Hebu nieleze kirahisi zaidi.
Polepole ni mwanasiasa aliyejikuta kundi lake halina nguvu na kundi lenye nguvu si lake. Anataka kumuondoa Samia asigombee urais. This is a CCM power struggle far and above anything else.
Kutaka Samia asiwe rais na kutaja mapungufu mengi ya Samia si lazima mtu awe muongo, kwa sababu ni kweli Samia ana mapungufu mengi, kaharibu mambo mengi ikiwa pamoja na alivyoanza kuchukua nomination za CCM, alivyoanza kampeni kabla ya bunge kuvunjwa, alivyopata nomination kwa kikao cha ambush nje ya ajenda ya kikao.All this is fair criticism against Samia. Wengi tunaona haya ma mengine mengi.
Mchungaji Dr. Malisa kafungua kesi mahakamani na mahakama imeitaka CCM kujieleza. Kuna kesi ya dharula imekuwa fast tracked imalizike tarehe 14 August nafikiri ili kuwahi ikamilike kabla ya uchaguzi. Kwa hiyo si jambo ambalo analisema Polepole tu, wengi tunaona haya mapungufu. Mahakama imeona CCM ina cha kujieleza, lingekuwa jambo dogo kesi ya Dr. Malisa ingetupiliwa mbali.
Samia nchi imemshinda watu wanatekwa na kuuawa anasema kifo ni kifo tu. Samia nchi imemshinda, hawezi uongozi wa kweli na haki.
Lakini Polepole hampingi Samia kwa sababu Samia hafanyi uongozi wa kweli na haki.
Magufuli alifanya siasa chafu za kununua wapinzani. Alivunja katiba kwa kukataza mikutano ya kisiasa. Polepole ndiye alikuwa anaongoza mpango mzima wa kununua wapinzani. Anajua mengi sana kuhusu mauaji na utekaji wa siku za Magufuli. Kwa hivyo Polepole hasumbuliwi na uongozi mbaya. Anasumbukiwa na ukweli kwamba katolewa from the center of power katupwa Cuba huko awe mbali na siasa za Tanzania.
Polepole anampinga Samia kwa sababu si team yake ndani ya CCM. Kina Polepole ni Sukuma Gang waliotaka katiba ipindishwe Samia asiwe rais. Hawajaridhika Samia kuwa rais wanataka mtu wao awe rais.
So this is a power struggle within CCM. Hayo mambo ya uongozi anayodai Polepole yana contradictions nyingi sana.
Polepole anasema yeye anasimamia katiba na ukatiba dakika moja, dakika ya pili anasema Samia asigombee urais kwa sababu utamaduni na desturi vinamzuia.
Kwa nini anataka kutumia utamaduni na desturi sehemu ambayo CCM na nchi zina katiba ambazo hazimzuii Samia kugombea urais?
Kwa nini anataka kumvunjia Samia haki yake ya kikatiba?
Kwa nini Polepole anasema Samia aache urais abaki Mwenyekiti wa CCM? Kama Samia hafai urais kwa nini afae uenyekiti wa CCM? Haya, labda Samia kaharibu nomination process, kwa nini Polepole hataki nomination process irudiwe watu wote wa CCM wanaotaka kugombea waruhusiwe kugombea, akiwamo Samia, kama wajumbe hawamtaki Samia wamkatae, kama wanamtaka wampitishe?
Kwa nini anataka kutumia utamaduni na desturi, vitu ambavyo havijaandikwa popote, wakati CCM ina katiba na kanuni zilizoandikwa, nchi ina katiba na sheria zilizoandikwa?
Ukichunguza sana utaona Polepole hana nia ya kuweka ukweli wazi, ana nia ya kufanya siasa za kumuondoa Samia.
Ndiyo maana hata kwenye kusema maneno anadunduliza kupata mileage, jambo la kusema kwa neno moja anataka kulisema kwa maneno elfu moja.