Polisi Dodoma: Mwenye taarifa kuhusu waliompiga Lissu risasi apeleke polisi

Polisi Dodoma: Mwenye taarifa kuhusu waliompiga Lissu risasi apeleke polisi

Sijui upelelezi kuhusu wale walipuaji wa IMMA Advocates nao umefikia wapi. Mtu asiyejulikana ni hatari sana hapa Tanzania. No wonder watu wamemaintain mizigo yao kadhaa isiyojulikana na bado maisha yao ya ndoa yapo safi kabisa
Mimi nadhani tusimuulize sirro anything labda tumuulize alie "WISH TO BE IGP KASHAKUWA IGP"? Sometimes wishes get granted jamani am just thinking loud nipo kwenye fog nene saana huku namuombea president lissu apate afya arudi kutupigania ....
 
Nimemssikia IGP Sirro akiongea na media jana akisema Jeshi la Polisi liko serious(makini)kwenye kuchunguza nani waliohusika na shambulio la mauaji kwa Mbunge Tundu Antipas Lissu.
Ahadi za IGP kwamba wako makini na watawakamata waliohusika na shmabulio hilo zinaonesha hammanishi anachokisema. Nitaeleza.

Kuna habari za kuaminika kwamba gari lililokuwa likimfutilia Tundu Lissu toka Bungeni akielekea nyumbani kwake mchana huo ni GARI LINAJULIKANA na ndiyo hilo hilo ambalo hata Mbunge wa MTAMA(CCM) Nnape Nnauye amelitaja jana alipohojiwa na media. Nnape Nauye amesema alipoongea na BBC kwamba kwa nchi ambayo inaheshimu Utawala wa Sheria haiwezekaqni watu wawe wana toa taarifa kwa Polisi Nnape akiwa mmoja wao kwamba kuna GARI LINAWAFUATILIA na ni gari hilohilo lilimewahi kumfutilia Lissu alipolitaja kwa rangi na namba zake. Gari hilo ni T460CQV aina ya Toyota Premio la vijana wa TISS. Angalia Link hii ni ushahidi tosha: Youtube
Tundu Lissu alitoa taarifa hizi kwa IGP Sirro na Kamanda Kipilimba akiwatuhumu kuwatuma watu wa Usalama wa Taifa kumfuatilia TL badala ya kufanya kazi ya kufuatilia wahalifu.

Kama IGP Sirro yuko serious basi aanze na hili gari T460 CQV linaloendeshwa na vijana wa TISS. Watu hawa ndio walio mnyoshea bastola/bunduki Nnape Nnauye alipofukuzwa Uwaziri alipounda Tume ya kuchunguza sakata la RC Paulo Makonda baada ya kuvamia Clouds TV akiwa na Polisi. Hivo IGP Sirro anza na usajili wa gari hilo kujua nani mmiliki wake,anakaa wapi ana kazi gani na ana uhusiano gani na TISS. Nina hakika akipatikana mwenye gari hilo basi waliotaka kumwangamiza Tundu Lissu nao watapatikana.
Kazi kwako Kamanda Sirro if and only if you mean serious about this business.
Nje ya hayo IGP Sirro anaenda kuwa IGP ZIRO(0).
TISS gani hao ambao wanatumia NAMBA hizo hizo za gari MOJA Kila siku?

Na AINA MOJA kila wakati katika KAZI yao? Kwani wao wangali NI WANAFUNZI?
Huo ni UVUMI na uongo mkubwa.

Professionals hawafanyi kazi namna hiyo. Eti mpaka KILA MTU analijua gari na KUKARIRI namba zao wakiwa katika SURVEILLANCE?
Huo ni uongo mkubwa.
Hao ni ni WAHUNI na wahalifu TU.
Period!
 
Bora angesema uchunguzi tufanye wenyewe
 
Msaliti hawezi kuwa kipaumbele ...Taifa lina mambo mengi ya kuyashughulikia ambayo yanaleta TIJA... why spent time and shilings kwa ajili ya MSALITI...

Ila wale waliopewa almasi ya dollar million 200 wao ni wazalendo au wale waliopelekwa kwenye maboard ya wawekezaji kuwa wwenyeviti wakala na kusaza hawa ndiyo wazalendo.Hawa waliotuletea vivuko vibovu kwa mabilioni ya shilingi hawa ndiyo wazalendo.

Hawa waluouza raslimali zetu na wao.kujigawia keki ya Taifa wanaoitwa ati wastaafu hawa ndiyo wazalendo.

Mkuu kwadanganye Lumumba FC siyo watanzania wa.Marne ya Leo.
 
TISS gani hao ambao wanatumia NAMBA hizo hizo za gari MOJA Kila siku?

Na AINA MOJA kila wakati katika KAZI yao? Kwani wao wangali NI WANAFUNZI?
Huo ni UVUMI na uongo mkubwa.

Professionals hawafanyi kazi namna hiyo. Eti mpaka KILA MTU analijua gari na KUKARIRI namba zao wakiwa katika SURVEILLANCE?
Huo ni uongo mkubwa.
Hao ni ni WAHUNI na wahalifu TU.
Period!
kwahyo TISS ni professionals sana?? kma ni professionals mbona almas zimeibwa kwa nusu karne hawakuzuia?? mbona twiga walisafirishwa hawakuzuia.? makinikia je???

hii nchi bhana kila mtu anageuka security expert consultant
 
Hata kama mtu si security expert ama consultant kama ulivyosema. Hata basics tuunaweza kujua uongo na ukweli.
Sijui kama TISS wamepungukiwa na magari na budget yao ni ndogo kiasi cha kutumia gari lilelie basi afazali waongezewe budget ili wafanye kazi vizuri.

Hii ni too AMATEURISH/ Ya USANII na maigizo.
Haiingi akilini.

Mambo ya Almasi na uliyoyasema nafikiri kuna taasisi mbali mbali zinazoweza kufanya kazi pamoja na si kutegemea kitengo kimoja.

Ndo naomba ujiulize.
Kwa nini Mh. Rais Aliomba bunge lichunguze haya na si TISS?
Ukipata jibu basi rudi tujadiliane.
 
Polisi wetu wanapenda mteremko hawataki kujituma asee
 
Wana JF na Moderators,
Watu tunajaribu uanzisha thread kuonyesha mwanga ambao utamsaidia IGP Sirro na Polisi kupata vyanzo vya kuwabaini wahusika wa tukio la kumshambulia Tundu Lisu. Ajabu ni kuwa JF moderators wanaunganisha threads zingine ili kupoteza lengo!!
Nimeweka uzi hapa kusema IGP hayuko serious kuwasaka wahalifu hawa kwasababu tayari Lissu na Nnape walishawahi kupeleka malalamiko kwa IGP na hakuchukua hatua. Je, IGP alikuwa anasun=biri watu wafe kwanza ndipo achukue hatua??
IGP amesema ameshatuma Polisi Dodoma wenye weledi katika upelelezi wa kukamata wahalifu wa tukio kama hilo. Lakini hapohapo tunaambiwa Polisi kwa maana ya RPC Dodoma anataka mtu mwenye ushahidi apeleke Polisi. Huu ni ujinga na upuuzi...!. Kwanini Polisi inataka kutumia raia au Wananchi kubaini hawa wahalifu??
Polisi wamesomea hiyo kazi na wanalipwa mshahara kwa kazi hizo. Kwanini wasumbue wananchi kusaidia kuwabaini hao wauaji?? Kama Lissu na Nnape walishatoa taarifa Polisi na hawakuchukua hatua nani watamwamini akiwapelekea taarifa leo kuhusu tuhuma hiyohiyo iliyolalamikiwa tena na mhanga wa tukio???

Siungi mkono kutaka eti kuwahoji Dreva wa Tundu Lissu na Katibu Mkuu CHADEMA ati wamesema wanawajua wahusika. Hii haingii akilini hata kidogo. Kwanini IGP hataki kumhoji Nnape au Hussein Bashe wote Wabunge wa CCM ambao walishafuatiliwa na kutishiwa kuuawa??Polisi lazima wajue Dreva wa Lissu naye alikuwa mhanga maana zile risasi 32 hata yeye zingelimpata na nina hakika atakuwa bado yuko kwenye shock(mshtuko). Unapomwita kumhoji dreva kwa vile aliona ile gari yenye tinted iliyorusha risasi naona humtendei haki na hakuna weledi wowote hapo isipokuwa ni ubabbaishaji unao ongeza hasira kwa watanzania.

IGP na timu yake wajitafakari vinginevyo waachie ngazi. Wanachofanya ni usanii na kucheza na akili za Watanzania. Polisi hawana nia ya kuwakamata wahusika na hapo ndipo tunaporudi nyuma na kutafakari kwamba Polisi au TISS wanajua kinachoendelea...!! Kumhoji KM Mashinji au Dreva wa Lissu ni kutaka kupoteza lengo na kujiridhisha kama kweli hawa 2 wameshawabaini wahusika ambao wako ndani ya system ili wapate mbinu za kujipanga ili kuinusuru Serikali isiaibike,

Kwa kifupi ni kwamba Polisi hawatakamata mtu yeyote watakayemkamata zaidi ya ubabaishaji na mwisho wa siku jambo hili litaachwa hewani tu kama ilivyotokea kwa Ben Saanane.
Inasikitisha sana lakini Mungu yupo na anajua kila kitu toka A-Z na kuna siku haya yote yatawekwa bayana....!!
 
Hao walilipoti polisi hayo yote uliyoandika juu yao? Embu weka na namba za mashitaka yaobkwanza then tuendelee.. hata ya Lissu weka. Hao wote wahojiwe hadi wajue kuacha kudandia mengine na kusingizia wengine.. watahojiwa tu.. sio kukimbilia kutaka kuficha wanayojua.

Dereva anasakwa sasa hivi kaambiwa ajitokeze kuhojiwa.. so subiri uone aibu itakavyowapata wengi wadaku na wanaopenda kusingizia serikali na Raisi wetu mpendwa juu ya kila kitu.
 
Rais yeye IGP yeye waziri yeye bunge yeye mahakama yeye..

Mnategemea kuwa na IGP gani zaidi?...

I think i could be IGP...
 
Hao walilipoti polisi hayo yote uliyoandika juu yao? Embu weka na namba za mashitaka yaobkwanza then tuendelee.. hata ya Lissu weka. Hao wote wahojiwe hadi wajue kuacha kudandia mengine na kusingizia wengine.. watahojiwa tu.. sio kukimbilia kutaka kuficha wanayojua.

Dereva anasakwa sasa hivi kaambiwa ajitokeze kuhojiwa.. so subiri uone aibu itakavyowapata wengi wadaku na wanaopenda kusingizia serikali na Raisi wetu mpendwa juu ya kila kitu.
Tupishe tafadhali..
Wewe ni mmoja wapo wa lile kundi tuhumiwa.
 
Hivi kwa mfano nikaenda Dodoma nikasema muhusika ni Sizonje kitakachofuata ni nini? Hawa polisi wetu ni bure kabisa

Mwisho wa siku watasema aliyempiga Lisu risasi ni fundi seremala
 
Hao walilipoti polisi hayo yote uliyoandika juu yao? Embu weka na namba za mashitaka yaobkwanza then tuendelee.. hata ya Lissu weka. Hao wote wahojiwe hadi wajue kuacha kudandia mengine na kusingizia wengine.. watahojiwa tu.. sio kukimbilia kutaka kuficha wanayojua.

Dereva anasakwa sasa hivi kaambiwa ajitokeze kuhojiwa.. so subiri uone aibu itakavyowapata wengi wadaku na wanaopenda kusingizia serikali na Raisi wetu mpendwa juu ya kila kitu.
Anayekulala ana Kazi kuliko askari Jela!!

ACHA nikae KIMYA...!
 
Back
Top Bottom