Polisi Dodoma: Mwenye taarifa kuhusu waliompiga Lissu risasi apeleke polisi

Sijui upelelezi kuhusu wale walipuaji wa IMMA Advocates nao umefikia wapi. Mtu asiyejulikana ni hatari sana hapa Tanzania. No wonder watu wamemaintain mizigo yao kadhaa isiyojulikana na bado maisha yao ya ndoa yapo safi kabisa
Mimi nadhani tusimuulize sirro anything labda tumuulize alie "WISH TO BE IGP KASHAKUWA IGP"? Sometimes wishes get granted jamani am just thinking loud nipo kwenye fog nene saana huku namuombea president lissu apate afya arudi kutupigania ....
 
TISS gani hao ambao wanatumia NAMBA hizo hizo za gari MOJA Kila siku?

Na AINA MOJA kila wakati katika KAZI yao? Kwani wao wangali NI WANAFUNZI?
Huo ni UVUMI na uongo mkubwa.

Professionals hawafanyi kazi namna hiyo. Eti mpaka KILA MTU analijua gari na KUKARIRI namba zao wakiwa katika SURVEILLANCE?
Huo ni uongo mkubwa.
Hao ni ni WAHUNI na wahalifu TU.
Period!
 
Bora angesema uchunguzi tufanye wenyewe
 
Msaliti hawezi kuwa kipaumbele ...Taifa lina mambo mengi ya kuyashughulikia ambayo yanaleta TIJA... why spent time and shilings kwa ajili ya MSALITI...

Ila wale waliopewa almasi ya dollar million 200 wao ni wazalendo au wale waliopelekwa kwenye maboard ya wawekezaji kuwa wwenyeviti wakala na kusaza hawa ndiyo wazalendo.Hawa waliotuletea vivuko vibovu kwa mabilioni ya shilingi hawa ndiyo wazalendo.

Hawa waluouza raslimali zetu na wao.kujigawia keki ya Taifa wanaoitwa ati wastaafu hawa ndiyo wazalendo.

Mkuu kwadanganye Lumumba FC siyo watanzania wa.Marne ya Leo.
 
kwahyo TISS ni professionals sana?? kma ni professionals mbona almas zimeibwa kwa nusu karne hawakuzuia?? mbona twiga walisafirishwa hawakuzuia.? makinikia je???

hii nchi bhana kila mtu anageuka security expert consultant
 
kwahyo TISS ni professionals sana?? kma ni professionals mbona almas zimeibwa kwa nusu karne hawakuzuia?? mbona twiga walisafirishwa hawakuzuia.? makinikia je???

hii nchi bhana kila mtu anageuka security expert consultant
Hata kama mtu si security expert ama consultant kama ulivyosema. Hata basics tuunaweza kujua uongo na ukweli.
Sijui kama TISS wamepungukiwa na magari na budget yao ni ndogo kiasi cha kutumia gari lilelie basi afazali waongezewe budget ili wafanye kazi vizuri.

Hii ni too AMATEURISH/ Ya USANII na maigizo.
Haiingi akilini.

Mambo ya Almasi na uliyoyasema nafikiri kuna taasisi mbali mbali zinazoweza kufanya kazi pamoja na si kutegemea kitengo kimoja.

Ndo naomba ujiulize.
Kwa nini Mh. Rais Aliomba bunge lichunguze haya na si TISS?
Ukipata jibu basi rudi tujadiliane.
 
Polisi wetu wanapenda mteremko hawataki kujituma asee
 
Wana JF na Moderators,
Watu tunajaribu uanzisha thread kuonyesha mwanga ambao utamsaidia IGP Sirro na Polisi kupata vyanzo vya kuwabaini wahusika wa tukio la kumshambulia Tundu Lisu. Ajabu ni kuwa JF moderators wanaunganisha threads zingine ili kupoteza lengo!!
Nimeweka uzi hapa kusema IGP hayuko serious kuwasaka wahalifu hawa kwasababu tayari Lissu na Nnape walishawahi kupeleka malalamiko kwa IGP na hakuchukua hatua. Je, IGP alikuwa anasun=biri watu wafe kwanza ndipo achukue hatua??
IGP amesema ameshatuma Polisi Dodoma wenye weledi katika upelelezi wa kukamata wahalifu wa tukio kama hilo. Lakini hapohapo tunaambiwa Polisi kwa maana ya RPC Dodoma anataka mtu mwenye ushahidi apeleke Polisi. Huu ni ujinga na upuuzi...!. Kwanini Polisi inataka kutumia raia au Wananchi kubaini hawa wahalifu??
Polisi wamesomea hiyo kazi na wanalipwa mshahara kwa kazi hizo. Kwanini wasumbue wananchi kusaidia kuwabaini hao wauaji?? Kama Lissu na Nnape walishatoa taarifa Polisi na hawakuchukua hatua nani watamwamini akiwapelekea taarifa leo kuhusu tuhuma hiyohiyo iliyolalamikiwa tena na mhanga wa tukio???

Siungi mkono kutaka eti kuwahoji Dreva wa Tundu Lissu na Katibu Mkuu CHADEMA ati wamesema wanawajua wahusika. Hii haingii akilini hata kidogo. Kwanini IGP hataki kumhoji Nnape au Hussein Bashe wote Wabunge wa CCM ambao walishafuatiliwa na kutishiwa kuuawa??Polisi lazima wajue Dreva wa Lissu naye alikuwa mhanga maana zile risasi 32 hata yeye zingelimpata na nina hakika atakuwa bado yuko kwenye shock(mshtuko). Unapomwita kumhoji dreva kwa vile aliona ile gari yenye tinted iliyorusha risasi naona humtendei haki na hakuna weledi wowote hapo isipokuwa ni ubabbaishaji unao ongeza hasira kwa watanzania.

IGP na timu yake wajitafakari vinginevyo waachie ngazi. Wanachofanya ni usanii na kucheza na akili za Watanzania. Polisi hawana nia ya kuwakamata wahusika na hapo ndipo tunaporudi nyuma na kutafakari kwamba Polisi au TISS wanajua kinachoendelea...!! Kumhoji KM Mashinji au Dreva wa Lissu ni kutaka kupoteza lengo na kujiridhisha kama kweli hawa 2 wameshawabaini wahusika ambao wako ndani ya system ili wapate mbinu za kujipanga ili kuinusuru Serikali isiaibike,

Kwa kifupi ni kwamba Polisi hawatakamata mtu yeyote watakayemkamata zaidi ya ubabaishaji na mwisho wa siku jambo hili litaachwa hewani tu kama ilivyotokea kwa Ben Saanane.
Inasikitisha sana lakini Mungu yupo na anajua kila kitu toka A-Z na kuna siku haya yote yatawekwa bayana....!!
 
Hao walilipoti polisi hayo yote uliyoandika juu yao? Embu weka na namba za mashitaka yaobkwanza then tuendelee.. hata ya Lissu weka. Hao wote wahojiwe hadi wajue kuacha kudandia mengine na kusingizia wengine.. watahojiwa tu.. sio kukimbilia kutaka kuficha wanayojua.

Dereva anasakwa sasa hivi kaambiwa ajitokeze kuhojiwa.. so subiri uone aibu itakavyowapata wengi wadaku na wanaopenda kusingizia serikali na Raisi wetu mpendwa juu ya kila kitu.
 
Rais yeye IGP yeye waziri yeye bunge yeye mahakama yeye..

Mnategemea kuwa na IGP gani zaidi?...

I think i could be IGP...
 
Tupishe tafadhali..
Wewe ni mmoja wapo wa lile kundi tuhumiwa.
 
Hivi kwa mfano nikaenda Dodoma nikasema muhusika ni Sizonje kitakachofuata ni nini? Hawa polisi wetu ni bure kabisa

Mwisho wa siku watasema aliyempiga Lisu risasi ni fundi seremala
 
Anayekulala ana Kazi kuliko askari Jela!!

ACHA nikae KIMYA...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…