Polepole: Kuna mtu alikuja kuniambia kuwa kiongozi wa awamu ya 5 atakufa

Polepole: Kuna mtu alikuja kuniambia kuwa kiongozi wa awamu ya 5 atakufa

Leo kwenye muendelezo wa mawasilisho yake huko mitandaoni Ndugu Humphrey Polepole amesema kuwa wakati wanakaribia uchaguzi mkuu 2020 kwenye kazi yake ya kusikiliza wananchi kuna bwana mmoja alimfuata akamwambia kuwa kuna watu wanapanga kumuua Rais wa wakati huo!

Anasema alipeleka ujumbe huo kwa muheshimiwa Rais, ambae pamoja na mengine alimwambia kuwa habari hizo akamwelezee msaidizi wake fulani ambae Ndugu Polepole hajamtaja.

Anasema pia palikuwepo dereva Taxi aliyekuwa akipewa bahasha na watu fulani aipeleke sehemu fulani. Siku moja dereva huyo alipewa bahasha ikiwa wazi/haijafungwa hivyo dereva alipata shauku ya kutaka kuona ni nini ambacho amekua akibebeshwa kwenye bahasha siku zote hizo. Ndipo alipofungua bahasha hiyo na kukuta list ya majina mengi ya watu/viongozi yakiwa yameandikwa kwa pamoja na codes zisizoeleweka, Anasema lilikuwemo jina la Rais wa awamu ya 5 na hata la kwake pia Polepole lilikuwepo!

Mwisho, Ndugu Polepole amemwambia muheshimiwa Rais wa sasa kuwa asiende kuchukua fomu kesho kwani kufanya hivyo itakuwa ni kuwatukana watanzania wote wanaoona mbali kuliko anavyoona yeye na hao waliomzunguka wanaomshinikiza kuchukua fomu na kuwania uRais.

Nimetafakari sana, wacha tuone!​
View attachment 3436166
Natambua hata wewe utakufa kilanfsi itapitia hayo kwahiyo wewe muhuni uliona ajabu kufa polepole bana anaongea ujinga wakuoza kweli
 
Muuaji wa kibaka ndio anaweza sahau, mtu yeyote anayepanga mipango mirefu ya kuuwa watu ngazi ya juu kwa nyakati tofauti na kwa njia tofauti akiwemo kumuua Rais usidhani ni muuza gongo au ana akili za kupikia andazi.

Hakuna kujisahau kwa kutuma barua iliyofunguliwa kwa dereva tax. Na hakuna mantiki kuandika list ya majina na kutumiana. Hata wauaji wa mwenyekiti wa kitongoji si wajinga kiasi hiki.
Inafikirisha ...

Kwanini wamtume dereva teksi kupeleka hizo barua wakati wangeweza kupanga gizani bila kuandika chochote.
 
Kuongea yote kwa siku moja hawezi, ina maana aongee siku tatu bila kula wala kunywa?
Anaweza. Polepole anaongea jambo la kusema neno moja kwa kutumia maneno elfu moja.

Angeeeza kumaliza yote muhimu anayotaka kusema katika siku moja.

Ila kawajulia wabongo wanapenda stories nyingi za ubuyu, ambazo ukizipima unakuta contradictions nyingi sana.

Hapa anakwambia anapenda haki, katiba, ukatiba, pale anakuambia Samia hafai kwa sababu hafuati tamaduni na desturi za CCM (bila ya Polepole kusisitiza katiba).

Wanaopenda ubuyu wanafurahia. Wanaoangalia deep wanaona huyu mtu anawachezea akili katika internal power struggle huku akijifanya anatafuta mabadiliko.
 
Mimi nashangaa watu wanamuona jamaa kama anatunga .. hawajui hizo ni codes na Zaid nashangaa watu wanawadharau Hawa matex driver na boda,,Mimi kati ya watu naowaheshim nikienda mahali papya ni boda boda na teksi drivers ...na wazee wale wanaokaaga kucheza bao na kunywa kahawa muda wote ...imeshaniokoa nisipate ukimwi...nyie acheni bwana ..ujasusi una mambo mengi anatumiwa mtu yoyote ambaye wewe humdhanii kabisa ...
Daah sasa hii ni ujasusi kwenye harakati za umalaya sindio 😃😃😃😃😃😃😃😃🤣🤣🤣🤣🤣
 
Ikiwa wazi ndio hoja hapo, kama ingeachwa wazi akaipeleka mmoja wao(anayehusika) isingekuwa tatizo.​
Hata Osama alitumia barua kwenda kuwasiliana na washirika wake ukitumia usasa km internet na simu ni rahisi kujulikana ...
 
Back
Top Bottom