Polepole: Kuna mtu alikuja kuniambia kuwa kiongozi wa awamu ya 5 atakufa

Polepole: Kuna mtu alikuja kuniambia kuwa kiongozi wa awamu ya 5 atakufa

Nimemaliza kumsikiliza pole pole naona taifa linaandaliwa vema kisaikolojia kujisimamia mwaka huu.

Nukuu za Pole pole.

1/ Mama ukichukua form na kugombea Urais utakuwa umetutukana watanzania wote.

2/Mama unataka kugombea na Salum Mwalimu wa chauma, Mama unataka kugombea na Mpina wa Act. Kweli mama unataka kugombea na hawa na moyo wako una amani kabisa?

3/ Kwani Act sisi ccm hatuijuhi? Pole pole anatufumbua macho na kututhibitishia jambo hapa kuhusu Act.

4/ Pole Pole anashauri mama amuachie Mh Lissu bila masharti aende kwenye familia yake. Kisha aitishe muafaka wa kitaifa kabla ya kuingia kwenye uchaguzi. Amesema vyombo vya dola vitajipanga kutokana na maamuzi ya wananchi ambao ndio wenye nchi. Hapa maana yake tume isituambie muda umekwisha. Kila jambo linawezekana waamuzi wa mwisho ni wananchi sio ratiba za serikali na vyombo vyake.

5/ Kuhusu Hayati magufuli sizumgumzii chochote kila mmoja ameelewa code za Pole pole.

6/ Kuhusu Ndugai na kobe wa uvvccm kupandishwa juu ya mti ili kumtukana Ndugai na kumlazimisha ajiuzulu pia sisemi.Mtu yule kutoka kundi la mtandao anayeogopeka na kutisha. Aliyekwenda Dodoma kwa Ndugai na kumwambia jiuzulu na kisha mzee akasema.Nimekosa mimi...Nimekosa sana..Nisameewe huyo naye simzungumzii.Pole pole Amesema kundi hilo linatisha sana.

Hamphrey Pole pole you made my day.

Chadema wako sawa tukatae wahuni kwanza ndipo twende kwenye uchaguzi.This is our country.

Wale mnaodharau msimamo wa chadema muwe na adabu mmeelewa sasa nchi iko wapi.

Wale mnaosema wana chadema wanamezwa na hoja za pole pole muwe na adabu.Huyu jamaa ametujengea nguvu ya mapambano leo kiasi kwamba tunaona kabisa huu ndio mwaka wa mabadiliko.

Kataa wahuni ponyesha Tanzania.
Hard times don't last.
 
Huyu anamjuwa JPM anawashibiki wengi na wengi hawajawahi kuamini kuwa JPM amefariki tu kuna kitu kafanyiwa lakini sote tunajuwa alikuwa mgonjwa na wasaidizi wake wengi waliondoka na corona. Kwa ufupi binadamu anaweza kuumwa ghafla na kufariki kawaida tu.

Analeta shutuma nzito sana ili kuwateka wale waliokuwa damu damu kwa JPM kuwadhibitishia kweli aliuliwa ni mbinu za kuleta mtafuruku. Sasa akili ya kawaida kabisa mtu mwenye information kama hizo kweli atampelekea Polepole? Rais anazungukwa na watu wa karibu sana ni ngumu sana kumfikia na kumdhuru labda watu wa ndani na yeye kasema hata kuonana na mkewe anapangiwa hayo maneno yake. Ni ya polepole ni kuwateka wale wafuasi wa JPM na hasa huku mitaani kuwaaminisha mlichokuwa mnadhania ni kweli sasa tuungane. Huyu mtu ni hatari sana.
Si kweli, anachosema kina ukweli mkubwa ndani yake ndio maana wanazima mandao hovyo, mara wanakwenda kumteka dada yake...

Jamaa anaonekana ana taarifa nyingi sana za siri kiasi cha wanamtandao kumuogopa...
 
Polepole ajifunze hilo bomu moja TU wanapoteana na ushahidi JUU. NAMBIE ushahidi WA kile kilicho somwa na dereva tax kikowapi?
Ndio anachosubiria wajichanganye kumjibu fyongo amwage mafaili yote hadharani, wewe hujamwelewa bado ila subiria episode nyingine utamwelewa taratibu yeye anawajua wote wanaohusika ila anawatonya waache Uhuni

Sogeza kete hio
 
Leo kwenye muendelezo wa mawasilisho yake huko mitandaoni Ndugu Humphrey Polepole amesema kuwa wakati wanakaribia uchaguzi mkuu 2020 kwenye kazi yake ya kusikiliza wananchi kuna bwana mmoja alimfuata akamwambia kuwa kuna watu wanapanga kumuua Rais wa wakati huo!

Anasema alipeleka ujumbe huo kwa muheshimiwa Rais, ambae pamoja na mengine alimwambia kuwa habari hizo akamwelezee msaidizi wake fulani ambae Ndugu Polepole hajamtaja.

Anasema pia palikuwepo dereva Taxi aliyekuwa akipewa bahasha na watu fulani aipeleke sehemu fulani. Siku moja dereva huyo alipewa bahasha ikiwa wazi/haijafungwa hivyo dereva alipata shauku ya kutaka kuona ni nini ambacho amekua akibebeshwa kwenye bahasha siku zote hizo. Ndipo alipofungua bahasha hiyo na kukuta list ya majina mengi ya watu/viongozi yakiwa yameandikwa kwa pamoja na codes zisizoeleweka, Anasema lilikuwemo jina la Rais wa awamu ya 5 na hata la kwake pia Polepole lilikuwepo!

Mwisho, Ndugu Polepole amemwambia muheshimiwa Rais wa sasa kuwa asiende kuchukua fomu kesho kwani kufanya hivyo itakuwa ni kuwatukana watanzania wote wanaoona mbali kuliko anavyoona yeye na hao waliomzunguka wanaomshinikiza kuchukua fomu na kuwania uRais.

Nimetafakari sana, wacha tuone!​
View attachment 3436166
Nijuavyo kuna messengers alichosema kaka yetu ni code kuwalinda hao messenja
 
NAMI NAKUTANDIKA SWALI MKUU KUONYESHA HUFIKIRII NJE YA BOX. JE SAMIA ASINGE CHUKUA FOMU UNAONA HUYU POLEPOLE ANGEONGEA CHOCHOTE? KAMA ANA NIA NJEMA NA TAIFA KWA NINI ASUBIRIE SAMIA KISA KUCHUKUA FOMU NDO AJITOKEZE JE SAMIA ASINGE CHUKUA FOMU? INA MAANA KUSINGE KUWA NA HAJA YA KUONGEA HAYO. JE HUO NDO UZALENDO?



Kwishaaaaaa
Swali la kindezi issue ni muda sahihi na wakati sahihi wa kuongea na yeye ameona huu ndio wakati sahihi wa kuongea
 
Anaweza. Polepole anaongea jambo la kusema neno moja kwa kutumia maneno elfu moja.

Angeeeza kumaliza yote muhimu anayotaka kusema katika siku moja.

Ila kawajulia wabongo wanapenda stories nyingi za ubuyu, ambazo ukizipima unakuta contradictions nyingi sana.

Hapa anakwambia anapenda haki, katiba, ukatiba, pale anakuambia Samia hafai kwa sababu hafuati tamaduni na desturi za CCM (bila ya Polepole kusisitiza katiba).

Wanaopenda ubuyu wanafurahia. Wanaoangalia deep wanaona huyu mtu anawachezea akili katika internal power struggle huku akijifanya anatafuta mabadiliko.
Kama mambo muhimu ya taifa yangekuwa yanaisha kwa siku moja ya maongezi, dunia yote ingekuwa imetatuliwa matatizo yake kwa haraka, ukweli ni kwamba, masuala ya haki, katiba, na mustakabali wa nchi yanahitaji mazungumzo ya mara kwa mara, ufafanuzi wa kina, na uvumilivu wa kuyajadili tena na tena , hizii si hadithi za ubuyu...

Hata Donald Trump, akiwa Rais wa Marekani, aliwahi kusema ataweza kumaliza vita vya dunia kwa siku moja tu akipewa nafasi, hadi leo, vita hivyo vinaendelea , hii inaonyesha kwamba masuala makubwa ya kisiasa na kimataifa hayawezi kumalizwa kwa maneno machache au siku moja, yanahitaji muda, mikakati, na mjadala wa mara kwa mara....
 
Kitengo kinatengeneza upinzani feki ndani ya CCM ili kudivert attention ya ya umma juu ya upinzani halisi wa nje ya CCM.

Kitengo kinajua umma unahitaji upinzani, ila kwa sababu kimeupiga pini upinzani halisi wa CHADEMA kinawapeni upinzani feki wa Polepole ili mhangaike nao.

Narudia tena, hakuna hero katika CCM ya leo anayeweza kuacha mpunga mrefu wa ubalozi kuja kupambana na Amir Jeshi mkuu eti kutetea taratibu za CCM. Hakuna
Umeongopewa na naani au wewe ndio ulikua mgawa bahasha kwa yule dereva Tax?
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Sasa atafanyaje kama chadema wanaamini na wanafurahia na wanapata Imani kabisa kuwa kupitia 'stori ya kipumbavu' kama hiyo itamfikisha lissu ikulu?!!! Acha ajikusanyie viewers za mizembe hii kutoka chadema.
Mmoja wa Wajinga aliyepo JF pole sana kwa Familia na Ukoo wako.
 
Mkuu hata mimi leo nilivyoanza niliweka screen mbili mpja nanenane kwa Ssh moja kwa slow slow polepole.
Sijamaliza dakika 15 nikaenda piga mishemishe tu,

Yeye amwage mchele wote hata liwe press la masaa 12, wstu waamue sio hivi inamendea mendea kwamba wakinyoosha mambo hatosema. Huu ni utapeli


Kuna mdau mmoja leo kasema ni kama anafanya blackmailing , nakubaliana naye
Atasema unachokitaka ni suala la muda tu usichoke kumsubiria
 
Akili zichaji kwa hizi ngonjera za Polepole?
Ajikite kwenye hoja za msingi mara zote sababu atapuuzwa na kukosa hata hii audience inafuatilia kila baada ya siku tatu.
Wewe unataka kusikia nini kutoka kwake? Hata akikwambia unachotaka kukisikia utaamini au utakuja hapa kuendelea kumpinga kwamba anakwambia uongo? Unataka nini evidence? Unataka akuonyeshee mafaili?
 
Back
Top Bottom