Polepole: Kuna mtu alikuja kuniambia kuwa kiongozi wa awamu ya 5 atakufa

Polepole: Kuna mtu alikuja kuniambia kuwa kiongozi wa awamu ya 5 atakufa

Leo kwenye muendelezo wa mawasilisho yake huko mitandaoni Ndugu Humphrey Polepole amesema kuwa wakati wanakaribia uchaguzi mkuu 2020 kwenye kazi yake ya kusikiliza wananchi kuna bwana mmoja alimfuata akamwambia kuwa kuna watu wanapanga kumuua Rais wa wakati huo!

Anasema alipeleka ujumbe huo kwa muheshimiwa Rais, ambae pamoja na mengine alimwambia kuwa habari hizo akamwelezee msaidizi wake fulani ambae Ndugu Polepole hajamtaja.

Anasema pia palikuwepo dereva Taxi aliyekuwa akipewa bahasha na watu fulani aipeleke sehemu fulani. Siku moja dereva huyo alipewa bahasha ikiwa wazi/haijafungwa hivyo dereva alipata shauku ya kutaka kuona ni nini ambacho amekua akibebeshwa kwenye bahasha siku zote hizo. Ndipo alipofungua bahasha hiyo na kukuta list ya majina mengi ya watu/viongozi yakiwa yameandikwa kwa pamoja na codes zisizoeleweka, Anasema lilikuwemo jina la Rais wa awamu ya 5 na hata la kwake pia Polepole lilikuwepo!

Mwisho, Ndugu Polepole amemwambia muheshimiwa Rais wa sasa kuwa asiende kuchukua fomu kesho kwani kufanya hivyo itakuwa ni kuwatukana watanzania wote wanaoona mbali kuliko anavyoona yeye na hao waliomzunguka wanaomshinikiza kuchukua fomu na kuwania uRais.

Nimetafakari sana, wacha tuone!​
What comes around,goes around.

Nadhani na Mama wanamtandao watamfanyia hivyo hivyo.Akishaapishwa tu,wanamuondoa na Makamu wake ambaye ni Mwenzao atanachukua kiti kama ilivyokuwa yeye.
 
Rais ndiye Kiongozi No 1 katika Taifa lolote lile. Kwetu hapa anapatikana kupitia Uchaguzi. Anachaguliwa na kuwekwa madarakani na wananchi wa nchi hii.
Kwa vyovyote vile Kiongozi wa nchi anatakiwa kulindwa dhidi ya maadui wa ndani na nje ili kuhakikisha kuwa yuko salama na anatekeleza majukumu ya kuwatumia wananchi bila mawaa yote.

Kauli ya Polepole binafsi imenishtua na kunisikitisha zaidi ya sana. Kama kulikuwa na taarifa za kuuawa kwa JPM na vyombo vinavyomlinda vikajulishwa, lakini bado mpango ukaendelea na ukafanikiwa, basi itoshe kabisa kuhitimisha kwa kusema kuwa, wapo watu walio juu ya Rais ambao wao wakiamua hili liwe, linakuwa. Na kama Taifa tunawajibika kutafakari kwa kina zaidi bila kuangalia huyu ni CCM yule ni CHADEMA nk. Vyombo vyetu vitumike kwa maslahi ya Taifa na watu wake na si kwa mtu binafsi hata kama ndiye kawaweka walipo Sasa.
 
Polepole sasa anaanza mzaha. Bahasha ya siri kama hiyo iende wazi na apewe tax driver kweli?​
hata mimi niliposikiliza niliona mbona kama hii kitu imeongezwa chumvi? Afadhali hata angesema ameifungua kiujanja ujanja ningeamini, lakini siyo kupewa ikiwa wazi.
 
Huyu jamaa ipo siku atakuja kuongea vitu ambavyo watawala hawapendi wananchi wavijue

Maana kilasiku anakuja na jambo jipya.
Then akishafanya hivyo nini kwani kitabadilika ?
Wananchi hata wakijua hicho walikuwa hawakijui wataweza kufanya nini ??! 🤣🤣😅
Najaribu kujiuliza tu Mimi mwenyewe kwa sauti 🤣🤷🏿‍♂️⁉️
Ndugu Polepole kwa Kweli bado nashindwa kumuelewa nini hasa anafikiria 😅🤷🏿‍♂️!
 
What comes around,goes around.

Nadhani na Mama wanamtandao watamfanyia hivyo hivyo.Akishaapishwa tu,wanamuondoa na Makamu wake ambaye ni Mwenzao atanachukua kiti kama ilivyokuwa yeye.
Makamu wake alikua team Nywele nyeupe kawekwa pale kutuliza ali ya hewa ingekua mbaya zaidi huyo Makamu asingekuepo hapo ageungana na Polepole maana bado team nywele nyeupe hipo ina nguvu kwa kiasi flani
 
Kifo cha magufuli kina utata sana maana Mwishoni kwenye kampeni mwili wake ulikua umenyongonyea sana sasa sijui peace maker na mwili umenyongonyea vitu viwilli tofauti lakini Kwanini polepole alikua kimya mpaka mda huu wa Uchaguzi?
Kweli John pamoja na kuwa na backup kubwa ya wafuasi.kipindi Cha campaign alionekana umenyong'onyea kiafya
 
Back
Top Bottom