Polepole: Kuna mtu alikuja kuniambia kuwa kiongozi wa awamu ya 5 atakufa

Polepole: Kuna mtu alikuja kuniambia kuwa kiongozi wa awamu ya 5 atakufa

Polepole kama Polepole anayoyaongea Watawala watakuwa wanajua kama anaongea ukweli au anaongopa. Kinachoniogopesha mimi ni Logic ya lawaida tu kwamba Polepole hay hayuko peke yake.

Je NYUMA YAKE YUPO NANI? Maana hii no vita ya madaraka ndani ya CCM pole kaigeuza ni vita ya kurejesha chama na serikali kwenye misingi, but it is simply ni vita ya makundi ndani ya CCM tena makundi ya tangu 1995.
 
hata muuaji huwa anajisahau, unaweza kuua na kuweka code hujulikani ila kuna siku Mungu akiamua kukuumbua, utakamatwa, mazoea yatakujaa na utajichanganya tu. hiyo mbona kawaida.
Muuaji wa kibaka ndio anaweza sahau, mtu yeyote anayepanga mipango mirefu ya kuuwa watu ngazi ya juu kwa nyakati tofauti na kwa njia tofauti akiwemo kumuua Rais usidhani ni muuza gongo au ana akili za kupikia andazi.

Hakuna kujisahau kwa kutuma barua iliyofunguliwa kwa dereva tax. Na hakuna mantiki kuandika list ya majina na kutumiana. Hata wauaji wa mwenyekiti wa kitongoji si wajinga kiasi hiki.
 
And you genuinely believe Polepole has a shot at winning exactly what? Unseating Samia from the presidency?
I don’t believe that Polepole, as an "individual", holds the power, but rather Polepole as a "system". I’ll give it time, the odds aren’t zero. Samia may remain in the presidency, but the legacy of her leadership could turn out to be more catastrophic than that of any other president in Tanzanian history.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Sasa atafanyaje kama chadema wanaamini na wanafurahia na wanapata Imani kabisa kuwa kupitia 'stori ya kipumbavu' kama hiyo itamfikisha lissu ikulu?!!! Acha ajikusanyie viewers za mizembe hii kutoka chadema.
Inasemekana wiki ijayo atawataja waliomuua Jiwe
 
Polepole ameanza kuniprove wrong. Inshort NAANZA kumpuuzia anaweza kua Yuko wright ila ana ongeza chumvi. Alafu anapanga tukio kubwa unasubiri ila akifanya halifanyi kwa ukubwa ulio kusudiwa SIKU HIZI hata simfatilii



Kwishaaaa
Kwani wewe una impact gani? Ukipuuza wewe wako maelfu wanaomfuata
 
Muuaji wa kibaka ndio anaweza sahau, mtu yeyote anayepanga mipango mirefu ya kuuwa watu ngazi ya juu kwa nyakati tofauti na kwa njia tofauti akiwemo kumuua Rais usidhani ni muuza gongo au ana akili za kupikia andazi.

Hakuna kujisahau kwa kutuma barua iliyofunguliwa kwa dereva tax. Na hakuna mantiki kuandika list ya majina na kutumiana. Hata wauaji wa mwenyekiti wa kitongoji si wajinga kiasi hiki.
Waliamua kuach alama tu.
 
Binafsi ninaamini yote anayosema pole pole maana haihiitaji PhD kuweza kuona uhalisia wa mambo yanayoonekana sasa na yaliyopita na anayozungumza.

It doesn’t take a genius to understand him, kama upinzani wanaona mbali, basi huu ndo muda mzuri kuungana na kupaza sauti kupitia taarifa anazotoa PolePole, mpasuko ukizidi kutokea kwenye CCM na watanzania kupitia hizi ajenda anazotoa Polepole basi upinzani unapita kati kati yao maana watapata support ya kuhusu katiba na reforms za uchaguzi maana wahuni watakuwa wamezidiwa nguvu, njia hii inaitwa “Divide and Rule”.

Huu sio muda wa kumbeza Polepole bali ni kuungana naye, atakayeitoa CCM ni mwana CCM, huu ndo muda wenu upinzani, CCM is more weaker than before, na polepole anawasaidia kwa kuutoa ukwel, sukumeni ukwel anaosema, tupeni madongo kuhusu huu mtandao wa wahuni, hojini kuhusu kifo cha JPM ili kuwatia hasira baadhi ya wanaccm waliompenda. Mbona upinzani mnaacha fursa nzuri hii ya kuleta ukombozi wa kweli TZ.
 
Leo kwenye muendelezo wa mawasilisho yake huko mitandaoni Ndugu Humphrey Polepole amesema kuwa wakati wanakaribia uchaguzi mkuu 2020 kwenye kazi yake ya kusikiliza wananchi kuna bwana mmoja alimfuata akamwambia kuwa kuna watu wanapanga kumuua Rais wa wakati huo!

Anasema alipeleka ujumbe huo kwa muheshimiwa Rais, ambae pamoja na mengine alimwambia kuwa habari hizo akamwelezee msaidizi wake fulani ambae Ndugu Polepole hajamtaja.

Anasema pia palikuwepo dereva Taxi aliyekuwa akipewa bahasha na watu fulani aipeleke sehemu fulani. Siku moja dereva huyo alipewa bahasha ikiwa wazi/haijafungwa hivyo dereva alipata shauku ya kutaka kuona ni nini ambacho amekua akibebeshwa kwenye bahasha siku zote hizo. Ndipo alipofungua bahasha hiyo na kukuta list ya majina mengi ya watu/viongozi yakiwa yameandikwa kwa pamoja na codes zisizoeleweka, Anasema lilikuwemo jina la Rais wa awamu ya 5 na hata la kwake pia Polepole lilikuwepo!

Mwisho, Ndugu Polepole amemwambia muheshimiwa Rais wa sasa kuwa asiende kuchukua fomu kesho kwani kufanya hivyo itakuwa ni kuwatukana watanzania wote wanaoona mbali kuliko anavyoona yeye na hao waliomzunguka wanaomshinikiza kuchukua fomu na kuwania uRais.

Nimetafakari sana, wacha tuone!​
View attachment 3436166
Polepole ni project ya samia na ccm ili kumpoteza lisu masikioni mwa watanganyika
 
Hapana mkuu Kuna vitu ukimtengenezea MTU taswira Fulani alafu aone tofauti inashusha shauku na maswali kibao. Tangu magufuli kafariki ni Miaka mingapi? NDO hayo yasemwe Leo mkuu tena KWENYE uchaguzi? JE haziwezi kuwa fitna za chaguzi?



Kwishaaaa
Kasema kwa sababu ya kilichotokea pale Dodoma, kupitisha mgombea kienyeji, lakini isingekuwa hivyo nadhani angeendelea na ubalozi wake..
 
Hawezi kumwaga kila kitu kwa sababu nia yake si kusema ukweli.

Angekuwa na nia ya kusema ukweli angesema yote.

Nia yake ni kujipatia popularity, influence na power.

Hivyo anatoa kidogo kidogo kwa hesabu za kujipanga apate popularity, influenxe na power.
Kuongea yote kwa siku moja hawezi, ina maana aongee siku tatu bila kula wala kunywa?
 
Back
Top Bottom