GE2025 Polepole yuko sahihi kuhusu utaratibu CCM kukiukwa; Ilani ya uchaguzi ya CCM iko wapi, na ikiletwa Samia ataisimamia kwa kipindi kimoja tu akiwa rais?

GE2025 Polepole yuko sahihi kuhusu utaratibu CCM kukiukwa; Ilani ya uchaguzi ya CCM iko wapi, na ikiletwa Samia ataisimamia kwa kipindi kimoja tu akiwa rais?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hilo nahisi waliliweka Ili hao waliyotajwa hapo juu wasiweze kumhujumu mkuu wao wa kazi.it is a very good idea .si unaona yanayotokea kule Kenya?
Sijakuelewa. Unaposema hilo unakusudia lipi? La utamaduni? Kwamba limewekwa ili PM, VP na Spika wasimhujumu Rais?

Sasa kuwawekea vizingiti ambavyo haviko hata kwenye maandishi ndiyo kunawazuiaje kumhujumu rais?

Yani mtu akitaka kumhujumu rais atashindwaje kwa sababu tu yeye hawezi kuwa rais?
 
kumbe mama samia alisimamia ilani ya CCM ya awamu ya tano.heee.kazi ipo wangosha.ila ni kweli.tulifanya makosa kuiita awamu ya sita bila ilani mpya ya chama.na ndiyo maana kila miradi aliyotekeleza ni ya awamu ya tano na anayesifiwa ni hati JPM aliyeshiriki kuiandaa.sasa kama kwenye uchaguzi huu inaandaliwa ilani mpya ya CCM ,ni dhahiri mama akishinda ataitekeleza kwa miaka mitano tu.in that case CCM iandae ilani ya miaka mitano tu
Sawa CCM iandae ilani ya miaka mitano , je! Nisifa ipi inayomsabanishia Mama apite bila kuingia kwenye mchujo ? Kinachomsababishia asiingie kwenye mchujo ili kupata tatu Bora na kisha jina moja ni kulipia?

Tuanzie hapa.
 
Mi Nina wasiwasi Nchimbi ndo atakuwa Rais, Samia hata mtu wa kugombea nae alikuwa anaweweseka amuweke nani, Sasa huyo nchi atamning'iniza
 
Tutakuwa watu wanafiki sana ikiwa tunaweza kumtazama Polepole kama mnafiki na asiye na mapenzi kwa Taifa lake .

Wazee hivi tunayajua maisha yakibalozi au tunayasikia tu kwenye radio?

Mtu kuyakataa maisha yakibalozi tena ubalozi wa Cuba kwa maslahi ya Taifa lake siyo jambo jepesi .

Najua hakuna mkamilifu ila jamaa amejitahidi sana .

Sote hapa tunaifahamu namna mazingira yalivyo kwawakati huu kupata kiongozi wa TAIFA kutokea upinzani siyo jambo jepesi japo tunajitahidi sana kuifikia hiyo ndoto .

Hii maana yake ni kwamba ,kama Taifa litakosa watu wa aina ya katiba ya Balozi mstaafu Polepole kusimama nakuwa tayari kuyaacha mapochopochobyote yakibalozi ili kuhakikisha siyo tu Taifa linapata viongozi kwa mtiririko unaoeleweka lakini kwangu ninaloliona nikuthubutu kumvusha kengele huyu jinamizi linyonyadamu lisilo na haya ,wazee siyo uamuzi wa mchezo mchezo mjue.

Mungu aendelee kuwatia moyo wote wanaoendelea kusimama imara hata ku_risk maisha yao kwa maslahi mapana ya Taifa.

Taifa lipo shimoni japo anamema yake lakini hili la chinja_chinja aah! No
#Mama_hapana
 
Tafsiri

Awamu ni kweli siyo ya 6 ni ya 5

Ila Katiba ya JMT inampa fursa Dr Samia kugombea sasa na atakaa kwa miaka 5 tu na Kwahiyo awamu ya 6 itakuwa ya miaka 5 kisha itakuja awamu ya 7

Kule Zanzibar awamu ya Idrisa ilikuwa ni miaka 5 tu

Ahsanteni sana
🤣 ukiona magazijuto yanakuwa mengi jua things are not okay
 
Tutakuwa watu wanafiki sana ikiwa tunaweza kumtazama Polepole kama mnafiki na asiye na mapenzi kwa Taifa lake .

Wazee hivi tunayajua maisha yakibalozi au tunayasikia tu kwenye radio?

Mtu kuyakataa maisha yakibalozi tena ubalozi wa Cuba kwa maslahi ya Taifa lake siyo jambo jepesi .

Najua hakuna mkamilifu ila jamaa amejitahidi sana .

Sote hapa tunaifahamu namna mazingira yalivyo kwawakati huu kupata kiongozi wa TAIFA kutokea upinzani siyo jambo jepesi japo tunajitahidi sana kuifikia hiyo ndoto .

Hii maana yake ni kwamba ,kama Taifa litakosa watu wa aina ya katiba ya Balozi mstaafu Polepole kusimama nakuwa tayari kuyaacha mapochopochobyote yakibalozi ili kuhakikisha siyo tu Taifa linapata viongozi kwa mtiririko unaoeleweka lakini kwangu ninaloliona nikuthubutu kumvusha kengele huyu jinamizi linyonyadamu lisilo na haya ,wazee siyo uamuzi wa mchezo mchezo mjue.

Mungu aendelee kuwatia moyo wote wanaoendelea kusimama imara hata ku_risk maisha yao kwa maslahi mapana ya Taifa.

Taifa lipo shimoni japo anamema yake lakini hili la chinja_chinja aah! No
#Mama_hapana
Tatizo la wabongo weng hawana akili na wanahulka kuchukulia mambo juu juu sana, laiti wangejua benefit za balozi basi wangepaswq kujiuloza kijana pole pole anaachaje all the benefit
Hapo ndio inapokuja ishu ya uzalendo
Polepole hajaacha ubalozi kwa kuwa Samia anauwa Watanzania

Pole pole kaacha ubalozi kwa kuvunja katiba ya nchi na CCM

Hoja za mazuzu kuwa why enzi ya JPM alikaa kimya ni mufilisi

Uuaji na utekaji wa Samia sio sababu ya polepole kukataa ubalozi

Ishu ni why tunakiuka taratibu
 
Nani ataisimamia dira ya CCM ya taifa 2050??
Hayo mambo ya ilani na mihula ni mbwembwe tu
 
Huyo anapigania maslai yake tu kusudi apate madaraka aendelee kuwaumiza Lissu ndo mzalendo Reforms sio za Lisuu kizazi na kizazi wanaweza kufaidika na

Ikiwa Polepole anasemwa anapigania maslahi binafsi, Samia tutasemaje? Unajua, mambo ya uongozi huwezi kulazimisha kwamba lazimauwe wewe. Katika hali ya kawaida huenda ingekuwa busara Samia kusema isiwe nongwa, ngoja mie niache. Kwa lazima yeye awe ndio raisi? Kwa nini, kama wewe kweli una nia njema na uongozi wa wananchi, ukiona uteuzi wako unaleta mitafaruku sana, husemi basi jama ngoja nijitoe?
 
Ibara na vifungu vya JMT viko sawa, kugombea sawa, ni mchakato. Huku nikujiteua
Samia na Kikwete wana lawama nyingi sana kuharakisha uteuzi na kuharibu utaratibu wa kumpata mgombea kwa kutumia ambush tactics. Hili hawakosi lawama na kwa kweli uteuzi unatakiwa kurudiwa, ama sivyo hata Samia akiwa rais atakosa uhalali fulani.

Lakini pia.

Samia kwa kauli yake amesema 2030 hatagombea urais, atarudi Kizimkazi, na kwa katiba ya sasa haruhusiwi kugombea.

Samia , kwa katiba ya nchi, ana haki ya kugombea urais mwaka 2025 na kuwa rais mpaka 2030, hili jambo limewekwa wazi kwenye katiba si jambo la kuganga ramli habari za "ofisi ya urais imetumika kwa miaka 10".

Katiba ya nchi imeweka wazi Makamu wa Rais akiwa rais kwa kifo cha rais ni wakati gani anaweza kugombea kipindi kimoja tu na wakati gani anaweza kugombea hata vioindi viwili.

Ibara ya 40 (4) inasema hivi kuhusu makamu wa rais kugombea urais baada ya rais kufariki. Nimeiweka hapo chini isome.

Moja ya items za ibara ya 37(5) ni mtu, makamu wa rais, kushika urais baada ya rais kufariki.

40 (4)
Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa
mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua
miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili,
lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au
zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu.
A
 
Ibara na vifungu vya JMT viko sawa, kugombea sawa, ni mchakato. Huku nikujiteua

A
Sasa ndiyo kashajiteua, mnamfanya nini?

Hivi kama Samia akishinda urais - na dalili zinaonesha atashinda, ana kila nguvu ya dola kushinda hata kabla hatujaenda kwenye kura - so akishinda, urais wake utakuwaje?

Ataweza kuendesha nchi sawa kwa urais unaoanza na wingu hili la kukosa uhalali?

Je, huu ni upepo unaopita tu, kama alivyojisemea Kikwete?

Au urais wake utagubikwa na wingu la kukosa uhalali na kelele za watu mwanzo mwisho mpaka ashindwe kuongoza vizuri?

Watanzania wanaweza ku focus kumshinda Samia mpaka jambo kubwa litokee?

Au hizi kelele za sasa ni mambo ya "ngoma ya watoto haikeshi"?
 
Back
Top Bottom