Mkuu ni niko central police mkoa fulani muda huu, wanasema mwacheli Lissu atutetee, tumeteseka sana
JPM amefanya mambo makubwa sana na kunyamazisha wapinzani ili yasiyofanyika yasisemwe na makosa yasionekane.
JK alifanya makubwa zaidi lakini hakuwanyamazisha wapinzani wake .
Hata Watu binafsi wengi walijipatia maendeleo yao kipindi cha JK.
Kama JK asingeyaendeleza majeshi na Wafanyakazi hasa kadaktari leo hii PM asingekuta Majeshi yatu yakiwa imara kama yaluvyo. JK aliboresha miundo mbinu ya majeshi yetu na maslahi yao. Alinunua Manowari, Alinunua ndege za kivita kulinda nchi yetu ,alinunua vifaru vingi, Aliwapa Mali asili silaha za kisasa kulinda wanyama wetu n.k. Mfano ni nyumba za kisasa za askari wetu alizojitahidi JK kuwajengea tofauti na JPM ambaye hajawajengea wanajeshi wetu hata nyumba za mabati kama wakati wa mkoloni. JK alijenga kambi za JWTZ nchi nzama lakini hakuwa anaweka mabango na matangazo ya kuzindua na kuhishia vyombo vyote vya habari kumsifia . Alijua ni wajibu wake kutumia Kodi za wananchi na mikopo ya nchi kujenga miundo mbinu ya serikali. JK alijenga sekondari za kata nchi nzima lakini hakuzifunga shule binafsi wala kuzifanya figisu.JK alijenga vyuo vikuu lakini hakufunga vyuo binafs. Vifaa vyote wanavyotumia majeshi yetu yote ni vile vile vya enzi za JK.
JK alojenga Hospitali kubwa Kama Mloganzira ,Jakaya na Dodoma lakini hakuchukua vyombo vyote vya habari kwenda kumsujudia ,kusifu,na kuchukua wachungaji kumweka kwenye ratiba za ibada kama Mungu.
Nchi hii inavurugwa na watu wabinafsi wanaotumia ukubwa wa CCM kufanya wanayotaka wakijua hawatafanywa lolote kama alivyosema Kheri yule wa UVCCM.Yani watu kama Kada wa CCM na Mwenyekiti wa NEC wanajawa na kiburi cha kufanya Chochote wanachoona kitawapa maslahi yao binafsi na kulinda vyeo vyao. Mungu haogopwi tena zaidi ya mtu aliyewateua. Hata vyombo vya dola,mahakama, bunge wote hawamuogopi tena Mungu zaidi ya mtu mmoja aliyewateua na kuwapa mishahara mikubwa. Wakuu wa wilaya ,wakurugenzi, wakuu wa mikoa,mawaziri, hawaheshimu katiba wala hawamuogopi Mungu zaidi ya mtu mmoja aliyewateua.
Kwa katiba hii CCM ikirudi madarakani itawaumiza watu wengi sana mana wamegundua kuwa watu wengi hawawapendi. CCM itatumia nguvu kubwa maradufu kuhakikisha lengo lao la kuua upinzani linatimia.
Kama kuna Mtu yeyote anayedhani kuwa CCM ikiua watu wote wasioiunga mkono watapata maendeleo ya madaraja watajidanganya. Maendeleo bila watu. CCM na tume ya uchaguzi wakiwaua maelfu ya watu wajue watanzanua wote ni ndugu.
Ndio maana polepole anatengeneza magenge ya watu wasiojulikana .Polepole na NEC wanapochafua hali ya hewa wanawachia mzigo mkubwa vyombo vya usalama.
Historia ya nchi hii tangu mkoloni kuna makabila makubwa yaliyokuwa yanapewa nafasi za kati za utawala lakini sio nafasi za juu kabisa. Ukimpa mtu nafasi ya juu kwenye makabila hayo yenya nguvu kubwa ,kielimu,kiuchumi,kisiasa na hata wingi wao kijamii basi watatumua nguvu kubwa sana kuyanyamazisha makabila madogo madogo wakiwa na matumaini ya kutumia ukubwa wao kuteka afasi zote za madaraka ,uchumi, ajira n.k. Haikuwa jambo la kubahatisha kuona uoanda mmoja unapewa madaraka ya juu yote mpaka TUME ya uchaguzi. Ni mwanzo tu. Wakifanikiwa kuua upinzani watawaengua wa makabila menginene kwenye ukanda huo na hatimaye watawaengua mpaka wabaki wa ukoo mmoja tuu. Ndio maana wenye akili kwenye ukanda ule wanaikataa CCN wakijua kuwa hii ya kujifanyia Kikanda ni danganya toto kwa watu wachache wenye uchu wa madaraka. Uchu huo wa madaraka upo mpaka ndani ya vyombo vya dola. Kuepuka mgawanyo wa Kikabila ulioanzishwa na Bashiru Alli na Polepole wakisaudiwa na NEC ni kuwakataa CCM nchi nzima. Malengo yao maovu yatashindwa.
Mungu aliyeimarisha Uchumi wa Misri ndiye huyohuyo aliyeishusha na kumwangamiza Firauni.
Mungu aliyeiondoa Korona ndiye huyohuyo aliyemponya Lisu na kumpa ujasiri wa kutetea Taifa lenye Haki na usawa kwa binadam sio kuumiza watu kwa sababu ya kujenga minara ya Babeli.