema kuwa mbona kipindi cha Magufuli mambo hayakuwa hivi?

4. Kesi ya Ugaidi dhidi ya Mbowe
Sasa miongoni mwa vitu vilivyofanya huyu mama achukiwe na umma ni hii kesi ya Mbowe. Umma ulitafsiri kesi ile kuwa ni ya mchongo, kwamba ni kesi ya Uongo. Watu wakaanza kusema kuwa kumbe huyu mama siyo mtenda haki na muungwana kama tulivyodhani hapo mwanzo. Hii kesi ilimuharibia Taswira huyu mama mbele ya umma kwa kiwango cha kutisha, hajawahi kurecover vizuri baada ya hapo. Kwa kweli namshangaa Mbowe ambaye baada ya kutoka Jela huku akiwa na mtaji mkubwa sana wa kisiasa alienda kuuza mtaji huo kiurahisi rahisi tu kwa Samia, wakati angejua thamani ya mtaji aliokuwa nao leo ndo angekuwa mwanasiasa maarufu na mwenye ushawishi kuliko mwanasiasa yeyote nchini. Pole zake.

5. Suala la mkataba wa Bandari
Ule mkataba ulipingwa na umma, na haukuridhiwa na umma hata kidogo. Ule mkataba siyo mzuri hata kidogo. Ni mkataba wa kuuza sovereignity na assets zetu muhimu kwa Taifa kwa nchi ya kigeni ya UAE. Wananchi waliugomea katakata. Lakini Samia ili kulinda political career yake akaamua maadamu ameshaharibu basi mbwai iwe mbwai hageuki jiwe. Matokeo yake bandari imekwenda, umma haukusikilizwa. Sasa chuki na hasira ya umma ndo anakutana nayo mitaani. Kwa maoni yangu huwezi kuwa rais wa watu, halafu watu wanakwambia hawataki mkataba huo uendelee wewe ukashupaza shingo, hawatokufarahia hata kidogo.

6. Kuanza kuminya Freedoms za watu
Sasa Samia baada ya kuona umma umeanza kuja juu, kumkosoa vikali akaja na ile strategy iliyofeli ya Madikteta ya kujaribu kufungia mitandao ili watu wasipate taarifa au wasiikosoe serikali. Kwa hiyo mtandao kama clubhouse ukafungiwa, na baadae mtandao wa twitter nao ukafungiwa, na siku hizi Polepole akiongea eti wanazima youtube na facebook. Sasa vitu vyote hivi accumulatively vinajenga chuki kubwa ya wananchi kwa serikali yake na yeye kiujumla. Kama angekubali kukosolewa na akatengeneza timu nzuri ya kujibu hoja kwa hoja kungeuwa hakuna haja ya kurudisha nyuma huko ambako watu walikuwa wanataka tusirejee tena.

7. Safari zisizoisha na matumizi holela ya fedha za umma
Wewe kila siku uko angani mara ulaya, marekani, Asia, Uarabuni. Wakati huo umma unamkumbuka Magufuli ambaye alishawaaminisha kuwa safari hizi hazina tija kivile. Wakati mwingine umma unawaona wasanii kwenye madege wanalipiwa safari na serikali wakiwa wameandamana na delegetion za serikali. ukirudi huko unaanza kununua Magoli ya Simba na Yanga wakati wanaoenda kuangalia mpira mtaani kwao kuna shida ya maji ya kunywa. Hao mashabiki wanafurahia kushinda mechi zao lakini usidhani eti watakupenda kwa sababu umenunua goli. Yaani they don't associate ushindi wao na pesa ulizowapa hadi wafikie hatua wasamehe ukosefu wa huduma bora hospitali wakushangilie wewe. Sasa haya mambo yalijenga taswira mbaya kwa rais na kufanya umma usimuangalie vizuri.

8. Mambo ya utekaji na kupoteza watu
Hii ishu ya wananchi kutekwa na kupotezwa, huku serikali ikijivua responsibility, lakini umma siyo mjinga, wanaona wanaotkwa na kupotezwa ni wale wenye muelekeo wa kuikosoa serikali, basi wananchi wanasema fumbo mfumbie mjinga mwerevu hulin'gamua. Sasa imagine eti wanakateka katoto kadogo kama Deusdedith Soka, Unamteka mtu kama Mdude Nyagali, Akina Mbise, bila kusahau listi ya watu kibao waliotekwa toka mwaka 2021, serikali ipo haichukui hatua madhubuti, hii ikawafanya watu waconclude kuwa hii ni "INSIDE JOB". Umma ukasababisha umchukie Samia mno tena mno. Yeyote aliyempa strategy ya kutawala kwa hofu, akiamini kuwa kwa kufanya hivyo labda watu watamuogopa kama walivyomuogopa Magufuli alimuharibia uungwaji mono wa kisiasa mbele ya umma kwa kiwango kisicho na mfano. Tena kilichochagiza hali hii ni tukio la kuumizwa kwa Father Kitima na namna alivyodeal na Ishu ya Askofu Gwajima. Damage kwa namna walivyodeal na hizi issues ilikuwa damaging sana.

9. Kesi ya Lissu na Kutumia Mahakama kisiasa
Siku hizi wakishindwa kujibu hoja za wananchi, au wakipata kibano kikali cha kisiasa, badala ya kujibu hoja, au kufanya siasa sasa mahakama inatumika kuwatoa kwenye kitanzi. Mahakama sasa imegeuka kama jumuia ndani ya Jumuia za CCM. Haitendi haki hata kidogo. Na ushahidi wa kwamba haitendi haki ni kuwa hatuoni haki ikitendeka katika maamuzi yake. Akina Mwabukusi, Dr Slaa na Mdude walivyokuwa wakitetea bandari wakapigwa kesi ya uhaini. Leo tunaona Lissu naye kapigwa kesi ya Uhaini. Lakini kila mwenye macho anaona wazi kuwa hamna kitu hapa ni mchongo mchongo tu. Kwamba tumekushindwa jukwaani ngoja tudeal na wewe kwenye kizimba!. Kwamba tumeishindwa CDM huko mitaani sasa tuwazuie kupitia kesi za mchongo. Haya mambo yanajenga chuki kali kwa umma, yanamfanya Samia aonekane ni dhaifu mno kiuongozi na yanamharibia taswira yake ndani na nje.
Mwanzoni nilizungumzia jinsi kesi ya Mbowe ilivyomharibia Samia heshima. Hii ya Lissu sasa ndo funga kazi, watu wanaona kesi yake inavyoendeshwa, wanaona waziwazi abuse ya power, chuki haiendi kwa mahakimu, chuki inarudi kwa yule aliyeifungua. yaani hii kesi imemharibia heshima Samia FIVE TIMES kuliko hata ile ya Mbowe.

10. Uteuzi wake wa kugombea urais ulivyofanyika na mbeleko ya kisiasa
Samia amepanda ngazi nyingi za uongozi kwa kushikwa mkono na wala si kwa kupambana nginjanginja, alishikwa mkono na maraisi waliopita, wakampa nafasi hizi na zile, mwaka 2015 akapewa nafasi ya umakamu wa Magufuli kingekewa tu kwa sababu wazee walisema awekwe yeye, hakuwa mwanasiasa prominent nchini, Mwaka 2021 akaukwaa urais baada ya kifo cha JPM, Sasa safari hii watu walitegemea apate urais kwa kusimama ndani ya taratibu, kanuni na katiba ya chama lakini mentality ileile ya "Kamlete", "mbeleko" ikatumika. Sasa hii inaibua chuki ndani ya CCM na hata nje ya CCM wanapoona mbona mtu anataka uarais sana hadi kufikia hatua za kanuni na taratibu za chama zinavunjwa?, hii nguvu yote ya kukwepa ushindani ya nini?

Kiufupi hayo i baadhi ya mambo ninayoyaona yamepelekea Samia kuchukiwa na kukosa ushahwishi wa umma kwa kiwango kikubwa sana.
Click to expand...
Kiufupi hayo i baadhi ya mambo ninayoyaona yamepelekea Samia kuchukiwa na kukosa ushahwishi wa umma kwa kiwango kikubwa sana.

Thanks Quote Reply
Report
  • Thanks
Reactions:allypipi, inchaji, Harmful and 9 others

Missile of the Nation​

JF-Expert Member​

Kiufupi hayo i baadhi ya mambo ninayoyaona yamepelekea Samia kuchukiwa na kukosa ushahwishi wa umma kwa kiwango kikubwa sana.
Kabisa

Thanks Quote Reply
Report
  • Thanks
Reactions:Harmful, Doji MD, stonecutter and 1 other person
[IMG alt="Bukirilo"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/765/765801.jpg?1736879520[/IMG]

Bukirilo​

JF-Expert Member​

Kauli zake zisizo na staha ... (1)kifo ni kifo tu (2) katiba si ni kijitabu tu . (3) ku deal na wanaomkosoa (4) utekaji kupotea na mauaji kwa Raia .

Thanks Quote Reply
Report
  • Thanks
Reactions:jimama26, allypipi, inchaji and 11 others
[IMG alt="Kimbesa11"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/323/323977.jpg?1661233541[/IMG]

Kimbesa11​

JF-Expert Member​

Samia anaungwa mkono na Watanzania wote kwasabu
1. Amepandisha madaraja na kuongeza mishahara Watumishi ambao walikaa miaka 7 bila daraja Wala nyongeza
2. Aliondoa VRF ya HESLB
3. AMEONGEZA AJIRA, Samia anaajir tuwe wakweli
4. Ameweka mifumo ya kiutumishi ambayo imeondoa urasmu kwenye kuhama na manunuzi
5. Samia amejenga kituo Cha afya kila kata
6. Samia ameweka mazingira mazuri ya biashara hakuna biashara inayofungwa Hadi Sasa.

OCTOBER TUNATIKI ✅✅
 
Kuogopa at this stage? That is a contradiction.

Si amesema ana Mungu wake wa rohoni haogopi yeye? Sasa anaogopa nini?

Kamsema wazi rais kuwa hafai kuendelea, baada ya kusema hilo anaogopa nini ?

Kuna beef gani kubwa zaidi ya kusema rais hafai akae pembeni?
You are right, ingekuwa USA asingeguswa ila hapa kwa mila za hi nchi kusema mkubwa hafai = to jinai( japokuwa kisheria hana kosa)

Ila kurudi kwenye point , sikiliza maongeze yake, anasema haogopi , means amejipanga but with wayy out, even speach zake kuna mambo hataki kuingia ndani kusema
 
Sisi tunamshkuru sana Mh Polepole kwa kujitoa kiasi hiki kwa Watanzania walio wengi. Historia itamkumbuka kwa kusimama upande wa haki. Watanzania walio wengi tumemuelewa na kumpenda sana.
 
Hoja zakitoto sababu mnashindwa kujibu hoja za polepole mnabaki na hoja kuwa kwenye serikali iliyopita na yeye alikuwemo.
Ok, alikuwemo kama nani? Alikuwa ni Rais?
Makamu wa Rais? Waziri mkuu? Au waziri wa mambo ya ndani?.nk.....
alikuwa mkubwa kuliko Samia?
Kuliko majaliwa?
Kuliko Mpango,?
Hoja zenu zinaonesha polepole kawashika makalio hapakaliki.
Mange kimambi ALIPO SEMA na anayoyasema kuhuso FEDHA nk JE nayeye ni rais, makamu,waziri?

Kwishaaaa
 
You are right, ingekuwa USA asingeguswa ila hapa kwa mila za hi nchi kusema mkubwa hafai = to jinai( japokuwa kisheria hana kosa)

Ila kurudi kwenye point , sikiliza maongeze yake, anasema haogopi , means amejipanga but with wayy out, even speach zake kuna mambo hataki kuingia ndani kusema
Kwa hivyo anavyosema yeye haogopi analindwa na Mungu wake wa rohoni ni muongo anatudanganya au ni mjinga anaji contradict tu?
 
Back
Top Bottom