Ni sahihi mkuu, na hata sasa wapo wanaendelea kufurahia tukio hili..Very true, hata hapa Jukwaani kulikua na Wapuuzi wengi wengi sana waliotaka na kuhamasisha Tundu Lissu auwawe, maandiko yapo hapa na maandiko yanaishi.
Nape..watu wasiojulikana..Hawa polisi wetu huwa wanabadilika na kuwa hao wasiojulikana...nashangaa hizi movie zinavyoenda,
Baada ya office za Immma kulipuliwa mashahidi walisema waliofanya hilo tukio walionekana kuvalia sare za polisi kaki...lkn badae tukaambiwa watu wasiojulikana...
Lissu alishasema vijana Wa Sirro na Tissss wanamfatilia na Toyota Premio kila kona aendako,na Sirro+Tissss hawajakanusha hilo swala...
So finally ktk conclusion ni kwamba,Watu wasiojulikana ni hawa hawa polisi wetu na tixxx wetu waliopo ktk jamii yetu
Mnataka kwenda mbio wakati hakuna break..... Funzo sio tabia nzuri kutengeneza maadui bila sababu.... Ulimi uliponza kichwa!
Mungu awahurumie pia wale wote wasiojielewa na wenye ubinafsi uliopitiliza....asiwasahau wale wote wenye akili na nia mbaya ya kuliingiza taifa kwenye matatizo kwa sababu zao binafsi na kutumia udhaifu wa watanzania.... hawa ni pamoja na wale wote;Mungu akuhurumie sio akili yako.............. Nimeomba rehema kwa ajili yako
funguka zaidi mkuuThere were multiple shooters
The numbers of bullets (25) has got the hidden message for those with active brain
The truth is that the multiple shooting was just a camouflage
Lets pray for Our beloved hero.
Kugeuza tukio baya na Unyama aliofanyiwa Wakili Msomi Tundu Lissu kuwa MTAJI WA KISIASA ni mtindio wa Akili na Upuuzi unaopaswa kupingwa na kila anayejitambua.
Lissu sio Chadema tu Lissu ni Mtanzania na kila mtanzania atakayeonewa na kufanyiwa dhulma awe mwanasiasa asiwe mwanasiasa wote wanastahili huruma yetu na sauti zetu kuwalilia , na kuwapigania katika uzito sawa.
Lissu anatetea maslahi ya Tanzania yote kwa Ujumla hivyo ni haki ya kila mtanzania kumlilia na kumuombea. Kuleta chuki zenu au tofauti zenu za Vyama kipindi ambacho taifa limeungana kumlipa fadhila mtu aliyejitolea muda na maisha yake kulipigania ni Ujinga na Upumbavu unaokera sana.
Tukio la Lissu linapaswa kuchukuliwa kama chachu ya mapambano dhidi ya Waovu na Madhalimu wa haki za Binadamu na utu kokote kule walikojificha.
Unyama huu haukuanza na LISSU wengi tumewazika waliuawa kwa dhulma na kwa kuonewa tu bila kosa lolote.
Watu wengi ndani ya taifa hili wamepotea, wameuawa, wametekwa, wamefungwa Jela kwa dhuluma na Uonevu, na wengine maiti zao zimeokotwa kando kando ya mito, maziwa nk baadhi yenu hamkutaka kabisa kuongea na mliona hayawahusu.
Tulichukulie tukio hili kama kengere ya kuamsha mapambano dhidi ya Wahuni waliogeuza Taifa hili kuwa ni sehemu ambayo ukifumbua mdomo kuisemea haki unatafunwa. Tupambane na Wahuni wawe katika kichaka chochote walikojificha tukichome moto watoke angalau nasisi tuwe tunajiamini katika taifa letu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
Sent using Jamii Forums mobile app
Haikuwa eneo la Bunge ilikuwa ni Nyumbani kwa Mh. LissuYaani siyo siri nilipatwa na uchungu sana jana na usiku wa leo. Nilijiuliza mambo mengi mengi sana lakini nikawa sipati majibu. Na kilichokuwa kina nisumbua mpaka sasa ni kwamba serikali ilikuwa Dodoma kwenye kikao cha bunge, halafu bungeni kuna ulinzi wa kutosha, hiyo bunduki iliyotumika haikutoa mlio? Au ilikuwa kama mshale? Milio ya bunduki inafahamika ni aina gani na maaskari wanajua.
Swali: Iweje mtu aingie eneo hilo la bunge na kufetua risasi kama mvua asikamatwe? Huyo mtu alijiamini vipi? Au wabunge wetu hawana ulinzi? Hao watu wanaojitetea nao waliingia je eneo la bunge wakati magari yanakaguliwa? Bado kichwa kinapata moto.
Polisi ya bongo bwana...
Ingelikuwa ni wenzetu kwa kutumia vidhibiti vidogo vidogo tu kama ukubwa wa matundu ya risasi, maganda ya risasi n.k
Sasa hivi tungekuwa tushajua angalau silaha ilinunuliwa au ilosajiliwa kwa nani, mpigaji au wapigaji wanatumia mikono gani n.k...
Lakini sasa bongo kama kawaida yao upelelezi unategemea umbea umbea tu...
Sasa kazi Yao ni nini? Kama hawana taarifaHABARI MPYA: Kamanda wa Polisi Dodoma amesema yeyote mwenye taarifa kuhusu wahusika waliompiga risasi Tundu Lissu waiwasilishe polisi.
Kwa sasa wamepata taarifa kuwa gari iliyoonekana ni gari nyeupe aina ya Nissan.
Naye mkuu wa mkoa wa Dodoma amesema polisi wameshaanza kufanya upelelezi kuhusu wahusika na kusema watu waendelee kusubiri taarifa kutoka kwenye jeshi hilo
Amesema hawatapenda kuona mikusanyiko sehemu yoyote ya Dodoma mjini kwa sababu jeshi la polisi bado linafuatilia asili ya tukio lenyewe na mikusanyiko ya watu inaweza kutumika vibaya.
Pia wataendelea kuwafaamisha raia kwenye kila hatua watakayofikia
[HASHTAG]#Mwananchileo[/HASHTAG]